Nianze makala hii kwa kupongeza jitihada za dhati za serikali ya awamu ya Nne
katika uwekezaji wake kwenye sekta ya TEHAMA Nchini. Ni wazi kabisa nchi yetu
imepiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA kulinganisha nan chi nyingi Afrika.
Mifano michache ni pamoja na kuhama kutoka analogia kulekea Digitali, Mkonge wa
taifa, Kupatikana kwa Khala Mtandao la taifa, kuaandikisha upigaji kura
kimtandao na mengineyo mengi.
Aidha,
Jitihada kama vile kupatikana kwa sharia mtandao, kupatikana kwa vitengo
vinavyo shughulikia uhalifu mtandao, wakala za serikali mtandao na mengineyo
yamekua ni hatua ya kipekee iliyoweza kutoa matumaini kwa watanzania kutoka kwa serikali ya awamu hii ya Nne inayo ongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.
Jitihada
hizi njema naona bado kuna ya kufanyika zionyeshe matunda na zibaki salama kwa
muda mrefu. Nimeyasema hayo kufuatia kauli yangu niliyoitoa, Nilipo sema serikali ina
jukumu la kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama mitandao ili kuweza
kubakisha salama jiihada hizi za TEHAMA kwani isipo fanywa hivyo kuna hatari
kubwa mbele yetu kimtandao iyakayo pelekea jitihada hizi kuingia dosari kubwa.
Hatari
za kimtandao zitakazo pelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu, siasa zetu,
tamaduni na jamii yetu kwa kwa ujumla wake. Napo zungumzia uchumi nipamoja na
upotevu mkubwa wa fedha unaosababishwa na uhalifu mtandao ulio athiri taasisi
za fedha na mawasiliano nchini. Kumekua na wimbi kubwa la wizi wa fedha
kimtandao hii ni mjumuisho wa pesa kutoka mabenki pamoja na pesa zinazo potea
kutokea kwenye miamala ya simu.
Moja
ya changamoto iliyo sikika kwenye kikao nilichoshiriki kilicho husisha nchi ya ujerumani na Tanzania ni pamoja na lalamiko kutoka kwa mshiriki kuelezea kua
kupitia mtandao alipoteza pesa zake na kumekua na ugumu kuzipata pesa hizo.
Nilitolea ufafanuzi hilo kwa kueleza kua tatizo ni kubwa na kama hakuna
jitihada za dhati kudhibiti hili basi kuna hatari ya uchumi wetu kupitia
uhalifu huu mtandao kuporomoka.
Aidha,
Naomba nijikite zaidi kwenye Uchaguzi mkuu ujao Oktoba – Ni wazi kabisa kuanzi
uandikishaji hadi taratibu nyingine za kuelekea uchaguzi mkuu umehamishiwa
katika mtandao. BVR (Biometric Vote Registration) mfumo mtandao unaotumika
kuandikisha wapiga kura ambao kwa ujumla wake ni mfumo wwa kimtandao.
Kuna
hatari kubwa ya Mifumo hii kuathirika kimtandao na kusababisha kupatikana kwa
taarifa zisizo sahihi endapo wahalifu mtandao wataweza kuingilia na kufanya
marekebisho wa namna ya ufanyaji kazi wake. Hii inaambapatana na Matumizi
mabaya ya mitandao kuelekea uchaguzi ambapo inaweza kusababisha kuyumbisha
amani iliyoko Nchini. Nimelizungumza hili kwa kirefu sana kama inavyoweza
kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA"
Ikumbukwe
Wahalifu mtandao wamekua hawalali waki tafuta njia mpya za kuleta maafa mtandao
na ndio maana hata baada ya kumaliza kikao maalum cha wana usalama mitandao
tulipokutana Jijini Johannesburg, Ambapo Kwa ufupi taarifa yake inaweza
kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA" – Palitokea uhalifu mtandao ulio itikisa nchi ya
Marekani na baadae kwenye Mahojiano yangu na kituo cha BBC nikaweza kutolea
ufafanuzi walau kwa uchache ya wapi tunajikwaa kama tulivyo kubaliana mkutanoni.
Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia Video inayo onekana hapa.
WITO:
Naomba niendelee kutoa wito katika swala zima la ushirikiano kwani taifa au
kundi Fulani peke haliwezi kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao unao endelea
kukua kwa kasi. Aidha, Kuendelea kukuzwa kwa uwezo watu wentu wa ndani hasa
wanao shughulikia uhalifu mtandao nchini pamoja na kukukuza uelewa wa matumizi
salama mitandao kwa watumiaji.
Aidha,
Kupatikana kwa Chombo maalum kitakacho unganisha nguvu za vitengo kadhaa
vilivyopo ili kupatikana nguvu ya pamoja kufikia malengo ya kuweka taifa letu
salama pamoja na kuongeza uwekezaji katika usalama wetu wa mitandao Nchini.
No comments:
Post a Comment