Nikizungumza
na kundi maalum katika vikao vinavyoendelea nimewasilisha ujumbe wa Tahadhari
ambapo Uma umetahadharishwa juu ya mashambulizi takriban Milioni hamsini (50 Milioni) duniani kote katika kipindi cha sikukuu yatakayo
gharimu kati ya Dola 50 – Dola 5’000 kwa kila shambulizi.
Matarajio
hayo ni kutokana na matumizi makubwa ya mtandao katika kufanya miamala mbali
mbali ya manunuzi ya bidhaa katika kipindi hiki cha sikukuu ambapo watu wengi
duniani kote wamekua wakinunua vitu mbali mbali kwa wingi kwa njia ya mitandao.
------------------------------
RELATED POST:
------------------------------
Kwa
mujibu wa ripoti ya kitelijensia ya matishio mtandao, iliyo wasilishwa na NTT
Security – Imeeleza uwepo wa takriban utengenezwaji wa tovutiMilioni moja na nusu zenye mlengo wa kurubuni kila mwezi ambazo baadhi yao zinadumu kati ya
masaa ma nne had inane na kutoweka. Hili niongezeko la asilimia 74 (74%) kulinganisha
na takwimu za miezi sita iliyopita.









