KWA UFUPI:
Kutokana na ukuaji wa teknolojia pamoja na muunganiko wa vitu vingi katika
mtandao (IoT) vifaa vingi vya watoto vimekua mhanga mkubwa wa uhalifu mtandao –
Hii imepelekea kuchukuliwa kwa hutua mbali mbali za kulinda watoto mitandaoni.
Andiko hili lina angazia namna bora ya kulinda vifaa vya watoto vya TEHAMA.
-----------------------------------------
Kumekua
na matukio kadhaa yaliyo husisha kuingiliwa kimtandao (kudukuliwa) kwa vifaa
vinavyo tumiwa na watoto huku wahalifu mtandao wakiunda program tumishi zenye
nia ovu ya kukusanya picha na sauti za watoto.
Mfano,
kampuni ya V-Tech ambayo inatengeneza vifaa vya TEHAMA vya watoto Ilipata
kudukuliwa na wahalifu mtandao ambapo taarifa nyingi za watoto zilijikuta
mikononi mwa wahalifu mtandao.
Shirika
la umoja wa mataifa linalo husiana na TEHAMA (ITU) limekua na kampeni maarufu ya
Kuwalinda watoto mtandaoni – Child online protection (COP) ambayo imeongezewa
nguvu na Kampeni nyingine ya wanausalama mtandao ijulikanayo kama siku ya
usalama mtandao “Safer internet day” ambazo kwa pamoja zinatoa msaada ingawa
kuna kila sababu kwaa wazazi nao kuchukua hatua kuwalinda watoto wao kimtandao.