WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Saturday 22 December 2018

SHUTMA ZA UJASUSI MTANDANO DHIDI YA UCHINA



KWA UFUPI: Australia, Marekani na Uingereza zimeitupia lawana nchi ya Uchina kuhusika na ujasusi mtandao katika mataifa yao na mataifa Rafiki – Shutma ambazo zime eleza uchina kuhusika na wizi wa taarifa za siri za kibiashara za serikali na makampuni ya Teknologia.
---------------------------
Niliwahi kueleza mara kadhaa mwelekeo mpya na hatari wa Uhalifu mtandao ambapo nilitahadharisha kuhusiana na vita mtandao (Cyber Warfare) pamoja na Ujasusi Mtandao (Cyber Espionage) ambavyo kwa sasa mataifa makubwa yanawekeza zaidi kwenye matumizi ya teknolojia kudhuru na kuingilia mataifa mengine kimtandao.

Kundi la APT-10 la uchina limeshutumiwa na Uingereza na Marekani kuingilia makampuni takriban 45 ya Teknolojia, Taarifa za wafanyakazi takriban laki moja za wanajeshi wa majini wa marekani pamoja na computer mbali mbali za shirika la NASA.



Zhu Hua pamoja na Zhang Shilong, ambao ni raia wa Uchina wameshtakiwa na Marekani kuhusika na kufanya mashambulizi mtandao kwaniaba ya wizara ya ulinzi ya uchina (Chinese Ministry of State Security) – Naibu Mwanashria mkuu wa Marekani , Bwana  Rod Rosenstein alielezea shutma hizo.