Aina
hii Malware inayojulikana kama Tyupkin yaleta maafa katika mashine za ATM.
Tyupkin imekua ikisambazwa na kundi la wahalifu mtandao kutokea ulaya mashariki
na kusababisha pesa nyingi kuweza kutoka kupitia ATM mashine ambapo tayari
wataalam wa usalama mitandao kutoka Kaspersky Lab wakishirikiana karibu na
polisi wasio na mipaka “Interpol” wamesha anza oparesheni ya pamoja kutafuta
chanzo na ugunduzi katika mashine 50 umebainika hadi sasa.
Video
inayo onyesha kilichotokea kwenye Mashine Hizo:
Uchunguzi
wa kina umeonyesha Mashine zilizo athirika zimekua zikigundulika kuwa na Window
XP yenye 32-bit ambayo tayari Microsoft walisha tahadharisha watumiaji wake.
Utafiti unaonyesha Mashine nyingi za ATM bado zimeendelea kutumia Window XP
ambapo imekua ikirahisisha sana kuingiliwa na wahalifu.
Tahadhari
imeendelea kutolewa katika maeneo mengine kwani ingawa kunajitihada za dhati za
kukabiliana na Tyupkin bado inaonekana kusambaa katika maeneo mengine mbali
mbali duniani na hofu ni kubwa kua huwenda Afrika ikaonekana kua ni enoo jipya
litakalo athirika.
No comments:
Post a Comment