KWA UFUPI: Australia, Marekani na Uingereza zimeitupia lawana
nchi ya Uchina kuhusika na ujasusi mtandao katika mataifa yao na mataifa Rafiki
– Shutma ambazo zime eleza uchina kuhusika na wizi wa taarifa za siri za
kibiashara za serikali na makampuni ya Teknologia.
---------------------------
Niliwahi
kueleza mara kadhaa mwelekeo mpya na hatari wa Uhalifu mtandao ambapo
nilitahadharisha kuhusiana na vita mtandao (Cyber Warfare) pamoja na Ujasusi
Mtandao (Cyber Espionage) ambavyo kwa sasa mataifa makubwa yanawekeza zaidi
kwenye matumizi ya teknolojia kudhuru na kuingilia mataifa mengine kimtandao.
Kundi
la APT-10 la uchina limeshutumiwa na Uingereza na Marekani kuingilia makampuni
takriban 45 ya Teknolojia, Taarifa za wafanyakazi takriban laki moja za
wanajeshi wa majini wa marekani pamoja na computer mbali mbali za shirika la NASA.
#Infosec #Cybersecurity - - - Australia has joined The US and UK to accuse China of attempts to steal data through #cyberattacks— YUSUPH KILEO (@YUSUPHKILEO) December 21, 2018
Zhu Hua pamoja
na Zhang Shilong, ambao ni raia wa
Uchina wameshtakiwa na Marekani kuhusika na kufanya mashambulizi mtandao
kwaniaba ya wizara ya ulinzi ya uchina (Chinese Ministry of State Security) –
Naibu Mwanashria mkuu wa Marekani , Bwana Rod
Rosenstein alielezea shutma hizo.