Kushirikiana katika maswala mbali mbali ili kuweza kufikia malengo ni jambo kubwa lililopata kusikika katika mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka unaoendelea Nchini Kenya unaojadili changamoto mbali mbali za sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Swala la usalama katika mitandao limepata kuangaliwa na changamoto mbali mbali katika mijadala Rasmi (Ndani ya Kikao) na isiyo rasmi (tuwapo nje ya ukumbi wa mkutano) zilipata kuangaliwa kwa ukaribu.
Swala
uhimu nililo jifunza ni jinsi uhalifu mtandao katika mataifa haya mawili Kenya
na Tanzania yanavyo fanyika na kujua ya kua kubadilishana mawazo katika hili
litasaidia kujipanga kukabiliana na uhalifu mtandao ambao tayari kwa nchi ya Kenya
umeendelea kukua ikiwa bado kwa Tanzania haujaonekana sana huku Kenya
Ikijifunza pia ili kuweza kujipanga kabla ya uhalifu usika kuweza kushika kasi.
Namna
mbali mbali zinazotumika na wenzetu wa Kenya ambao wameathirika sana na uhalifu
mtandao (Mfano: Wakati Mkutano unaendelea – Baadhi ya mifumo mtandao ya
serikali iliripotiwa kuangushwa na wahalifu mtandao) kwenye kukabiliana na
uhalifu mtandao huku tukiangalia kwa karibu namna ambavyo teknolojia
zinazotumika kupambana na uhalifu mtandao katika nchi hiyo zinavyoweza kutoa
msaada wa kina kwenye makabiliano na uhalifu mtandao Nchini Tanzania.
Hii
nifursa nzuri kwa wa Tanzania kuweza kujipanga na kujenga tabia ya kukusanya
Guru wa maswala ya TEHAMA ili kujadili changamoto mbali mbali na namna
tunavyoweza kutumia wataalam wandani kuweza ku ongeza tija kwenye maswala mbali
mbali hususan maswala yahusuyo usalama mitandao kwani tulikubaliana kwa pamoja
maswala ya usalama mtandao yamekua changamoto kubwa na yamepelekea kutakiwa
kupatikana nguvu ya ziada na pamoja kukabiliana nayo kwa kushirikiana ki mawazo
na njia mbali mbali zinazoweza kusaidia katika mapambano dhiidi ya usalama mitandao.
Hili
linatokana na uhalisia wa kua Uhalifu mtandao hauna kizuizi, Mhalifu anaweza
kuwa popote duniani na kufanya uhalifu katika sehemu nyingine yoyote kwa kuleta
madhara makubwa sana. Sambamba na hili ni kuwa kila siku teknolojia inakua na
aina mpya za uhalifu zinaibuka katika mataifa mbali mbali hivyo kushirikiana
taarifa zinaweza kuongeza tija kwenye makabiliano na uhalifu mtandao.
Mwisho
Kabisa ni Wito kwa Wataalam wetu wa ndani. TEHAMA inakua kila kukicha na
teknolojia kwa ujumla inabadilika mara kwa mara hivyo hatuna budi kuweza
kushiriki katika makongamano na mafunzo mbali mbali ya kila mara ili kuweza
kujiongezea uwezo wa maswala mapya ambayo yanaweza kutufanya tukaendana na
wakati katika maswala ya TEHAMA. Picha zaidi za Mkutano huu zinapatikana "HAPA"
No comments:
Post a Comment