KWA UFUPI: Steffan Needham,
Amabae alihudumu kama mshauri wa maswala ya tehama (IT Cosultant) katika
kampuni ya Voova ya nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka 2 Jela kwa kosa
la kuharibu taarifa za muajiri wake wa wa zamani.
--------------------------------
Kwa
mujibu wa Thames Valley Police ya Nchini Uingereza, Mtuhumiwa alifukuzwa kazi
na mwaajiri wake na baadae kuharibu taarifa zote muhimu za kampuni hiyo kwa
kile kilicho tafsiriwa kama kulipiza kisasi kutokana na kufukuzwa kwake.
Uharibifu
wa taarifa umekadiriwa kuigharimu kampuni hiyo kiasi cha Dola laki sita na
elsfu Hamsini (US$650,000) ikiwa ni pamoja na kupelekea wafanyakazi kadhaa
kupoteza kazi zao.
Mtuhumiwa
amehukumiwa chini ya sheria ya nchini Uingereza ya mitandao (Computer Misuse
Act)