Kumeendelea
kukua kwa uhalifu mtandao maeneo mengi duniani – Huku baadhi wakitafsiri hili
linatokana na wana usalama mtandao kuonekana kulemewa (Kuzidiwa) na wahalifu
mtandao.
Hili
limepingwa katika kikao kilicho kamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, Nchini
Afrika kusini ambapo binafsi nilishiriki na kuzungumza na wenzangu kuhusiana na
namna sahihi ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao – Kubwa nililozungumzia ilikua
ni kuwa rudisha wenzangu kwenye mstari kwa kuwakumbusha juu ya taratibu
tulizojiwekea na zinazo takiwa kufatwa na mataifa yote duniani.
Pamoja
na mambo mengine, nilikumbusha umuhimu kuhakiki hatua zote za uchunguzi zinakua
katika maandishi – Zaidi, nilicho zungumza pia kinaweza kupatikana katika Habari
inayoweza kusomeka “HAPA”
Kuhusiana
na ukuwaji wa uhalifu mtandao kila mmoja wetu amekiri hili halisababishwi na
wana usalama mtandao kuzidiwa nguvu –
Lawama imeonekana kuelekezwa kwa mataifa mbali mbali pamoja na watumiaji wa
mwisho “Users”.
Lawama kwa mataifa mbali mbali – Kila uhalifu mtandao
unao jitokeza leo umekua ukitabiriwa kabla na mapendekezo kutolewa na wana
usalama mtandao isipokua tu kwa matukio machache sana mfamo, Tukio la ModPOS.
Mataifa
kupitia vitengo vyake vya kukabiliana na uhalifu mtandao vilipaswa kufatilia
maangalizo na maelekezo yanayo tolewa bahati mbaya sana mataifa mengi yamekua
hayatekelezi hili. Mara zote baada yatatizo lililotabiriwa na kutolewa
ufafanuzi kujitokeza ndipo vitengo husika katika mataifa vitaonekana kutahadharisha
wananchi wake kitu ambacho wana usalama mtandao
tumekubaliana hatua hii ya “Fire fighting” Kuangaika na tatizo baada ya kutokea
ndio hasa sababu ya kuendelea kukua kwa uhalifu mtandao.
Tukio
la hivi karibuni la uhalifu mtandao aina ya Ransomware ambao kimsingi umedumu
kwa muda mrefu na maangalizo yalisha tolewa umetumika kama mfano – Atahri za
uhalifu huu (WanaCry) inaweza kuonekana kwenye video hapa chini.
Mapendekezo:
Tumekubaliana kimsingi ya kua lazima vitengo vyetu vya kukabiliana na uhalifu
mtandao katika mataifa yetu kurudishwa kwenye mstari kwa kukumbushwa kuwa wana
jukumu la kutoa tahadhari ya matukio ya kihalifu mtandao kabla haya jotokeza na
si vinginevyo.
Pia,
Tumekubaliana kimsingi kukuza ushirikiano wa kuhabarishana taarifa za
kiitelijensia, kubadilishana uwezo na mbinu dhidi ya udhibiti wa uhalifu
mtandao ambao bado ni tishio kubwa maeneo mengi duniani.
Lawama kwa watumiaji wa mwisho – Mataifa kadhaa
yamekua na tabia ya kutahadharisha juu ya uhalifu mtandao, kupitia machapisho
na taarifa mbali mbali ila watumiaji wa mwisho wameonekana kutofatilia taarifa
hizi – Mfano uliotolewa ni takwimu ndogo zikionekana kwa watu wengi kufatilia
taarifa zinazotolewa zenye mlengo wa kuzungumzia chagamoto za uhalifu mtandao
na maeneo mengine ya muhimu.
Mmoja
wa wazungumzaji alieleza, Unapoweka taarifa mbili moja inayo husisha taarifa ya
tahadhari ya jambo muhimu na nyingine kuelezea taarifa ya msanii mkubwa
kupaikana na tukio lolote basi wengi wataonekana kufatilia zaidi taarifa ya
msanii na kuacha taarifa yenye tahadhari juu ya usalama wao katika mtandao
ambao kimsingi una hatari kubwa sana hasa kwa kipindi hiki ambapo kila kitu
kimeunganishwa kimtandao.
Aidha,
kumekua na mjadala ulio onekana kuwatetea watumiaji mtandao “Users” ambao
ulieleza lugha ngumu inayo tumiwa na wafikisha taarifa hizi unaopelekea
watumiaji kutoelewa nao unasababisha kukua kwa changamoto ya watumiaji
kutozingatia wanacho ambiwa.
Mapendekezo:
ELimu ya uelewa (Awareness program) imeshauriwa kutiliwa mkazo na kila taifa
ila pia elimu hii lazima ifate misingi saba tuliyo jiwekea mwa 2015, ambapo
tulikubaliana kimsingi ya kua inapaswa
kua ya namna nzuri na rahisi kwa kila mtumiaji kuelewa kirahisi – Kitu ambacho
mataifa mengi bado yameonekana kutofanyia kazi hili.
Binafsi,
Juu ya hili niliwasilisha kwenye wizara yetu (Nchini Tanzania) ya mawasiliano
kupitia kikao ambacho nilizungumza na watendaji katika wizara.
Pia nimepata fursa ya kuwa
na mazungumzo marefu na Mbwana, Ivo Vegter, ambaye ni mwandishi wa vitabu vya
usalama mtandao ambavyo baadhi yake nimekua nikivisoma sana pamoja na kutoa
wito kwa wawekezaji katika sekta ya usalama mtandao kuwekeza nchini – Tayari kumekua
na muitikio kwenye hili.
Aidha,
Nimezuru Jukwaa la Deloitte, Mahali nilipo wahi kufanyia kazi Nimefurahishwa
na hatua ya Deloitte kuanzisha kitengo maalum kitakacho kabiliana na uhalifu
mtandao.
Tukio la
tofauti lililojiri katika vikao vilivyo isha ni kutoa fursa ka kujumuika nasi kwa
vijana wa umri mdogo waliozidi 30 ili kuonyesha uwezo wao katika kusaidia kupambana
na uhalifu mtandao – Hatua hii imenifurahisha zaidi kwani kuwekeza kwenye
vijana wadogo wenye uwezo ni jambo ambalo hata nchini Tanzania tayari nimesha
lishauri.
Itakumbukwa
vijana wengi wadogo wamekua wakionekana kusababisha halifu kubwa za kimtandao
zilizo gharimu Nchi kubwa duniani – Rejea tukio la TalkTalk la Nchini uingereza
lililo sababishwa na kijana wa miaka 16.
Kwa ujumla kulikua na
mijadala mingi na mirefu iliyo ambatana na kuonyeshana gunduzi mpya katika
sekta ya usalama mtandao huku vikao vidodgo vidogo vya pembeni baina ya
wanausalama mtandao vikitumiwa kujadili maswala mbali mbali hasa katika kukuza
mashirikiano na kubadilishana uzoefu na usaidizi katika maeneo mengi katika
kukabiliana na uhalifu mtandao.
No comments:
Post a Comment