WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday, 20 August 2015

SHERIA MTANDAO: YASIYOTAJWA ITAKAPO ANZA KUTUMIKA SEPTEMBA MOSI

Zikiwa zimebaki siku chache kuanza kutumika kwa sheria mtandao Nchini Tanzania, Mengi yame endelea kuzungumzwa ikiwa ni pamoja na kurudia mapungufu yaliyopatikana katika sheria ya awali iliyo wasilishwa bungeni na kusambazwa kwa maneno kua sharia hii mtandao ipo kuziba watanzania midomo huku wengine wakizungumzia itakiuka faragha za watanzania. Sheria hii inakuja kusaidia mambo mengi nani wazi mengi hayo yamekua hayazungumzwi kabisa.


Hivi karibuni kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa maswala ya usalama mitandao ambapo moja ya mijadala iliangazia sharia hii na kutolea ufafanuzi yale yaliyokua hayajaeleweka vizuri. Binafsi Nilikua mmoja wa washiriki ambapo kwa ujumla wetu tulianisha mambo kadhaa na kuzidi kutoa hofu kwa yale ambay yameendelea kupotoshwa kuelekea matumizi ya sharia hii mtandao. Makala hii itajikita kwenye hayo yasiyo zungumzwa kwa wingi hivi sasa.

Upotevu wa fedha, hivi karibuni akizungumza na Jeshi la polisi waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alitahadharisha kua shilingi trilioni 54.4 zitakuwepo kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa mitandao, endapo Sheria za Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika.

Alianisha kua fedha hizo ni sawa na trioni 4.4 kila mwezi. Profesa Mbarawa amesema fedha hizo lazima zilindwe  kwa kuwekewa sheria zenye kuzuia na kutoa adhabu kwa watu watakaoingilia mihamala ya fedha. Kuzilinda fedha hizo Sheria mtandao haina budi kuwepo ili kuwapa uwezo wahusika kufanya kazi yao ipasavyo.

Udukuzi, Wimbi la udukuzi wa tovuti na mitandao yakijamii na barua pepe za watu binafsi bado ni changamoto nchini – Malalamiko yameendelea kua mengi na hakuna namna nyingine ya kuhimili tatizo pasipokua na sharia mtandao ili kutoa fursa kwa wahalifu hao kuchukuliwa adhabu stahiki.


Cyberbullying, Kudhalilisha watu mitandaoni ambapo kila siku kunakuja aina mpya ya udhalilishaji na unyanyasaji mtandao ambapo malalamiko yamekua mengi. Kumekua na watu kazi yao ni kutukana wengine kudhalilisha wengine na kuwafanya wengine wawe waoga kuwa mitandaoni – Binafsi, Si mtumiaji wa Instagram: Ila nimekua nikisikia malalamiko mengi sana kwa watumiaji wake na wengine wakidai wamekua wakilazimika kufunga akaunt zao kutokana kudhalilishwa na hata wasio wajua.

Catfishing, Kumekua na wimbi la watu wakitumia picha za wngine na kutengeneza akaunt fekiAkaunti ambazo baadae zinatumiwa vibaya na wahalifu hao ikiwa ni pamoja na kuandika yanayoweza kumuaribia sifa ambayo mhusika halisi anayo zenye madhumuni ya kuwapotosha wengine na kutengeneza chuki na uhasama.

Wizi wa simu, Kumeendelea kua na wimbi la watu kuiba simu za wengine ambapo baadae zinaweza kutumika vibaya ili kumsababishia mmiliki halisi kuingizwa matatani – Sheria hii situ itadhihirisha na kudhibiti hali ya wizi wa simu hizi bali na kuhakiki wahusika wanapotumia vibaya wanagundulika kirahisi. Hii ilipaswa kua ni fursa kwa wanaopotelewa na simu wakati huu kuendelea kutoa taarifa zaidi ili sharia ifate mkondo wake na si kulalamikia sharia hizi.

Vikoba, Kumekua na wizi wa kitapeli unaotumia jina la vikoba ambapo kupitia mitandao watu wana rubuniwa na kujikuta wakilipa pesa ambapo baadae wanajikuta zimeingia mikononi mwa wahalifu mtandao. Malalamiko ya aina hii nimeyapata sana nan i wazi yanahitaji sharia mtandao kuweza kukabiliana na wahalifu hawa.

Clickjacking, Ni dhahir kua kumekua na aina ya uhalifu amabao umeendelea kukua kwa kasi ambapo picha zisizo rafiki zinasambazwa kwenye akaunti za wengine zinazo hamasisha wengine kubonyeza zikiwa na mfano wa Video – Kitu ambacho kimekua kiki ibua hisia mbali mbali kwa waathirika na kupelekea wengine kutaka kufunga akaunti zao kutokana na hali hii. Uhalifu huu unahitaji kudhibitiwa na msumeno wa hili lazima pawe za sharia itakayo ipa mamlaka husika kufanya kazi yake ipasavyo.

Faragha, Hofu hii napenda kuendelea kuiweka sawa kwa kueleza kua – Ikiwa kina kitu kimoja maadili ya wanausalama mitandao yanasisitiza ni faragha ya mtu na ndio maana kuna siku maalum inayojulikana kama DPD (Data Privacy Day – Siku ya Faragha ya taarifa) ambapo nikatika kukumbusha kua faragha ni moja ya vitu muhimu kuangaziwa macho.


Kuelekea uchaguzi, Uchaguzi uko njiani – Inawezekana kwa haraka tusione athari za matumizi mabaya ya mitandao leo kutokana nan chi yetu haijashuhudia machafuko makubwa kama yaliyotokea katika nchi nyingine barani Afrika (Kenya, Misri, Libya, Tunisia n.k.

Maelezo sahihi ni kua mitandao ya kijamii yalitumika kama silaha kubwa kuchochea machafuko katika nchi hizo na hili lilisababisha Nchi kama (Iran na Uturuki) kua makini sana na kuhakiki wamedhibiti na kufungia mitandao ya kijamii ikiwa ni hatua za kudhibiti machafuko yaliyokua yameznza kuonyesha ishara.

Kusambaza taarifa zisizo sahihi zenye chuki na uchochezi mtandaoni zinaweza kua chachu ya watu kufarikiana na kugombana na hatimae kukua na kusababisha hali kua mbaya – Tumeshuhudia mara kadhaa watanzania kupitia mitandao ya kijamii kurushiana matusi kupitia mitandao na hata wakati mwingine kutishiana ikiwa ni katika kujibu kilicho andikwa na mtoaji mada huku mtoaji mada akiwa kimya ilhali wachangiaji wako katika mabishano makali.

Yamejri mara kadhaa ugumvi wa mtandaoni kuamishiwa katika hali ya kawaida inayo pelekea watu kupigana na kuumizana kutokana na yaliyoanzia mtandaoni wakati watu hao wakichangia mada iliyopelekea kutukananana na kutishiana na baadae kua kweli.

Natoa wito kwa watanzania kutambua serikali ya nchi yoyote haiwezi kudhamiria kuhamishia raia wake gerezani na ndio maana msisitizo mkubwa ni kuhakiki kunapatikana elimu stahiki na sahihi kwa watanzania kujua kuhusiana na uhalifu huu mtandao na namna ya kujilinda nao. Sambamba na hili kuhaki pana patikana elimu ya ujuzi stahiki wa kimaadili na utaalam sahihi wa uchunguzi wa makosa haya unapatiwa wale wote wanao husika ili kuhakiki wasio na hatia hawaingii matatani.


No comments:

Post a Comment