WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 22 May 2017

KUENDELEA KUKUA KWA UHALIFU MTANDAO - NANI WA KULAUMIWA?

Kumeendelea kukua kwa uhalifu mtandao maeneo mengi duniani – Huku baadhi wakitafsiri hili linatokana na wana usalama mtandao kuonekana kulemewa (Kuzidiwa) na wahalifu mtandao.

Hili limepingwa katika kikao kilicho kamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, Nchini Afrika kusini ambapo binafsi nilishiriki na kuzungumza na wenzangu kuhusiana na namna sahihi ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao – Kubwa nililozungumzia ilikua ni kuwa rudisha wenzangu kwenye mstari kwa kuwakumbusha juu ya taratibu tulizojiwekea na zinazo takiwa kufatwa na mataifa yote duniani.

Pamoja na mambo mengine, nilikumbusha umuhimu kuhakiki hatua zote za uchunguzi zinakua katika maandishi – Zaidi, nilicho zungumza pia kinaweza kupatikana katika Habari inayoweza kusomeka “HAPA”

Kuhusiana na ukuwaji wa uhalifu mtandao kila mmoja wetu amekiri hili halisababishwi na wana usalama mtandao  kuzidiwa nguvu – Lawama imeonekana kuelekezwa kwa mataifa mbali mbali pamoja na watumiaji wa mwisho “Users”.