Uhalifu
mtandao umeendelea kua changamoto maeneo mengi Duniani.Taasisi za kifedha,
Usafirishaji, Nishati,na maeneo mengine mengi yameendelea kukabiliwa na matukio
ya kihalifu mtandao huku athari zake kuendea kukua kila kukicha.
-------------------
NEWS UPDATES:
Following a pair of breaches, LINODE is now changing user procedures to improve
security. The web hosting company was the target of two breaches over the past year.
Both incidents, one in July 2015, the other in December 2015, involved stolen
customer account access credentials. In response to the December breach, Linode force-reset all customer
passwords. The company is changing authentication procedures to separate
customer application from credentials. Linode is also employing credit card
tokenization, and altering its internal policies with guidance from a NIST
framework.
-------------------
Mataifa
mengi yameendelea kuwekeza kwenye Vitendea kazi (Vizuizi - Tools), Kuimarisha
ushirikiano ndani na kuvuka mipaka ya Nchi (Collaboration) kuongezea elemu
wataalam wa kukabiliana na uhalifu mtandao (Capacity building) huku sheria za
uhalifu mitandao zikionekana kuboreshwa zaidi kwenye mataifa mengi. Yote haya
yakiwa ni hatua za kukabiliana na uhalifu mtandao.
Ifahamike,
Elimu ya uelewa ndio SILAHA kuu – Mataifa
mengi bado Imekua ni Nadra kuona mikakati Madhubuti ya elimu ya uelewa (Awareness)
stahiki na endelevu itakayo mpa fursa Mwananchi wa kawaida kuweza kujikinga
binafsi na kufahamu namna ataweza kutatua tatizo pale atakapo kabiliwa na
uhalifu mtandao.
Kulitambua hili Katika kukabiliana na uhalifu mtandao jambo la kwanza limekua
ni kuhamasisha elimu ya uelewa. Na katika maazimio 11 ya mwaka jana Elimu ya
uelewa ilikua ni azimio la kwanza. Aidha, Wataalam wa usalama mitandao
wameendelea kutengeneza Video, Katuni, Michezo na mengineyo yenye malengo ya
kukuza uelewa kwa jamii juu ya matumizi salama ya mifumo yetu ya Ki TEHAMA.
Pamoja
na jitihada hizi na kupatikana mwezi maalum wa kukuza uelewa (Octoba) bado
pameonekana changamoto kadhaa zinaz sababisha elimu hii ya uelewa kutotoa
matunda tunayotegema.
Mosi,
Elimu ya uelewa imekua si endelevu – Unaweza kukuta shirika/Kampuni na hata
Taifa linakua na elimu ya uelewa kwa wakati Fulani na baadae kusahaulika
kabisa. Na maeneo mengi unakuta Mwezi Octoba pekee ndio elimu ya uelewa
inatolewa zaidi huku miezi mingine pakiwa hakuna elimu hii.
Nini Kifanyike,
Elimu ya Uelewa lazima iwekewe taratibu maalum Walau kila baada ya miezi mitatu
na ikiwezekana Katika Vikao vya asubuhi Makazini Kwa Wiki Mara Moja kutolewe
elimu hii.
Pili,
Elimu ya uelewa kukosa ubora – Kutokana na Msisitizo ambao upo wa kuhakiki
elimu ya uelewa inatolewa, wanao tekeleza hili wamekua hawafati Maelekezo
sahihi ya namna ya kufikisha elemu hii kitu kinachopelekea kuona elimu hii kuwepo
bila mafanikio kuonekana.
Nini Kifanyike,
Kama ilivyo katika mambo mengine – Elimu ya uelewa ina taratibu zake za namna
ya kuifikisha kwa walengwa ili kuweza kuonyesha matokeo tegemewa. Ni lazima
taratibu hizi ambazo tumekubaliana kimsingi baina ya wataalam kote duniani
kufatwa ili kuhakiki elimu husika inakua na ubora stahiki na tunafikia malengo
tegemewa.
TANZANIA:
Moja ya mambo kadhaa ambayo nimekutana nayo ninapo shiriki katika mijadala au niwasikilizapo
wadau/wanachi wanapo zungumzia swala la usalam mtandao – Kilio Kikuu imekua ni
kukosekana elimu ya uelewa. Mfano Ni mjadala Unaoweza kusomeka kwa “KUBOFYAHAPA”
Ki
Uhalisia elimu kwa kiasi chake imekua ikitolewa lakini haifikii Malengo
tarajiwa kutokana na kutokidhi vigezo – Imekua ikitolewa kimazoea tu bila
kufata taratibu stahiki ambazo zimekubaliwa kimsingi na wataala wote kutoka
maeneo yote duniani. Na Hili ndio tatizo kubwa. Hatuna budi kubadilika.
Elimu
ya uelewa inapotolewa ipasavyo na ikaonyesha matunda tegemewa ina uwezo mkubwa
wa kupunguza uhalifu mtandao Nchini kwa takriban Asilimia 75%.
Nilipata
andikia makala Ndefu yenye ufafanuzi wa Njia Madhubuti ya kukabiliana na
uhalifu mtandao inayoweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA” ambapo nilianisha mambo
mengi ya kuzingatiwa na umuhimu wa elimu hii kwa jamii zetu.
Natoa
Wito – Elimu hii ya Uelewa iweze kupewa kipaumbele stahiki ikiwa ni silaha
tosha ya kukabiliana na uhalifu mtandao Nchini ambao unaonekana kutaka kuanza
kushika Mizizi.
When was Your Last time you updated your Password? - Lini Ilikua mara yako ya Mwisho kubadili neno lako la siri?
No comments:
Post a Comment