WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 29 June 2015

KUA MAKINI NA FARAGHA (PRIVATE SETTINGS) MTANDAONI

Ijumaa 26 – 06 – 2015 nilishiriki katika mjadala ulio jadili uchumi wa kidigitali katika kongamano lililo andaliwa na COSTECH ambapo kwa upande wangu niliangazia uhalifu mtandao unavyoweza kuleta athari kwenye uchumi wetu ukizingatia sasa miamala mingi ya kifedha imekua ikifanywa kwa msaada wa TEHAMA ( Simu, ATM , Mitandao).

Nilitolea ufafanuzi hali halisi kwa sasa na tuendako huku nikitolea mfano uchumi wa taifa lolote unavyoweza kuyumbishwa au kudondoshwa kabisa wa endapo wahalifu mtandao watahujumu TEHAMA zinazotumika kurahisisha shughuli za kibiashara zinazokuza uchumi wa taifa.

Aidha, Nilitolea ufafanuzi mambo muhimu yakuzingatia ili kujiweka salama kimtandao – Baada ya mjadala huo nilipokea maswali mengi yaliyolenga kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na uhalifu mtandao pamoja na kutaka nitolee ufafanuzi zaidi angalizo muhimu zinazoweza kuboresha hali ya usalama mitandao.

Hapa Nitaangazia mambo kadhaa walau kwa uchache ya kuzingatia utumiapo mitandao situ wakati wa kufanya miamala ya kibiashara bali nitatolea na majibu ya maswali ya msingi niliyopata kuulizwa.

Mazingara ya Faragha (Private setting): Mara nyingi watumia mitandao wamekua hawana uelewa mzuri wa kwanini pakawa na private settings kwenye mitandao mingi hasa ya kijamii na yamasiliano pamoja na simu zetu za viganjani. Wengi wamekua wakiacha au kutoa ruhusa kwa yeyote kuona kila afanyacho mtandaoni na alipo kwa kutoweka sawa Private settings.

Teknolojia mpya (New technology): Ununuapo kifaa kipya chene teknolojia ya juu jitahidi kujua unahitajika kua makini zaidi kuhakiki unafunga wigo wa watu kuweza kukuingilia/ dukua kwani teknolojia mpya zina rahisisha maisha yetu pamoja na kuja na changamoto zaidi. Mfano: unapoamua kutumia TEHAMA katika vyombo vya usafiri au kuongoza vifaa vya nyumba yako ujue unaongeza wingo wa kudukuliwa na athari ni kubwa zaidi tofauti na anaetumia TEHAMA kuwasiliana kwa simu na meseji pekee.

Jithibitishie kumjua unaezungumza nae kupitia Mitandao/simu: Uhalifu unaokua kwa kasi kubwa hivi sasa ni pamoja na spoofing – Aina ya uhalifu inayo mruhusu mhalifu kutumia namba au kifaa chako cha komputa kwa kutumia utambulisho wako. Maana Kuna tovuti na visaidizi kadhaa mitandaoni vinavyoruhusu mtu kubadilisha namba za watu na kufanya waweze kutumia utambulisho wa mlengwa wake pasi na muhusika kujua.


Hii inasababisha upokee simu kutoka kwa namba unayo ifahamu wakati anae kupigia ni mhalifu au kupokea barua pepe kutoka kwa unaemfahamu wakati mwandishi ni mhalifu. Hivyo hakikisha hutoi taarifa muhimu mpaka ujiridhishe unaye wasiliana nae ni muhusika sahihi.

Matumizi ya Neno la siri: Nimekua nikizungumzia sana hili la matumizi sahihi ya neno la siri madhubuti (strong password) – Leo nasisitiza tu kua utumiapo neno la siri madhubuti unaweza kujilinda kwa kiasi kikubwa na uhalifu mtandao. Naposema neno la siri madhubuti lina jumuisha Herufi kubwa na ndogo, namba, n.k (Mfano: A6g#HT7c) pia hakikisha neno la siri ni refu. Muhimu: kwa vile vijavyo na maneno ya siri (Default passwords – Mfano Switch/ Router n.k) hakikisha unabadilisha. Mfano rahisi matukio kadhaa ya kihalifu mtandao yameripotiwa kutekelezeka kirahisi kutokana na udhaifu wa maneno ya siri.

Kua makini sana na wale watumiao jina/picha zako mitandaoni: kumekua na mtindo wa watu kutumia majina ya wenzao mitandaoni ambapo baadae yameonekana kuleta athari kubwa sana. Mjadala tunaoendelea nao toka Jumamosi (27 – 06 – 2015) unahusiana na athari za wanaotambulika kama (evil twin) wanaotumia majina ya wenzao kusababisha sintofahamu mitandaoni. Kitu ambacho kimekua na mchango mkubwa sana kwenye uhalifu unaotambulika kama (Cyber bullying) ambapo hadi sasa kuna ripoti kadhaa za walio ondoa uhai wao baada ya kuathirika na uhalifu huu. Ni moja ya vitu vinavyo tengemewa kupatiwa mwarubaini lakini ikiwa bado hatujafika hapo ni vizuri ngazi ya mtu binafsi kujenga tabia ya kua na umakini kwa wale wanaotumia majina yako mitandaoni. Hadi sasa tayari kuna Virahisishi vinavyoweza kutambua nani anatumia jina au picha zako mitandaoni.

Kuna mengi ya ku elezea na nitajitahidi kufanya hivyo wakati mwingine na kwa haraka haraka – Nilipata kuulizwa kuhusiana na Wizi mtandao kupitia ATM ambapo naweza sema bado ni tatizo la mataifa mengi nabado linakua ni tatizo linalo athiri sana uchumi na suluhu kadhaa zimeendelea kupatikana. Huku Tanzania ikiwa na muelekeo wa kufika pazuri pia kama utayari utapatikana.

Aidha, Nilipata kuulizwa juu ya miamala inayofanywa katika mitandao ya intaneti. Ushauri: miamala hii inapofanywa kupitia mitandao iliyo ongezewa ulinzi aina ya hhtps – Ambapo wawasiliano yanakua fiche (encrypted) inaaminika kua salama ingawa wahalifu walifanikiwa kusababisha uhalifu aina ya heartbleed ambao uliathiri aina hii ya ulinzi mtandao. Utatuzi umepatikana ingawa bado changamoto kadhaa bado zipo.


Mwisho kwa sasa napenda kuendelea kutoa msisitizo kua swala la usalama mitandao lazima lianze katika ngazi ya mtu binafsi pasi na kusubiri aina flani ya watu kuimarisha ulinzi wako wa mitandao. Aidha, Ku ripoti matukio ya kihalifu mtandao ni muhimu sana ili papatikane suluhu ya haraka kuepusha adhara zaidi.

2 comments:

  1. Kaka mimi nakukubali sana.
    Natamani sana kua kama wewe, naomba unishauri kaka yangu
    Nimekuandikia kupitia contact kileo natumaini utanijibu.
    ahsante.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashkuru - Nimeiona na nimesha kujibu.
      Nakutakia kila la kheri.

      Delete