Teknolojia
imeendelea kurahisisha maisha na kwa sasa kumekua na ukuaji wa matumizi ya simu
za viganjani kufanya miamala ya fedha maeneo mengi ya bara la Afrika. Kufuatia
ongezeko kubwa la watumiaji wa simu, mabenki na kampuni za simu zimeendelea
kuhakiki simu zinatumika kufanya miamala ya kifedha.
Kwa
mujibu wa ripoti ya mwaka jana (2015) ya GSMA State of the industry, huduma
za kifedha kupitia simu kwa sasa zinapatikana katika nchi 93 duniani ikiwa na
jumla ya huduma 271 kwa ujumla wake, kwa wastani watoa huduma za kifedha
kupitia simu wana safirisha kiasi cha dola
milioni 33 kwa siku. Takwimu hizi zinategemewa
kuendelea kukua.
Aidha,
Mwaka jana (2015), European investment bank ilianisha Afrika kuongoza duniani kwa
matumizi ya Simu za viganjani kufanya miamala yakifedha. Kwa Upande wa Nchi ya Kenya,
asilimia 62 (62%) ya watu wake
wamekua wakitumia simu za viganjani kufanya miamala ya kifedha.
-------------------------------------
NEWS UPDATE: Some of the contributing factors in the US $80 million theft from the
Bangladesh central bank included the use of inexpensive, second-hand routers
and the lack of a firewall. In addition, an investigation conducted by BAE
Systems suggests the attackers tricked the SWIFT financial software with custom
malware.
--------------------------------------
Imefika
wakati, Tunaweza kulipia huduma mbali mbali, kuhamisha fedha, kununua bidhaa,
na mambo mengine kadhaa kupitia simu zetu za viganjani. Urahisi huu katika
maisha pia umeambatana na ukuaji wa wahalifu mtandao wanaoendelea kwa kasi kuja
na njia tofauti tofauti kufanikisha wizi wa fedha zinazo patikana au kuhamishwa
kupitia simu zetu za mikononi.
Kwa
mujibu wa ripoti ya 2014 ya ACFE, The Nationals on occupational Fraud
and abuse inaeleza kupitia kesi
1,483, dola bilioni 3 zimepotea kutokana na wizi mtandao. Aidha, Kila mwaka
Nchi ya Kenya pekee inapoteza kiasi cha Shilingi bilioni 5 za kenya (sawa na Dola milioni 50) huku ikitabiriwa kiasi
hicho kinaendelea kuongezeka.
Mabenki
yameendelea kutumia teknolojia ya neon la siri la mara moja (One
time Password – OTP) kama njia kulinda fedha za wateja wake ambapo
teknolojia hii tayari imekuwepo kwa muda mrefu sasa – Imepitwa na wakati.
Itakumbukwa mwaka 2012, Australia ilionya mabenki kutotegemea mfumo wa message
kutoa taarifa miamala kwani sio salama sana na kuzitaka zibuni njia mpya ambayo
ni salama zaidi.
Hili
linathibitishwa na wataalam mtandao kutokana na ongezeko kubwa la uhalifu aina
ya Man
in the middle attack ambapo
mhalifu anakaa baina ya watu wa wili wanaofanya mawasiliano hasa miamala ya
kibiashara na kufanikiwa kusoma na kuchukua taarifa zinazo safirishwa na baadae
kuzitumia taarifa hizo kuiba pesa kwenye mitandao au kupata taarifa za watu.
Mbali
na hilo, wengi wame endelea kuathiriwa na uhalifu wa Phishing attack ambapo
zinatengenezwa programu tumishi feki, kutumiwa barua pepe zenye mlengo wa
kukusanya taarifa na mambo mfano wa hayo ya kidanganyifu ili kuweza kufanikisha
wizi wa taarifa pamoja na fedha.
Tukijadili
changamoto mbali mbai nchini Kenya zinazokabili taasisi za kifedha hasa
zinazotumia huduma ya fedha kupitia simu za viganjani (Mobile banking),
tuliweza kuangazia mapungufu mbali mbali ambayo bado tunayo katika bara na hasa
ukanda wa Afrika mashariki ambapo huduma za kifedha kwa njia ya simu ndio zimeshika
kasi.
