Nimekamilisha
vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia mualiko
maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili (ya kwanza ikiwa
ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya pili ikiwa ni namna ya
uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada hizo mbili ambazo
zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna mengi nikajifunza kutoka kwa washiriki. Aidha,
nilishiriki mijadala duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za
uhalifu mitandao na kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.
Kenya
ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo zimeorodheshwa kua na uhalifu
mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya kusini.
Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na kuangazia bara la
Afrika na baadae Afrika mashariki na hatimae kujikita na twakwimu za Nchi ya
Kenya.
Kwa
upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizo wasilishwa katika mkutano, hadi
kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha,
matumizi ya intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”.
Takwimu hizo zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil)
kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.
Palizungumzwa
matukio ya kudukuliwa kwa tovuti Nchini humo ambapo, tovuti za serikali 103
ziliathiriwa mwaka 2013, na 3 kwa mwaka wa 2014 huku twitter ya serikali mwaka
jana (2014) ikiwa ni miongoni mwa zilizo dukuliwa na kutumiwa vibaya. Nilihoji
tofauti kubwa ya udukuzi wa tovuti na kujulishwa baada ya tukio la aina yake la
mwaka 2013 serikali iliamua kuzifunga tuvuti zake nyingi hasa zile zilizo
onekana hazina umuhimu sana kua hewani kitu ambacho kilichangia kupunguza namba
kubwa ya udukuzi kwa mwaka 2014.
Kwa
upande wa pesa zinazopotea kwa nyia ya simu – Miamala inayo fanywa kwa njia ya
simu ni asilimia kumi (10%) ya fedha za miamala yote kila mwezi huku idadi hiyo
kuonekana kushtusha wengi.
Ikumbukwe
nchi ya Kenya, matumizi mabaya ya mitandao ilipelekea kuchochea na kusababisha
vurugu ilisababisha matatizo makubwa sana kipindi cha uchaguzi kilichopita
ambapo kwa mujibu wa mchambuzi mmoja wa maswala ya uchanguzi alichapisha andiko
na kueleza mitandao ilikua chanzo kikubwa cha kueneza chuki na fujo kipindi cha
uchaguzi uliopita.
Yote
hayo – Takwimu zote hizi kwa nchi ya Kenya zimesababishwa na jambo moja zuri
sana ambapo ni kua na uwazi wa takwimu na taarifa za kihalifu mtandao ambapo
kwa Afrika imekua ni nchi pekee iliyofanikisha swala hili. Itakumbukwa nilitoa
pongezi kwa nchi hiyo baada ya ku ainisha takwimu zake kwa mara ya kwanza mwaka
jana (2014) na kufanya iwe ya kwanza Afrika katika hili.
Kilicho
nifurahisha zaidi ni hatua taifa hilo limechukua kukabiliana na uhalifu
mtandao. Tayari nchi hiyo ina “National cybersecurity master plan” na sheria
mtandao ambapo kosa la udukuzi adhabu ni miaka kumi (10) jela, faini ya KSH
10,000 au vyote kwa pamoja. Pia ina strategy ya maswala ya usalama mitandao na
kupitia mamlaka ya TEHAMA “ICT Commission” wamesha zindua andiko linalotoa
muongozo wa kuwalinda watoto katika mitandao.
Hayo
ni uchache katika mengi ambayo tayari taifa limeweka katika mikakati yake.
Zaidi ni mikakati ya kukuza uelewa na ujuzi kwa watu wake ili kuweza kuendelea
kutumia vizuri mitandao pamoja na namna ya kukabiliana na uhalifu
mtandao.Aidha, Mpango wa serikali kuimarisha ushirikiano ambapo CERT – KENYA
inajumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama huku mashirika binafsi yakiwa na
nafasi kubwa kuisaidia ili kukabiliana na uhalifu mtandao. Mfano wa Hili ni
mshiriki kutoka Microsoft alipo tolea ufafanuzi kampuni hiyo inavyo fanya kazi
karibu na serikali ya kenya kukabiliana na uhalifu mtandao nchini humo kupitia
CERT –KENYA.
Kilicho
nipa faraja kubwa ni kauli ya pamoja kua Kenya imefanya mengi lakini
pakakubalika kua kuna mengi bado yakufanyia kazi ili kuweza kupiga hatua zaidi
katika maswala ya usalama mitandao nchini humo. Ni marachache sana mataifa
yanakiri kua bado safari ni ndefu ili kufikia malengo. Pamoja na hatua kubwa
nilizo ziona katika nchi hiyo lakini bado walikiri kuna safari ya kupiga ili
kusonga mbele zaidi.
