Nchi
ya Tanzania imepata bahati ya kipekee kuwa mwenyeji wa warsha ya Kimataifa ya
maswala ya usalama mitandao iliyo shirikisha mataifa mbali mbali kujadili na
kuongezeana uwezo wa jinsi wa kukabiliana na changamoto kubwa katika maswala ya
uhalifu mitandao.
Warsha
hii imekuja muda muafaka baada ya taarifa niliyo iandikia "HAPA" niliyo himiza
na kuonyesha umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za pamoja kwenye vita dhidi ya
uhalifu mtandao ikizingatiwa uhalifu mtandao ni uhalifu usio mipaka na kuna
mahitaji makubwa ya kushirikiana katika taarifa na utaalam.
Warsha
hii imekua na mafanikio makubwa sana ambapo nikiwa kama mtaalam wa maswala ya
usalama mitandao na uchunguzi wa makosa ya digitali naweza kusema ni mengi tumeweza
kubadilishana na uwezo wa kuendeleza
mapambano zaidi dhidi ya uhalifu mtandao umeongezeka kwa washiriki wote.
Wito
Mkubwa ulitolewa na katibu mkuu wa wizara ya sayansi mawasiliano na teknolojia
nchini profesa Patrick Makungu kuwataka wataalam na washiriki wengine kutochoka
na kuongeza jitihada kukabiliana na wimbi la uhalifu mtandao linalokua kwa kasi
duniani kote ili kuweza kuwa mbele ya wahalifu mitandao kupitia hotuba aliyo
isoma kwa niamba ya Waziri wa Wizara
hiyo kama inavyoweza kusomeka "HAPA"
Aidha,
Mkurugenzi mkuu wa COSTECH, Dr. Hassan Mshinda alifafanua umuhimu wa warsha na
kueleza nifursa nzuri sana kwa watanzania na kuanisha ni mikakati endelevu
yakuendelea kukuza uwezo wa wataalam wa ndani. Mimi binafsi pia nilipata
kujadili namna ya kukuza ushirikiano na wageni hao katika eneo hili muhimu la
usalama katika mitandao.
Mwezi
Octoba pia umeaswa kutumika vizuri ili kuweza kuhakiki uelewa wa maswala ya
usalama mitandao kwa watumiaji umeweza kufanyiwa kazi huku pakiainishwa
jitihada mbali mbali za serikali ya Tanzania inayo endelea nazo kuweza
kukabiliana na wimbi la uhalifu Mtandao nchini.
Taarifa hii imeweza kuandikwa kwa kifupi kwa lugha ya kingereza kama inavyoweza kusomeka kwenye gazeti la "DAILYNEWS"
Taarifa hii imeweza kuandikwa kwa kifupi kwa lugha ya kingereza kama inavyoweza kusomeka kwenye gazeti la "DAILYNEWS"
JOPO LA WANANDAAJI KUTOKEA WA WARSHA YA USALAMA MITANDAO KUTOKEA COMSAT WAKIBADILISHANA MAWAZO NAMI KUPANGA MIKAKATI ENDELEVU NA RAFIKI KUONGEZA UWEZO KWA WATAALAM WA NDANI |
No comments:
Post a Comment