Kampuni
ya Microsoft imetoa angalizo kwa wateja wake ambao bado wanatumia “Window XP”. Kampuni
hiyo imeeleza kuwa hapatakuwepo na “updates” zaidi kwenye “Window XP Service
Pack 3” baada ya mwezi wanne mwaka 2014.
Akiongea
na wataalam mbali mbali wa maswala ya ulinzi mtandao August 16 Mwaka 2013,
Bwana Tim Rains alisema “Ingawa Window XP wakati imetolewa ilikua ni yenye ubora
na yenye kupendwa zaidi, kwa sasa imekua
ni dhaifu kutokana na ongezeko la uhaifu
mtandao”
Aliongeza
na kusema Mara baada ya kuacha kuendelea kuihudumia Window XP wahalifu mtandao
“Hackers” watatumia mianya hiyo kuweza kuingilia Komputa za wateja wao ambao
watakua wanaendelea na matumizi ya Windo XP huku akiendelea kusisitiza Windows
mpya ambazo zimekua ziki endelea kutolewa na Kampuni hiyo Ya Microsoft
zimeendelea kutafutiwa suluhu pale tu inapo onekana wahalifu mtandao wameweza
kugundua namna ya kupenyeza na kuweza kuingia katika Komputa za watu bila
ridhaa yao bodhaa zao za Microsoft.
“Kwa
sasa Microsoft Security Response Center imekua ikotoa “Updates” kwa wateja wao ili
kuwalinda dhidi ya wahalifu wenye nia ya kupenya kwenye komputa zinazotumia
bidhaa zao. Ifikapo tarehe 8 ya Mwezi wa Nne mwaka Huu wa 2013, Makampuni
ambayo bado yatakua yanatumia Window XP wahalifu mtandao “Attackers” wanaweza
kuwa na namna ya kutafuta mapuungufu katika Window XP ambapo baadae wanaweza
kutumia mapungufu hayo kuleta athari na Kampuni ya Microsoft haitakua na
usaidizi wa bure au wa kulipia ndidi ya hali hiyo kwani tayari itakua imekwisha
acha kutoa msaada dhidi ya Window XP” alisema bwana Tim Rains.
Wachangiaji
wa mada hiyo waliweza kuonyesha Hisia tofauti dhidi ya angalizo hilo, Na tulipo
zungumza na bwana Yusuph Kileo ndidi ya Taarifa hiyo alisema, “Naimani kabisa
Tarehe zitafika nabado baadhi ya Makampuni yataendelea na matumizi Ya Window
hiyo ambapo huwenda ikaongeza urahisi wa wahalifu kupenyeza katika mifumo mbali
mbali inayo tumia window Hiyo ya XP ingawa Microsoft tayari wamesha tangaza ya
kua msaada zaidi katika Window XP hautakuwepo na huwenda ikawa ndio sababu ya
wahalifu kuanza kutumia mwanya huo kuingilia Komputa za watu wenye matumizi ya
Window hiyo ya XP”
Aidha
kwa taarifa nyingine, Tarehe 19 Ya Mwezi wa nane 2013 Jijini California Nchini
Marekani Jaji Charles Breyer wa mahakama ya Wilaya jijini humo ametoa hukumu
kwa watumiaji wa mitandao ambao wamekua na tabia ya kubadilisha IP (internet
protocol) au kuwa na matumizi ya “Proxy server” kwa malengo ya kuzingilia
Tovuti nyingine “Public Websites”.
Katika
kesi hiyo iliyo husisha makampuni mawili ya nchi hiyo yaliyo jilikana kama “Craigslist”
pamoja na “3taps” Jaji huyo Alifafanua
kwa kusema mtumiaji anapokua na tabia hiyo atakua amekiuka kipengele cha katiba
ya nchi hiyo kinachojulikana kama CFAA “Computer Fraud and Abuse Act”.
Alipo
ulizwa bwana Yusuph Kileo kuhusiana na tukio hilo alizungumza na kusema
“Kilichotokea katika kesi hiyo ni kwamba 3taps wali ingia kwenye Kampuni ya
Craigslist kwa kubadilisha IP(Internet Protocol) yake na kutumia “Proxy server”
ili kuficha utambulisho wake “Identity” huku wakichukua taarifa kutoka katika
kampuni ya Craiglist ndipo Graiglist
walipo fungua mashtaka dhidi ya kampuni ya 3taps.
Baadae jaji ndipo alipo toa hukumu kenye kesi
hiyo aki nukuu moja ya sheria ya nchi hiyo inayojulikana kama CFAA” ambapo Sheria
hiyo inaelekeza kuingia hatiani kwa yeyote atakae ingilia Komputa ya mwingine
bila ridhaa na kuchukua taarifa zozote.
Sheria
hiyo ni ya “18 USC § 1030 - Fraud and related activity in connection with
computers” kipengele cha (a) (2) (c) inayo eleza “Whoever intentionally
accesses a computer without authorization or exceeds authorized access, and
thereby obtains information from any protected computer . . . . ”
Aidha
Bwana Yusuph Kileo Alieleza jambo jingine ambapo anategemea kumpokea mgeni ambaye
ndie Mmiliki wa Wolfpack Security na
Director wa SANS- Africa pia ni
Mwenye kiti wa Kundi Linalojihusisha na Ulinzi mtandao katika Nchi za
Africa ambapo yeye ni mwanachama wake wa kudumu. Mgeni huyo anategemewa
kuwasili Nchini jioni ya tarehe 12 September 2013 na Kuondoka Nchini Tarehe 13
September 2013.
Aidha
bwana Yusuph Alieleza Mgeni huyo Anategemewa kuhudhuria Chakula Cha jioni na
Wataalam wa Tanzania katika Fani ya TEHAMA Ambapo watapata fursa yaku
badilishana mawazo.
Pia
anategemewa kutoa mafunzo mafupi siku inayofatia na kasha kupata kuzungumza na
baadhi ya Wadau nchini ili kuweza kubadilishana mawazo kuhusiana na hali ya
uhalifu mtandao katika ngazi ya afrika na Dunia Kwa Ujumla.
Itakua
Ni fursa kwa wataalam wa kitanzania Kuweza kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja
na mtu huyu adimu ambae amekua mwandalizi na mfunguzi mikutano inayo wahusisha waatalaam wa maswala ya ulinzi
mtandao na Uchunguzi wa makosa yadigitali ambaye pia ni mwanachama wa Wataalam wa ulinzi mtandao na Uchunguzi wa
makosa ya Digitali Duniani.
Source: Mwananchi Jumanne August 27 2013.
Source: Mwananchi Jumanne August 27 2013.
No comments:
Post a Comment