Nchini
Tanzania Matumizi ya TEHAMA yame endelea kukua katika maeneo mbali mbali. Hii
ime endelea kurahisisha upatikananaji wa huduma muhimu na kuwezesha watu
kuendelea kuwasiliana kwa urahisi.
Viwanda
na Taasisi mbali mbali zimeendelea kutumia TEHAMA ili kukuza ufanisi na kufikia
watu wengi kwa kipindi kifupi. Miamala ya kifedha, ukusanyaji kodi, pamoja na mawasiliano
ni baadhi tu ya mambo yanayo wezeshwa na TEHAMA nchini.
Usalama
wa mifumo ya TEHAMA ni moja ya jambo muhimu sana ambapo Tanzania inapaswa
kuwekeza ili kujilinda na aina zozote za kialifu mtandao ambazo zinaweza
kupelekea huduma muhimu kutopatikana na hatimae uchumi wa Nchi kuyumba.
-------------------
STATISTICS: Tanzania installed 27,000 KMS
of optic fiber connecting all regions and it has 7 mobile operators – About 94%
network coverage, 85% SIM
penetration and 40% internet users.
-------------------
Mkutano
mkuu wa mwaka wa wataalam wa TEHAMA nchini Tanzania ulio fanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita (26 – 27, Octoba – 2017) jijini Dar-es salaam ulipata kujadili
usalama mtandao ambapo mada kadhaa zilizo jikita katika kutoa elimu ya namna
bora za kuimarisha usalama wa mifumo yetu zili wasilishwa na kujadiliwa.
Binafsi,
Nilizungumza na washiriki kuhusiana na namna bora ya kulinda taarifa zinazo
patikana kwenye simu zetu na komputa mpakato (Protecting Mobile devises Data)
ambapo vifaa hivi vimekua vikitumika katika utendaji wa shughuli za kiofisi na
kufanya miamala ambapo taarifa hizo zimekua muhimu kulindwa dhidi yawahalifu
mtandao.
-------------------
QUOTE: “Companies today allow Individuals to make use of their own mobile
devises to perform their jobs with direct access to organization’s sensitive
data – Therefore, Data in our mobile device are very important for the
operations and financial well-being of our business.” – Yusuph Kileo.
-----------------------
Kumekua
na kawaida ya kusoma barua pepe za ofisini kupitia simu zetu za viganjani,
Kufanya kazi za kiofisi kupitia komputa mpakato binafsi tukiwa maeneo mbali mbali
huku yote haya yakipelekea kuweka taarifa muhimu za kikazi kua hatarini kuweza
kuingia katika mikono ya wahalifu mtandao endapo hatua stahiki ya kuzilinda
hazitachukuliwa.
Aidha,
Vifaa hivi vinaweza kuibiwa na taarifa hizi muhimu kuwa katika hatari ya kutumika
vibaya. Hivyo umuhimu wa kuzilinda taarifa hizi muhimu ni wajibu wa kila
mtumiaji.
Umakini
wa Programu tumishi, tunazo zi weka kwenye simu zetu ni wa kuzingatiwa kwa
kiasi kikubwa kwani kutokana na chunguzi mbali mbali ambazo tumeendelea
kuzifanya katika ngazi ya kidunia, umebaini asilimia kubwa ya program tumishi
kua na tabia ya kuiba taarifa za watumiaji na kuzitumia watakavyo.
---------------------
Non-sanctioned applications create a risk to the mobile devises and
for enterprises.
October, 2016 – The Top 10 flash App
were discovered as Malware.
Feb, 2017 – According to Cisco, 27% of
222,000 assessed applications present a high-risk.
May, 2017 –100’s of Apps investigated were all found with serious Snooping
and spying Characteristics.
---------------------
Jitihada
mbali mbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na makubaliano ya mwaka 2014 yaliyo
elekeza kila program tumishi kueleza kwa ufupi kila watakacho toa bure kwa
mtumiaji na watakacho chukua kwa mtumiaji sanjari na kutoa fursa ya mtumiaji
kukubali au kukataa. Aidha, Tuliasa watengenezaji wa Program tumishi kuhakiki
wanazilinda ili kutoruhusu wahalifu mtandao kuziingilia na kuzitumia vibaya kwa
kufanya uhalifu.
Wazungumzaji
wengine walionyesha mapungufu mbali mbali ya kiusalama mtandao yanayo patikana
nchini na kuasa taifa kufunga mikanda zaidi.
Kiujumla,
Kukuza uelewa kwa watumiaji mitandao kua na matumizi bora, Kuongezea wataalam
wetu ujuzi, Kuimarisha mashirikiano katika kudhibiti matukio ya kihalifu
mtandao, Kuondoa urasimu usio wa lazima katika kukabiliana na uhalifu mtandao, Kuwa
na watu sahihi maeneo sahihi ya kudhibiti uhalifu mtandao, na kua na vifaa
sahihi na madhubuti vya kukabiliana na uhalifu mtandao ni miongoni mwa mambo
yaliyo onekana kutakiwa kufanyiwa kazi ili kuweza kupiga hatua dhidi ya
kukabiliana na uhalifu mtandao nchini.
Matukio
ya kihalifu mtandao yanayo kumba taasisi moja hayapaswi kujirudia kwenye
taasisi nyingine – huo ulikua wito wangu kwa washiriki wote. Utoaji wa taarifa
za kialifu mtandao ili ziweze kupatiwa suluhu ni muhimu pia kwani kuficha
taarifa hizi huku matukio kuendelea kuonekana yakijirudia kunaweza kupelekea
changamoto za upotevu wa fedha kimtandao kuendelea kukua nahii ina athari kubwa
kwa uchumi wa taifa.
Wito
ulitolewa kwa vyuo vyetu Nchini kuondokana na mifumo ya kizamani iliyo nyuma na
wakati kwa kujitazama upya na kuandaa mitaala itakayo weza kutengeneza wataalam
wenye uwezo wa kukabiliana na uhalifu mtandao nchini.
No comments:
Post a Comment