WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday, 12 May 2015

UMUHIMU WA USHIRIKIANO KWENYE VITA DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

Nianze mada hii kwa kurudia pongezi kwa rafiki yangu Bwana Joe, Kwa kuongezewa nguvu na Nchi yake ya Marekani. Tayari taarifa rasmi ya hili nimeiandikia, na inaweza kusomeka zaidi kwa “KUBOFYA HAPA”. Bwana Joe amekua na imani inayofanana sana na yangu kwa muda mrefu ya kua uhalifu mtandao ni mbio za sakafuni endapo hapatakua na ushirikiano thabiti.

Kume kua na hoja nyingi kutoka mataifa mbali mbali juu ya kusua sua katika ushirikiano unao vuka mipaka huku uhalifu mtandao kutotambua mipaka iliyopo katika mataifa yetu. Uhalifu mtandao umeendelea kufanyika huku ukivuka mipaka na athari kuendelea kushika kasi ya aina yake hivi sasa.

Nategemewa kuangazia changamoto kadhaa tulizo nazo katika bara la Afrika na nini kifanyike katika hotuba yangu kwa wataalam mbali mbali wa usalama mitandao baadae mwezi huu jijini Johannesburg ambapo changamoto kubwa iliyoafikiwa na wanausalama kutokea maeneo yote duniani ni kukosekana kwa ushirikiano wa dhati na endelevu katika kupambana na uhalifu mtandao.

Hili limekua ni tatizo zaidi nchini Tanzania kwani hata ushirikiano wa ndani umekua ukiyumba sana baina ya vitengo mbali mbali vinavyo husiana na usalama mitandao nchini licha ya kua na malengo yananyofanana ya kutokomeza uhalifu mitandao. Kuna kila haja ya kujiangalia zaidi kwenye hili hasa kwa sasa tunapo hitaji zaidi kua na mipango pamoja na mikakati madhubuti ya kuweza kufikia malengo ainishwa.

Ku sainiwa kwa sharia mtandao kunatoa fursa ya vitengo kadhaa vilivyoko nchini kufanya kazi yake kwa kujua vitafanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao unaokua kwa kasi nchini. Lakini Hofu yangu kubwa ni ushirikiano dhaifu kwa vitengo hivi ambapo watu na vitendea kazi kwa mgawanyo wake ni dhahiri kabisa malengo yatafikiwa kwa kiasi kidogo sana.

Nimekua nikipitia kiandikwacho (Maoni ya wengi) juu ya hofu ya utayari tulio nao kama taifa na najua kila mmoja anashaka kua utayari kama taifa bado ni hafifu – Mimi niko tofauti kwenye hili. Rais, Dr. Kikwete amewekeza sana katika kuimarisha miundo mbinu ya TEHAMA nchini huku wahisani wakichangia baadhi ya vitendea kazi.

Tatizo ni kua vitendea kazi vimekua vikigawanywa katika vitengo vilivyomo nchini vinavyo jihusisha na maswala ya usalama mitandao huku watenda kazi wakigawanywa hivyo hivyo licha ya kuwa na nguvu kazi ndogo sana kulinganisha na wahalifu mtandao.

WITO:
Kama taifa lita hakikisha limekuza nguvu kazi kupitia (Capacity building) na kutengeneza nguvu kazi za ndani kama inavyo fanywa na mataifa mengine sasa na kuhakiki hili limekua endelevu kuna hatua kadhaa tutapiga. Hili litakaa vizuri endapo kutakua na ushirikiano thabiti na endelevu hivyo:-


1.     Vitengo vyote vilivyoko nchini havina buni kuwa kitu kimoja na kuhakiki hakuna kimoja kinachodhani kiko juu ya mwenzake.

2.     Ushirikiano wa taarifa, Vifaa na ujuzi baina ya vitengo vyote vya ndani iwe ni kitu cha lazima.

3.     Kukuza ushirikiano na mataifa mengine katika utendaji na kujifunza zaidi iwe ni moja ya desturi zetu.

4.     Wahusika wote kujua ushirikiano unaambatana na kuhakikisha – Kila mmoja ana kila sababu ya kutambua umuhimu na faida zinazopatikana kwa kushirikiana.


5.     Vitengo vyote vilivyoko- Kipatikane kimoja kitakachokua ni HUB au kiunganishi ya vingine vyote ili kuweza kufikiwa kwa malengo tegemewa.

1 comment:

  1. kaka nashkuru kwa maneno yako mazuri kweli kabisa bila ushirikiano katika kila kitu lazima pawe na ugumu wa mambo kusgea.
    Niko Mlimani mwaka wa 2 natamani sana kuwa kama wewe je, nini nifanye? au njia gani nipitie?

    ReplyDelete