Unapo wadia mwisho wa mwaka wizi kupitia mtandao
umekua ukishika kasi zaidi – Mataifa mengi duniani yamekua yakikumbwa na wimbi
kubwa la uhalifu mtandao unao ambatana na upoteaji wa pesa. Itakumbukwa mwaka
jana kuelekea mwisho wa mwaka ndio kirusi kipya aina ya ModPOS kilionekana kwa
mara ya kwanza na kilifanikiwa kudhuru maeneo mengi na kusababisha kiasi
kikubwa cha fedha kupotelea mikononi mwa wahalifu.
Mwezi huu wa kuminamoja pekee tayari kumekua na
matukio mengi yenye mlengo wa kuwapatia pesa wahalifu mtandao. Kwa sasa Uhalifu
mtandao kpitia kirusi cha RANSOMWARE kinachoendelea
kushikakasi wamefanikiwa kupata mamilioni ya fedha. Kirusi hiki kinapelekea
mhalifu mtandao kumfungia uwezo mmiliki halali kutumia kifaa chake akimtaka
alipe kiasi cha pesa ili kurudishiwa huduma. Uhalifu huu umepiga hodi Barani
Afrika na hadi sasa wengi wameendelea kua waathirika.
Mifumo ya hospitali, mashule na watu binafsi ni
miongoni mwa waathirika wa kubwa wa uhalifu huu ambapo kila mfumo ulio fungiwa
na kirusi cha Ransomware ili kufunguliwa kiasi cha dola Miatatu (300) na zaidi
kimekua kiki hitajika. Kupitia matukio yaliyo ripotiwa duniani kote, takwimu halisi
ya pesa zilizo ingia mikononi mwa wahalifu mtandao kwa mwezi huu wa kuminamoja pekee
kutokana na Ransomware bado haija patikana ingawa ina kadiriwa kuzidi dola
milioni 829.
Aidha, Mabenki nayo hayako salama – Idadi ya Mabenki
yaliyo vamiwa kimtandao imeendelea kukua zaidi kuanzia mapema mwezi huu huku
hali hii ikitegemewa kuendelea zaidi maeneo mengi. Tukio kubwa zaidi kwa sasa
ni kutokea uingereza ambapo hadi sasa benki ya Tesco baada ya kushambuliwa
kimtandao zaidi ya Paundi milioni mbili zimeweza kupotelea mikononi mwa
wahalifu mtandao na benki hiyo imelazimika kuwalipa wateja wake.
Urusi nayo, kwa mwezi huu pekee kumekua na idadi
kubwa ya mabenki yaliyo vamiwwa kimtandao. Kwa undani wa hili taarifa ya awali
inaweza kusomeka HAPA – Imezungumzwa ya kua uchunguzi unafanywa,
Uchunguzi unategemea kueleza kama mashambulizi mtandao yaliambatana na kuibiwa
kwa fedha kwenye mabenki husika taarifa mpya zinaelezea hofu ya kua kuna kiasi
kikubwa cha pesa kitakua kimepotea pia inayo mabatana na hasara ya huduma
kukosekana kutokana na mashambulizi hayo.
Changa moto kubwa tulio nayo kutoka taasisi za
kifedha ni kutopokea taarifa na wakati mwingine matukio yanapo kua makubwa
taarifa inayotolewa inakua si sahihi – Inaficha uhalisia wa ukubwa wa tukio
kitu ambacho kinapelekea wahalifu mtandao kuendelea kushika kasi.
Mitandao yasimu hasa barani Afrika ambapo huduma za
kifedha kupitia mitandao ya simu inapatikana, napo kumekua na aina nyingi ya
wizi mtandao amabapo matukio ya watu kuibiwwa pesa yame endelea kushika kasi.
Kuna matukio mawili kwa kipindi hiki yamejitokeza nitayatolea
mfano hapa ili kukuza uelewa kwa watumiaji mitandao ya simu kua makini :–
Tanzania:
Nilifahamishwa na mtu ninae mfahamu mwenye huduma za uwakala wa fedha kupitia
mitandao ya simu ambapo alinieleza, kwaufupi – Alikua akiwasiliana na mtu
kupitia simu akimueleza ni mhusika kutoka kampuni moja ya simu nchini na kwenye
mawasiliano aliyo eleza alikua akiamini kabisa ni mtu sahihi yalikamilika kwa
mhusika kupoteza kiasi cha zaidi ya Milioni saba za kitanzania.
