Katika
Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa
katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL
INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa
misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo
yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.
Aidha,
Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa
technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia
97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa
na dosari ya kipekee.
Itakumbukwa
India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo
alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana
na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.
Katika
Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati
ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na
tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo
tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.
Katika
mazungumzo yangu maalum yaliyo ambatana na mahojianao na vyombo vya habari katika kuangazia dhamira yao hii ya kukabiliana na uhalifu
mtandao kupitia wizi wa ATM, Nilipata kuunganisha mawazo na kujua namna gani
Taifa la Tanzania tunaweza kuwekeza zaidi kukabiliana na hali hii ambayo pia ni
tishio katika Mabenki yetu.
Moja
ya mambo muhimu katika hili ambalo nimeona nililete nyumbani ni kuhakikisha
tunaongeza aina ya tatu ya utabulisho katika miamala inayofanyika hivi sasa ya
kifedha katika ATM zetu zote za mabenki yote. Hili litaongeza usalama katika
miamala na pia tayari mataifa yaliyo jaribu aina hii ya suluhisho katika wizi
mtandao imeanza kuonyesha matunda.
Natoa
Wito kwa mabenki kuangazia hili, na pia na imani kubwa mabenki ya Tanzania yatakaa
na kutafakari njia hii rafiki ya kuhakikisha miamala ya wateja wao inaweza
kubaki salama ili kuongeza imani kwa wateja wao juu ya fedha zao na wao
kutopata hasara kubwa inayopatikana hivi sasa kwenye miamala ya biashara kupia mashine
za ATM.
No comments:
Post a Comment