Mkutano
Mkuu ulio washirikisha wataalam wa sekta ya teknologia katika ngazi ya kidunia
umemalizika salama na kuna mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina .
Kwa kifupi yaliyojiri katika mkutano huo ni pamoja na :-
Kwa kifupi yaliyojiri katika mkutano huo ni pamoja na :-
1. Mapitio
ya takwimu za makosa mtandao kwa kina katika mwaka huu. Mjadala ulibobea zaidi
katika, nini hasa sababu ya makosa haya kuonekana kukua na nini kifanyike ili
kupunguza kasi ya ukuwaji makosa haya.
2. Namna
ya utumaji wa “Key” ambazo zimetumika kuficha maneno “Encryption Key” ili
kuweza kuongeza wigo wa usiri katika taarifa zinazo safirishwa kupitia
mitandao.
3. Hali
halisi katika Teknologia mpya ya “CLOUD COMPUTING” na wasi wasi uliozuka juu ya
usalama wa taarifa zinazopokea huduma kupitia teknologia hiyo. Pali jadiliwa
kwa kina usahihi wa hilo na nini kifanyike.
Bwana Yusuph Kileo akiwa na Steven “FOUNDER” NA “CEO” wa Cloud perspectives (Cloud computing) Nje ya Ukumbi wa mkutano mara baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya kikao hicho |
5. Mjadala
wa kina kuhusiana na “Social media” na jinsi inavyoweza kusaidia kuelimisha
jamii na kuleta mabadiliko chanya. Pia Namna ya kusaidia kuboresha na kuhimiza
matumizi bora ya mitandao hiyo ya kijamii “Control mechanism to social media”4. Changamoto
zilizopo katika ukusanyaji na uchunguzi salama wa vidhibiti vya makosa ya
Digitali “Digital forensics collections and investigations”
6. Mjadala
wa kina katika matumizi ya Open source security info management (OSSIM) ambapo
inatoa msaada mkubwa katika ulinzi wa mtandao ambapo mjadala huu ulifunguliwa
na mhakiki mkuu “Chief editor” wa kitabu maarufu kinacho tumika sana katika
ulinzi mtandao kiitwacho “Cyber security standard”.
|
7. Mjadala
Mwingine Kuhusiana na Teknologia Mpya ya Miwani ambayo inauwezo wa kuchukua
taarifa kwa njia ya sauti na video na kuzisafirisha taarifa hizo kwenda sehemu
nyingine. Tuliangali jinsi gani wa halifu sasa wameanza kuitumia vibaya
teknolojia hiyo na umakini unahitajika kiasi gani.
8. Mkuu
wa MENA, alifafanua juu ya ukuaji wa teknologia kwa sasa na kusisitiza mafunzo
ya mara kwa mara ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknologia.
9. Umuhimu
wa kuelimisha jamii kua swala la ulinzi mtandao si jukumu la kundi Fulani bali
ni jukumu la kila mmoja ilitumika kauli “ inaanza na wewe mimi na wengine wote,
kwa pamoja tutaweza kupunguza hali mbaya ya makosa mtandao”
10. Aidha
mjadala shirikishi kuhusiana na “Kifaa kipya kilichoko katika hatua za awali
katika utafiti ambacho kitatumia teknologia kuweza kutoa tiba ya ugonjwa wa
saratani “Cancer” ambacho kinategemea kupunguza madhara mengi yaliyopo kwa sasa
ikiwemo kuondoa swala la mgojwa kunyolewa kipara.
No comments:
Post a Comment