Zikiwa
zimebaki siku chache kuanza kutumika kwa sheria mtandao Nchini Tanzania, Mengi
yame endelea kuzungumzwa ikiwa ni pamoja na kurudia mapungufu yaliyopatikana
katika sheria ya awali iliyo wasilishwa bungeni na kusambazwa kwa maneno kua sharia
hii mtandao ipo kuziba watanzania midomo huku wengine wakizungumzia itakiuka
faragha za watanzania. Sheria hii inakuja kusaidia mambo mengi nani wazi mengi
hayo yamekua hayazungumzwi kabisa.
Hivi
karibuni kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa maswala ya usalama mitandao ambapo
moja ya mijadala iliangazia sharia hii na kutolea ufafanuzi yale yaliyokua
hayajaeleweka vizuri. Binafsi Nilikua mmoja wa washiriki ambapo kwa ujumla wetu
tulianisha mambo kadhaa na kuzidi kutoa hofu kwa yale ambay yameendelea
kupotoshwa kuelekea matumizi ya sharia hii mtandao. Makala hii itajikita kwenye
hayo yasiyo zungumzwa kwa wingi hivi sasa.
Upotevu wa fedha,
hivi karibuni akizungumza na Jeshi la polisi waziri wa Mawasiliano,Sayansi na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alitahadharisha kua shilingi trilioni 54.4
zitakuwepo kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa mitandao, endapo
Sheria za Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika.
Alianisha
kua fedha hizo ni sawa na trioni 4.4 kila mwezi. Profesa Mbarawa amesema fedha
hizo lazima zilindwe kwa kuwekewa sheria
zenye kuzuia na kutoa adhabu kwa watu watakaoingilia mihamala ya fedha. Kuzilinda
fedha hizo Sheria mtandao haina budi kuwepo ili kuwapa uwezo wahusika kufanya
kazi yao ipasavyo.
Udukuzi,
Wimbi la udukuzi wa tovuti na mitandao yakijamii na barua pepe za watu binafsi
bado ni changamoto nchini – Malalamiko yameendelea kua mengi na hakuna namna
nyingine ya kuhimili tatizo pasipokua na sharia mtandao ili kutoa fursa kwa
wahalifu hao kuchukuliwa adhabu stahiki.