Binafsi
niliwasilisha mada ya aina mbali mbali za wizi mtandao hadi sasa na namna ya
kukabiliana nazo, mahali tulipofikia hadi sasa kupitia matukio kadhaa makubwa
na mbino zilizoweza kutumika kama ambavyo tumekua tukijadili katika vikao mbali
mbali na mwisho nika zungumzia swala zima la kukabiliana na wahalifu wa ndani
kitaalam tunawaita insider threats ambao wameendelea kuwa tishio kubwa kwa
taasisis za kifedha.
Kwan
chi ya Kenya mbali na uhalifu huu wa wizi kupitia mitandao kuwa juu zaidi,
Tanzania nayo imeonekana kua na matukio mengi ya aina hii ambapo kwa ujumla
tuliangazia macho kwa ukaribu ili kuweza kutafuta suluhu kupitia mijadala
tuliyo kua nayo kwa siku tatu mfululizo.
Muhimu
ninayopenda kuasa taasisi za kifedha ni pamoja na :-
Kujenga
tabia ya kutoa elimu kwa uma ya uelewa juu wa namna ya kulinda pesa zao hasa
wafanyapo miamala kupitia mitandao ya simu au kupitia tovuti. Hili litasaidi
kupunguza idadi ya wanaojikuta kuingia kwenye matatizo ya kihalifu mtanda
(Kupoteza pesa zao) kwasababu tu ya kukosa uelewa.
Kuhakiki
wanaoshughulikia moja kwa moja udhibiti wa wizi wa fedha katika taasisis za
fedha wanapatiwa ujuzi wa kujua mbinu mbali mbali wahalifu mtandao wanatumia
kufanikisha wizi wa fedha na namna ya kukabiliana nao. Uchunguzi niliofanya
nimegundua kiasi ni kidogo sana cha wadhibiti hawa wanao jua matukio kadhaa
ambayo yameendelea kutokea ya wizi wa fedha na namna yalivyo tokea sanjari na
hatua zilizo chukuliwa kukabiliana nayo. Hii inadhihirisha kuna tatizo kubwa la
ufatiliaji ambapo lazima liboreshwe kwa kupatiwa elimu na kuhimizwa kua natabia
ya kufatili matukio.
Kuna
njia mbali mbali ambazo kwa ujumla wataalam mtandao wamekubaliana kimsingi
zifatwe ili kuweza kuzuia, na kama matukio yamejitokeza- basi namna ya
kukabiliana nayo ambazo ni nyingi kuzianisha zote kupitia andiko hili, lakini
lazima wahusika wajue na waingize katika vitendo.
Matumizi
ya teknolojia mpya zinazo weza kusaidia kupunguza wizi huu ikiwa ni pamoja na
kutotumika kwa Windows XP katika mashie zetu za kutolea fedha (ATM) pia ni muhimu kuangaziwa macho kwani kimsingi
matukio kadhaa ya hivi karibuni yamebainika yamejiri kutokana na matumizi ya
vifaa chakavu na vilivyopitwa na wakati
vya ulinzi katika taasisis za kifedha pamoja na kuwa na umakini mdogo
katika vifaa vinavyo saidia ulinzi ndani ya taasisis za kifedha.
Nitoe
wito kwa taasisi za kifedha kuhakiki ushauri wa kitaalam unaotolewa unafanyiwa
kazi ili kuweza kulinda fedha za wateja wao. Nchi ya Kenya imefanikiwa kuweka
mifumo mbali mbali kwenye taasisi za kifedha inayo mpa fursa mtumiaji kujua
kupitia jumbe pesa zinapotoka kwenye akauti zao ambapo huduma hii ni kwa
mabenki takriban yote.
Aidha,
wamekua na taratibu zinazfatwa na taasisi za kifedha za kuhakiki fedha za
wateja wa taasisi za kifeda zinabakishwa salama na kimsingi pale taasisi inapo
kiuka chombo cha serikali kinachodhibiti kinachukua hatua stahiki.
No comments:
Post a Comment