WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 4 December 2015

WAHALIFU MTANDAO WATIKISA ANGA YA WANAUSALAMA MITANDAO

Wanausalama mtandao kote duniani walikamilisha tukio muhimu sana linalofanyika kila mwezi Oktoba (Cybersecurity Awareness Month) lenye dhamira ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao huku ikiaminika kupitia tukio hilo uhalifu mtandao unaweza kupunguzwa kwa asilimia kubwa. Mataifa mengi yakiwa na mafanikio makubwa kutokana na hili ambapo Tanzania pia kupitia baadhi ya Makampuni  ilipata kushiriki.

Wakati bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliofanyika kwa ubunifu na umahiri wa hali ya juu ambapo wahalifu mtandao wamefanikiwa kusambaza kirusi aina ya ModPOS kinacho athiri mashine zinazotumika kukamilisha miamala wakati wa manunuzi.

Kirusi cha ModPOS, kimegundulika Nchini Marekani wakati wa sherehe za “Thanks Giving” ambapo watu wengi hufanya manunuzi. Kirusi hicho Kimekua kikifanikisha upotevu mkubwa wa pesa wakati wa miamala.

Mara baada ya ugunduzi huo wa ModPOS, mijadala kupitia mtandao ilianza baina ya wanausalama mitandao ili kuweza kufanikisha mambo makubwa matatu. Moja ni kuweza kugundua chanzo na jinsi ilivyo fanikishwa kuwepo bila kugundulika (Inaaminika kimedumu muda – Taarifa ambazo bado zinafatiliwa) Pili, Ilikua ni kutafuta suluhu ya kirusi hicho ili kiweze kuondolewa na Tatu, ni kupanga namna ya kukuza uelewa wa namna ya kujikinga na janga hili la ModPOS.


Hadi sasa bado hapaja patikana suluhu na inahofiwa huwenda kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka kirusi hicho kusambaa maeneo mengine huku mataifa yakitakiwa kuchukua tahadhari. Inakadiriwa kama kitaendelea kutopatiwa suluhu; pesa nyingi zitaishia mikononi mwa wahalifu mtandao na hasara itakayopatikana ni kubwa zaidi kupata kutokea.

Wakati hayo yakiendelea kuwa ni mjadala wa vuta nikuvute. Wahalifu wakadukua Kampuni ya VTech inayotengeneza midoli ya watoto ya kielektroniki kutumia TEHAMA ambapo walifanikiwa kuiba taarifa zaidi ya milioni tano ikiwa ni pamoja na Picha za watoto, Mawasilianao ya watoto na wazazi wao, Sauti za watoto, na taarifa za miamala wakati wa manunuzi.

Inaaminika kutokana na umakini mkubwa wanausalama mtandao wamekua wakiweka juu ya kuwalinda watoto wawapo mtandaoni kitu ambacho kimepelekea kua na program ya kidunia maarufu kama “Child Online Protection – COP” yenye dhamira ya kuhakiki watoto wanabaki salama watumiapo TEHAMA/ Mitandao, Wahalifu walitumia udukuzi wa VTech ili kuhamisha mawazo ya kukabiliana na ModPOS na badala yake nguvu kubwa ihamie kwenye udukuzi VTech.

Kufuatia udukuzi huo kwenye kampuni ya VTech wanausalama mtandao walishauri Kampuni hiyo kusitisha huduma zake za mtandao mara moja na kuendelea kutafuta suluhu ya tatizo. Huku kampuni hiyo ikitakiwa kuhakiki taarifa zilizo dukuliwa hazipatikani/ kusambwazwa mitandaoni. Kampuni ya VTech tayari imechukua uamuzi wa kusitisha huduma zake mtandao.

Hayo yakijiri, Nchini Kenya nako wameshatoa Ripoti/taarifa za mwaka kuhusiana na uhalifu mtandao ambapo uhalifu mtandao umeonekana kukua zaidi. Taarifa ilifafanua uhaifu mtando umebadili taswira na kuwa sit u wa kudukua maneno ya siri bali ni taarifa zinazoweza kupelekea mabilioni ya dola kuishia kwa wahalifu mtandao. Jitihada za dhati zimeendelea nchini Kenya ili kukabiliana na uhalifu huu mtandao.

Tanzania nayo haijabaki salama, Baada ya uhalifu mtandao maarufu kwajina la “vikoba” ulioshika kasi kipindi kifupi cha nyuma uliosababisha waathirika kuibiwa fedha zao na wahalifu mtandao. Baadae elimu juu ya uhalifu huo ilisambaa na hatimae kupungua sasa wahalifu mtandao wamekuja na aina mpya ya uhalifu mtandao wenye dhamira ya kuiba taarifa za watu baada ya kufanikiwa kutengeneza program yenye kuwashawishi watu kuingiza taarifa za wengine kwa madhumuni ya kudukua taarifa za watu binafsi.Ikumbukwe hili ni kosa na lazima wananchi wawe makini kwenye hili.

Aidha, wahalifu matandao wajakomea hapo, Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni ya kiusalama mtandao ya “Symantec” imefankiwa kugundua mbinu ambayo wahalifu mtandao wamekua wakitumia mtandao wa kijamii wa “LinkedIn” ambapo wahalifu wamekua waki dhamiria zaidi kuiba taarifa zinazopatikana kwenye mtandao huo baada ya kuweka ukaribu na watumiaji mtandao huo kwa kuwaomba urafiki na baadae kutumia taarifa zilizopo huko kufanya udukuzi.

Hili tayari Symantec kwa kushirikiana na LinkedIn imeanza opareheni funga akounti zozote zinazobainika kuwa ni za wahalifu mtandao na tunategemea kupata taarifa yake kamili hapo baadae.

Matukio hayo na mengine yanayowea kujitokeza watai tunaelekea mwisho wa mwaka ushauri mkubwa umeendelea kutolewa ku kuhakiki panakua na mpango endelevu wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao (Cybersecurity awareness).

Pamoja na hilo mataifa yana aswa kua na tabia ya kuhakiki yanatambua kwa ukaribu sana viashiria vyovyote vya kihalifu mtandao ili kuweza kuweka mataifa yao salama kimtandao. Zaidi ni pamoja na kukuza nguvu kazi watu kwenye sekta ya usalama mtandao pamoja  na kua na matumizi ya watu sahihi katika kukabiliana na uhalifu mtandao.


Natoa wito wa kutambua uhalifu mtandao upo na una madhara makubwa katika sekta zote kuanzia Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, nakadhaika endapo hatua kuanzia ngazi ya mtu binafsi hazitachukuliwa ili kuhakiki pana patikana usalama katika mitandao. Tujenge tabia yay a kutafakari kabla ya kutumia mitandao ili kuhakiki hatusababishi madhara kwa kuanzia kwa mtu binafsi pamoja na kwa wengine.

2 comments:

  1. Your blog has always been a good source for me to get quality tips on blogging. Thanks once again.
    cyber security conference

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thanks Faryal,
      I truly appreciate your feedback.

      Many thanks.
      -Kileo.

      Delete