Tulipata
kuangazia aina za uhalifu na namna zinavyofanyika kwa nchi ya kenya – hakika
aina hizi hapa kwetu pia ziko njiani na hofu yangu kubwa ni kwa kiasi gani
tutakua tumejiandaa? Kujua tatizo nihatua za awali za utatuzi na wengine
wakinyolewa ni vizuri tukatia nywele maji.
Kwa ufupi mambo yakufanyiwa kazi
ambayo bado ni changamoto kwa mataifa yote yaliyoweza kujadiliwa ni pamoja na:-
Bado
kumekua na dhana kua swala la usalama mitandao ni la kundi fulani ( wana TEHAMA
– waliojikita katika maswla ya usalama mitandao) Hili sasa linatakiwa libadilike
na katika kila kampuni au serikali lazima swala hili lianzie katika ngazi ya
juu kushuka hadi ngazi ya mmoja mmoja (Kila mtu)
Bado
udukuzi na uhalifu mtandao kwa ujumla umeendelea kushika kasi huku ugunduzi wa
tukio kutokea kuchukua hadi siku 200 kwa wastani baada ya tukio ambapo
tumekubaliana kimsingi hii ni namba kubwa sana na kunakila sababu ya kushusha namba
hizi – pia kuwe na njia za kuzuia tatizo kabla halijatokea ambazo ni madhubuti
kwa kufanyia kazi ushauri unaotolewa wataalam.
Uhalifu
wa ndani (Insider threats) bado ni changamoto kubwa sana katika anga ya dunia
na imeonekana kusahauliwa kabisa huku jitihada za dhati zikianza kuonekana
kukuza uelewa kwenye hili na sasa tayari “Mr. Robot” tamthilia mpya ya kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao imejikita kwenye hili.
Uhaba
wa wataalam katika maswala ya usalama mitandao ni la kuchukuliwa hatua za
haraka kwa kuhimiza mitaala ya usalama mitandao kuingizwa vyuoni huku wataalam
wanaopatikana kutumika vizuri – Wenye ujuzi watumike mahali husika kwani
imeonekana bado kuna changaoto ya kutotumiwa vizuri wataalm wa maswala haya
inaypelekea uhalikfu kukua kwa kasi kila kukicha. Hili limeonekana zaidi barani
Afrika na mataifa kadhaa wamesha anza kulifanyia kazi ili kuweka mabo sawa.
Sheria
mitandao kutumiwa ipasavyo lakini pia iambatane na kua na waelewa wa uchunguzi
wa makosa haya kwa kuzingatia maadili na taratibu za kitaalm zilizo sahihi na
kuhakiki uelewa unasambazwa kwa watu ili kuepusha wimbi kubwa la wahalifu
mtandao wanao fanya uhalifu huu bila kujua kuingia matatani – Imeonekana bado
kuna ugumu mkubwa wa kesi za uhalifu mtandao kuvuka mahakamani na watuhumiwa
kuwajibishwa kutokana na udhaifu mkubwa kwa mataifa ya Afrika mashariki
walionao katika kufata taratibu za kuwasilisha kesi hizi ipasavyo mahakamani
(Ujuzi bado Uko chini sana).
Ushirikiano
wa ndani ya mataifa pamoja na kuvuka mipaka bado ni changamoto inayo onekana
kuzikumba Nchi nyingi hasa barani Afrika huku Kenya ikiwa imeliona hili na
imepiga hatua nzuri kwa ndani ila bado wanakiri kuvuka mipaka bado ni
changamoto kutokana na utayari wa mataifa mengine katika hili.
Hayo
ni kwauchache tu kwani mengi sana yamejadiliwa na nategemea kutumia muda wangu
kadhaa kuwasilisha kidogo kidogo ili tuweze kuendelea kujifunza zaidi kupitia
vyanzo mbali mbali vya habari.
Ndugu Kileo,
ReplyDeleteHongera kwa kutuwakilisha, na shukrani kwa taarifa. Huwa napenda kujifunza mambo mapya, na kwa msingi huo umenipa changamoto. Nakutakia kila la heri.
Nashkuru sana Mbele - nawe Kila la Kheri.
Delete