Monday, 17 February 2014
FORENSICS TOOL PRESENTATION.
Katika Video Hii utapata Kujifunza namna ya Utumiaji wa "Fornsics Tool" ili kufanya mambo mbali mbali katika uchunguzi wa makosa ya Digitali.
HALI YA USALAMA WA KIMTANDAO - 3
Sehemu ya pili Wiki
Iliyo pita nilizungumziwa kipengele cha Tatu, kuhusu barua pepe, kuna wimbi la
wahalifu mtandao ambao wanatumia anuani za watu na mitandao mingine ya kijamii
kuandika kwa watu wasiowajua ama kueleza wanahitaji urafiki au wako katika mazingira
magumu hivyo wanahitaji msaada fulani kutoka kwako. Usijibu barua kama hizi,
kwani chochote utakachojibu kinaweza kukuingiza matatani.
Kuna kitu kitaalamu
kinaitwa “Reconnaissance” ambapo ni hatua mojawapo inayotumiwa na wahalifu
kukusanya maelezo ya watu wanaotaka kuwadhuru.
Muendelezo wiki hii
katika sehemu ya nne, Matumizi
Ya ATM, Kua makini sana na mtu anae kuomba kuhamisha fedha zake kwenyye account
yako ya benk ili aweze kuitumia account yako kutoa fedha hizo kwani kwa sasa
wahalifu mtandao katika maeneo haya ya Wizi katika ATM wamekuja na njia hii
ambapo wanatengeneza mazingira ya uhitaji wa msaada wako kwa kukuuomba
wakutumie fedha ili account yako itumike kuzitoa huku wakijua wao watakua
salama na wewe Unaetumika account yako unaingia matatani bila kujua kwani
maranyingi hali hii inakua inahusisha pesa za wiizi. na Kwa sasa Wizi wa aina
hii umekua ukija kwa kasi na wengei ambao kwa namna moja au nyingine huwenda
hawakujua kua ni tatizo na mara baada yakutoa msaada huu wanajikua wameingia katika
hatia ya kujibu mashtaka ya wizi Mtandao.
Tano, Website Feki, Kwa sasa Takwimu imeongezeka sana ya
websaiti Feki Ambbapo Tumeliona hili katika mapitio ya Makosa ya kimtandao
yajayo kwa kasi katika kikao kilichofanyika Jijini nairobi mapema mwezi wa sita
mwaka huu. Ambapo Kumeonekana watu wamekua wakitengeneza website ambazo zinakua
zinafanana na za mabenk ambazo unapo ingia kwa ajili ya kufanya "Online
Transaction" unaweza kujikuta umeweka details zako ambazo ni pamoja na
Paswed yako kwenye Website feki ambapo Baadae wahalifu mtandao wanakusanya taarifa hizo kwa matumizi ya wizi wa fedha. Lakini pia Inaweza ikawa ni katika
website za kawaida za social media ambapo kikubwa ni kufanya uingize details
zako katika website feki yenye kufanana na uliyo izoea na mara baada ya kufanya
hivyo tayari wanakua wamepata wanacho kihitaji.
Kwenye hili Kuna Somo Refu kiasi ambalo linaweza kutoa
ufahamu jinsi gani utaitambu website ambayo si halali (Feki) Nategemea kulitoa
karibuni. Naimani litatoa muono kwa watu ili kkuweza kua makini zaidi baada ya
utambuzi. Pia Kwenye hili Kumekua pia na wimbi la watu wamekua waki tengeneza
accounts za mitandao ya kijamii kwa kuiga mtu mwingine kisha kutumia watu
urafiki kwa nia za kuiba taarifa za mtu muhusika. ni vizuri pia tukawa makini
kwenye hili.
Napenda kuhitimisha kwa kusema, Sikuzote unapokua katika
mitandao unakua si salama hivyo kunanjia nyingi ambazo wenzetu katika nchi
mablii mbali wamekua wakionyesha jitihada waau kupunguza hali ya kua hatarini
uwapo mitandaoni kwa ku weka taratibu mbali mbalii ambapo kwa sasa tanzania pia
itakua ikijittahidi kuweka taratibu hizo na pia kutoa mafunzo ya ufahamu kwa
wananchi ili kupunguza hali hii ya Makosa Ya Kimtandao ambapo yanakua kwa kasi
sana shivi sasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)