WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday 17 March 2015

HOLLYWOOD WAZINDUA TAMTHILIA MPYA YA USALAMA MITANDAO

Nilipata kuzungumzia mchango mkubwa unaopatikana kupitia vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Tasnia ya filamu katika kutoa elimu ihusuyo maswala ya usalama mitandao. Hollywood wamekua wakiongoza katika kutengeneza vipengele mbali mbali vyenye kutoa ufafanuzi wa makosa mtandao yanavyo tendwa na namna ya kutambua na kujikinga.

Hatua yao hiyo imekua ikipongezwa sana na wataalam wa maswala ya mitandao duniani kote huku tukisistiza mataifa mengine yaweze kuiga juhudi hizo. Kuungana na wataalam wengine nilipata kuandika Makala ya kingereza inayosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”, Makala iliyofanya vizuri na baadae kupatikana katika gazeti moja la ughaibuni linalotoka maramoja kila mwezi.

Mwezi huu wa tatu Hollywood wameamua kuzindua tamthilia maalaum iliyopewa jina la CSI: CYBER ambapo imejikita katika maswala ya usalama mitandao. Katika tamthilia hiyo inatoa mafunzo mbali mbali kwa kuonyesha makosa yanavyo fanywa na namna ya upelelezi wa makosa hayo unavyo fanyika pia.

Mwandaaji wa Filamu Hiyo Amekiri kua kilicho mvutia kuifanya si tu hamasa kutoka kwa wataalam wa usalama mitandao bali pia ni pamoja na uhalisia kua kila siku ni lazima habari za uhalifu mitandao zitengeneze vichwa vya habari huku akiamini wengi wata tamani sana kuona filamu ihusuyo mambo wanayosikia sasa katika vyombo mbali mbali vya habari yahusuyo uhalifu mtandao.

Tamthilia hiyo imepongezwa na wataalam wa maswala ya usalama mtandao ambapo katika forum za mijadala mbali mbali tunayoendelea nayo imekua ikipewa uzito wa pekee kwa kupongezwa na kuambiwa imekuja muda muafaka kwani tayari athari za uhalifu mtandao zimesha mgusa kila mmoja kwa namna moja au nyingine.

Tamthilia hiyo imemshirikisha mwanamziki maarufu “SHAD MOSS” – anaejulikana sana kwa jina la BOW WOW na wasanii wengine wenye uwezo mzuri wa kuigiza. Tamthilia hiyo inategemewa kufanya vizuri sana na kufanikisha malengo ya kufikisha ujumbe kwa idadi kubwa ya watu.


Naomba nirudie tena kusema, Imefika wakati sasa kwa Tanzania kuihusisha tasnia ya filamu nchini kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na maswala ya uhalifu mtandao, jinsi ya kugundua na kukabiliana nayo ili kuongeza wigo wa uelewa kwa jamii nchini kwani inaaminika kupitia filamu darasa linaeleweka zaidi kwani wana filamu wananafasi kubwa sana katika kutoa elimu mbali mbali katika jamii.

Vita dhidi ya uhalifu mtandao si vita ya kundi fulani la watu au aina fulani ya watu bali ni swala linalo anzia katika ngazi ya mtu binafsi na kuonganisha nguvu ili kuhakiki taifa na dunia kwa ujumla inakua salama kimtandao.


Kwa kuzingatia Hili natoa wito kwa jamii ya kitanzania kutambua hali hii ya uhalifu mtandao na kuhakiki jitihada za dhati zinachukuliwa mapema bila ya kungoja hali kuwa mbaya kiasi cha kuwa na ugumu kupata suluhu ya jinsi ya kukabili uhalifu mtandao nchini.

Sehemu ya kwanza ya tamthilia hiyo inaweza kutazamwa kwenye video hapo chini

1 comment:

  1. Hi Brother Kileo, Hii ni maneno poa sana nimekua nikifatilia unacho write na na vutiwa sana na unavyo weka maneno.
    Mimi ni Silvia wa KE.

    ReplyDelete