Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo
kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara,
Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya
usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na
wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu
mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa
jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya
pekee duniani kote.
Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za
mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa
mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia
unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa
ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za
mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"
Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya
kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni
yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu
mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky
Lab.
Taarifa inaeleza kwamba genge la wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba Mamilioni ya Dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015.
Ripoti
hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua nambari za
akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba pesa.
Kaspersky
imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani
mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.
Hadi
kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa
kutoka kwenye akaunti za wateza.
Genge
hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina
ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.
Kampuni
hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na
polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani ,
Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.
Kamanda
wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa
wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa
mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.
Kaspersky
hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu
binafsi.
genge
hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za
benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye
kompyuta.
Kutokana
na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine
wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni
kumi.
Kwa
Tanzania Hali inaweza kubadilika kabisa siku za usoni kwani tayari mipango na
mikakati ya dhati ya kukabiliana na uhalifu huu wa kuibia watu pesa zao kupitia
ATM inaendelea kwa kasi na hatima ya kupata Muarobaini stahiki unategemewa
kutatua hali husika.
No comments:
Post a Comment