USHAURI
KWENYE HILI: Kwanza kabisa, tuwe na tabia ya
kujihakikishia tunao wasiliana nao ni watu sahihi hasa linapo kuja swala la
fedha kuhusika. Unaweza kulifanya hili kwa kuwasiliana moja kwa moja na huduma
kwa wateja au kwenda kwenye mtandao husika kabla ya kufanya muamala wowote.
Kenya:
Kuna mtu mmoja nae namfahamu, alipigiwa simu na mtu alio mfahamisha anatatizo
la laini yake kusajiliwa mara mbili. Katika mazungumzo yao katika simu
alijikuta akitoa taarifa zake binafsi na baadae kujikuta amepoteza pesa zote
alizo kua amehifadhi katika simu yake. Kiasi
ambacho ni cha takriban laki tisa za kitanzania.
USHAURI
KWENYE HILI: Kwanza kabisa, Hakikisha hutoi taarifa
zako binafsi kupitia simu. Makampuni ya simu yana jukumu la kuji hakikishia
mhusika anaye jaribu kutengeneza laini yenye namba inayo tumika ni sahihi ( kwa
Tanzania tumepiga hatua kwenye hili, tumekua na mikakati ya kuzuia watu
kutengeneza laini ambazo zimetumiaka “Swapping” na tayari nimeshauri maka mpuni
ya Kenya kua natabia hii) Hii ni njia pekee ya kukabiliana na tukio kama hili.
Kwa wastani Barani Afrika, Matukio kama niliyo
ainisha kwenye mifano miwili hapo juu yaliyo ripotiwa kwa mwezi huu pekee yanaelezwa
kupanda kwa asilimia 12.7 kulinganisha na miezi 6 iliyopita. Takwimu hizi ni
kubwa sana na ni lazima elimu sahihi ya uelewa “Awareness” itolewe kwa
watumiaji ambapo jukumu hili linatakiwa liwe la mitandao ya simu.
Kwenye hili la elimu ya uelewa, Nimeshuhudia
Vipeperusi vinavyo tolea ufafanuzi wa kuhakiki mtumiaji huduma za kifedha
kupitia simu anabaki salama na fedha zake ambavyo nilirizishwa navyo Nchini Kenya – Tanzania tunavyo vipeperushi
pia vinavyo bandikwa kwa mawakala lakini bado havina taarifa za kutosha.
Aidha, Kwa nchi zote zenye kutumia huduma za fedha
kupitia mitandao ya simu ni lazima vielewe vipeperushi vinavyo bandikwa kwa
mawakala pekee havitoshi lazima kuwe na njia nyingine nzuri ya kukuza uelewa wa
watumiaji ili kulinda fedha zao wanapo ziifadhi kupitia simu zao za mkononi.
Niendelee kutoa wito, Jukumu la ulinzi mtandao
lazima lianzie katika ngazi ya mtu binafsi. Aidha, Lazima tuwe na tabia ya
kuripoti matukio haya ya kihalifu mtandao ili yapatiwe suluhu. Ni vigumu
kukabiliana na uhalifu huu kama hakuna taarifa zinazotolewa. Pia ni lazima tuwe
na tabia ya kua na tabia ya kuzuia tatizo pasi na kungoja litokee ndio
tuhangaike kutafuta suluhu.
Mataifa
ya Afrika lazima yashirikiane kukabiliana na uhalifu mtandao,
Sheria mtandao ziwe zina wiana ili kuweza kufanya kazi maeneo yote, tuhakiki
tunakua na watu sahihi wenye uwezo sahihi wa kukabiliana na uhalifu mtandao
pamoja na kuwekeza kwenye vifaa vya uthibiti uhalifu mtandao – Elimu ya uelewa
pamoja na kuwaongezea watu wetu ujuzi mara kwa mara ya maswala haya ya usalama
mtandao.
No comments:
Post a Comment