Ijumaa 26 – 06 – 2015 nilishiriki katika mjadala ulio jadili uchumi
wa kidigitali katika kongamano lililo andaliwa na COSTECH ambapo
kwa upande wangu niliangazia uhalifu mtandao unavyoweza kuleta athari kwenye uchumi wetu ukizingatia sasa miamala mingi ya kifedha imekua ikifanywa
kwa msaada wa TEHAMA ( Simu, ATM , Mitandao).
Nilitolea
ufafanuzi hali halisi kwa sasa na tuendako huku nikitolea mfano uchumi wa taifa lolote unavyoweza kuyumbishwa au kudondoshwa kabisa wa endapo wahalifu
mtandao watahujumu TEHAMA zinazotumika kurahisisha shughuli za kibiashara zinazokuza uchumi wa taifa.
Aidha,
Nilitolea ufafanuzi mambo muhimu yakuzingatia ili kujiweka salama kimtandao – Baada
ya mjadala huo nilipokea maswali mengi yaliyolenga kutaka kufahamu zaidi
kuhusiana na uhalifu mtandao pamoja na kutaka nitolee ufafanuzi zaidi angalizo muhimu zinazoweza kuboresha hali ya usalama mitandao.
Hapa
Nitaangazia mambo kadhaa walau kwa uchache ya kuzingatia utumiapo mitandao situ wakati wa kufanya miamala ya kibiashara bali nitatolea na majibu ya maswali
ya msingi niliyopata kuulizwa.
Mazingara ya Faragha (Private
setting): Mara nyingi watumia mitandao wamekua hawana uelewa
mzuri wa kwanini pakawa na private settings kwenye mitandao mingi hasa ya
kijamii na yamasiliano pamoja na simu zetu za viganjani. Wengi wamekua wakiacha
au kutoa ruhusa kwa yeyote kuona kila afanyacho mtandaoni na alipo kwa kutoweka
sawa Private settings.
Teknolojia mpya (New technology):
Ununuapo kifaa kipya chene teknolojia ya juu jitahidi kujua unahitajika kua
makini zaidi kuhakiki unafunga wigo wa watu kuweza kukuingilia/ dukua kwani
teknolojia mpya zina rahisisha maisha yetu pamoja na kuja na changamoto zaidi.
Mfano: unapoamua kutumia TEHAMA katika vyombo vya usafiri au kuongoza vifaa vya
nyumba yako ujue unaongeza wingo wa kudukuliwa na athari ni kubwa zaidi tofauti
na anaetumia TEHAMA kuwasiliana kwa simu na meseji pekee.
Jithibitishie kumjua unaezungumza nae
kupitia Mitandao/simu: Uhalifu unaokua kwa kasi kubwa hivi sasa ni
pamoja na spoofing – Aina ya uhalifu inayo mruhusu mhalifu kutumia namba au kifaa
chako cha komputa kwa kutumia utambulisho wako. Maana Kuna tovuti na visaidizi
kadhaa mitandaoni vinavyoruhusu mtu kubadilisha namba za watu na kufanya waweze
kutumia utambulisho wa mlengwa wake pasi na muhusika kujua.
Hii inasababisha upokee simu kutoka kwa
namba unayo ifahamu wakati anae kupigia ni mhalifu au kupokea barua pepe kutoka
kwa unaemfahamu wakati mwandishi ni mhalifu. Hivyo hakikisha hutoi taarifa muhimu
mpaka ujiridhishe unaye wasiliana nae ni muhusika sahihi.
Matumizi ya Neno la siri:
Nimekua nikizungumzia sana hili la matumizi sahihi ya neno la siri madhubuti (strong
password) – Leo nasisitiza tu kua utumiapo neno la siri madhubuti unaweza
kujilinda kwa kiasi kikubwa na uhalifu mtandao. Naposema neno la siri madhubuti
lina jumuisha Herufi kubwa na ndogo, namba, n.k (Mfano: A6g#HT7c) pia hakikisha
neno la siri ni refu. Muhimu: kwa vile vijavyo na maneno ya siri (Default
passwords – Mfano Switch/ Router n.k) hakikisha unabadilisha. Mfano rahisi matukio
kadhaa ya kihalifu mtandao yameripotiwa kutekelezeka kirahisi kutokana na
udhaifu wa maneno ya siri.
Kua makini sana na wale watumiao
jina/picha zako mitandaoni: kumekua na mtindo wa watu kutumia
majina ya wenzao mitandaoni ambapo baadae yameonekana kuleta athari kubwa sana.
Mjadala tunaoendelea nao toka Jumamosi (27 – 06 – 2015) unahusiana na athari za
wanaotambulika kama (evil twin) wanaotumia majina ya wenzao kusababisha
sintofahamu mitandaoni. Kitu ambacho kimekua na mchango mkubwa sana kwenye
uhalifu unaotambulika kama (Cyber bullying) ambapo hadi sasa kuna ripoti kadhaa
za walio ondoa uhai wao baada ya kuathirika na uhalifu huu. Ni moja ya vitu vinavyo
tengemewa kupatiwa mwarubaini lakini ikiwa bado hatujafika hapo ni vizuri ngazi
ya mtu binafsi kujenga tabia ya kua na umakini kwa wale wanaotumia majina yako
mitandaoni. Hadi sasa tayari kuna Virahisishi vinavyoweza kutambua nani anatumia
jina au picha zako mitandaoni.
Kuna
mengi ya ku elezea na nitajitahidi kufanya hivyo wakati mwingine na kwa haraka
haraka – Nilipata kuulizwa kuhusiana na Wizi mtandao kupitia ATM ambapo naweza sema
bado ni tatizo la mataifa mengi nabado linakua ni tatizo linalo athiri sana
uchumi na suluhu kadhaa zimeendelea kupatikana. Huku Tanzania ikiwa na muelekeo
wa kufika pazuri pia kama utayari utapatikana.
Aidha,
Nilipata kuulizwa juu ya miamala inayofanywa katika mitandao ya intaneti. Ushauri:
miamala hii inapofanywa kupitia mitandao iliyo ongezewa ulinzi aina ya hhtps – Ambapo
wawasiliano yanakua fiche (encrypted) inaaminika kua salama ingawa wahalifu walifanikiwa kusababisha
uhalifu aina ya heartbleed ambao uliathiri aina hii ya ulinzi mtandao. Utatuzi
umepatikana ingawa bado changamoto kadhaa bado zipo.
Mwisho
kwa sasa napenda kuendelea kutoa msisitizo kua swala la usalama mitandao lazima
lianze katika ngazi ya mtu binafsi pasi na kusubiri aina flani ya watu
kuimarisha ulinzi wako wa mitandao. Aidha, Ku ripoti matukio ya kihalifu mtandao ni
muhimu sana ili papatikane suluhu ya haraka kuepusha adhara zaidi.
Kaka mimi nakukubali sana.
ReplyDeleteNatamani sana kua kama wewe, naomba unishauri kaka yangu
Nimekuandikia kupitia contact kileo natumaini utanijibu.
ahsante.
Nashkuru - Nimeiona na nimesha kujibu.
DeleteNakutakia kila la kheri.