Wanausalama
mtandao kote duniani walikamilisha tukio muhimu sana linalofanyika kila mwezi
Oktoba (Cybersecurity Awareness Month) lenye dhamira ya kukuza uelewa wa
matumizi salama ya mitandao huku ikiaminika kupitia tukio hilo uhalifu mtandao
unaweza kupunguzwa kwa asilimia kubwa. Mataifa mengi yakiwa na mafanikio
makubwa kutokana na hili ambapo Tanzania pia kupitia baadhi ya Makampuni ilipata kushiriki.
Wakati
bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na
uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliofanyika kwa ubunifu na
umahiri wa hali ya juu ambapo wahalifu mtandao wamefanikiwa kusambaza kirusi
aina ya ModPOS kinacho athiri mashine zinazotumika kukamilisha miamala wakati
wa manunuzi.
Kirusi
cha ModPOS, kimegundulika Nchini Marekani wakati wa sherehe za “Thanks Giving”
ambapo watu wengi hufanya manunuzi. Kirusi hicho Kimekua kikifanikisha upotevu
mkubwa wa pesa wakati wa miamala.
Mara
baada ya ugunduzi huo wa ModPOS, mijadala kupitia mtandao ilianza baina ya
wanausalama mitandao ili kuweza kufanikisha mambo makubwa matatu. Moja ni
kuweza kugundua chanzo na jinsi ilivyo fanikishwa kuwepo bila kugundulika
(Inaaminika kimedumu muda – Taarifa ambazo bado zinafatiliwa) Pili, Ilikua ni
kutafuta suluhu ya kirusi hicho ili kiweze kuondolewa na Tatu, ni kupanga namna
ya kukuza uelewa wa namna ya kujikinga na janga hili la ModPOS.







