ANGOLA
Imekumbwa na Shambulio la kimtandao kutoka katika kundi la wahalifu mtandao
wajulikanao kama “Anonymous” ambapo
tovuti 20 za serikali ya Nchi hiyo zimefanikiwa kuangushwa na kundi hilo la
kihalifu mtandao.
Tukio
hilo lilitokea kufuatia shinikizo la kuachiwa huru watu 17walioshikiliwa nan
chi hiyo kutokana na kosa la wakipingana
na uongozi wa raisi wa Nchi hiyo Mh. Jose Eduardo dos Santos.
Tukio
hilo la kushambuliwa kwa tovuti za Nchi ya Angola limepokelewa kwa Maskitiko
makubwa sana na wana usalama mtandao wa Nchi za Afrika na imeonekana changamoto
iliyojitokeza iwe ni funzo kua mataifa ya afrika bado yanahitaji jitihada za
dhati kuhimili vishindo vya wahalifu mtandao.
------------------------
NEWS
UPDATES: A Portuguese branch of the Anonymous hacking group says it has shut
down about 20 Angolan government websites in retaliation for the jailing of 17
youth activists for plotting a rebellion against President Jose Eduardo dos
Santos' government.
-------------------------
GHANA
ilipata kuathirika na tukio la kuangushwa tovuti zake mwaka jana kitu ambacho
kilipelekea Nchi hiyo kupitia Makamu wake wa Raisi kujipanga zaidi kuhimili
vishindo vya kihalifu mtandao.Taarifa zaidi kuhusiana na tukio la Ghana inasomeka
kwa ku “BOFYA HAPA”
TANZANIA
Imepata kuathirika na tatizo la kuingiliwa tovuti kadhaa kipindi cha nyuma na
kusababisha tovuti husika kushindwa kutoa huduma na mara nyingine kuingiziwa
vitu visivyo faa.
KENYA
Pia Ilipata kuathirika kwa kiasi kikubwa kwa tovuti zake kitu kilicho sababisha
baadhi ya tovuti kufungwa moja kwa moja – Tulipata kujadili hili kwa kina nilipo
udhuria mkutano wa usalama mitandao wa Nchi za Afrika mashariki uliofanyika
mwaka jana nchini Kenya.
UGANDA,
kuimarisha amani ya nchi hiyo kipindi cha uchaguzi mwaka Huu ililazimika
kufunga mitandao yake ya kijamii pamoja na mifumo mingine ya kimtandao ikiwa ni
hofu ya amani kuyumba. Huu ni mfano ulio hai wenye mazingatio makubwa ndani
yake.
AFRIKA kwa ujumla wake matukio kadhaa yamepata
kutokea nabado yame endelea kutokea
ambapo ni zao la kutotiliwa mkazo swala zima la ulinzi mitandao kwa Nchi
zetu barani Afika kitu ambacho nadhani imefika wakati pakatiliwa manani
mapendekezo ambayo yamekua yakitolewa ili kuweza kubakisha bara letu salama
kimtandao.
DUNIANI
kote kumeendelea kuzaliwa makundi lukuki
ya Kiahalifu mtandao amabapo yameendelea kusababisha maafa makubwa maeneo mbali
mbali Duniani – Mfano Kundi la “Carnabanak” tayari limefanikiwa kuiba ma bilioni
ya kimarekani hadi sasa kwa mujibu wa Ripoti iliyo wasilishwa mapema mwaka huu.
Uchumi,
Utamaduni, Siasa, Upatikanaji wa Huduma Muhimu ni kwa uchache tu wa mambo
ambayo yameendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa kupitia uhalifu mtandao.
Juhudi
mbali mbali bado zinaonekana ingawa kiujumla wake Nchi za Afrika bado
zimeonekana kutoa uzito mdogo sana kukabiliana na tishio kubwa la uhalifu
mtandao.
Kumekua
na baadhi ya Nchi za Afrika zilizo fanikiwa kuwa na Sheria mitandao ambapo
baadhi bado zimeendelea kua na changamoto. Kuwapo na Sheria pekee bado imekua
ni changamoto kwani vinavyo takiwa kwenda sambamba na sheria hizo ili kuweza
kufikiwa malengo tarajiwa bado havitiliwi uzito.
Hili
limesababisha uhalifu mtandao kuendelea kutikisa na kuathiri jamii zetu huku
baadhi kushindwa kujua athari hizi
zinaweza kupelekea mambo mengi kujitokeza. Kuyumba kwa Uchumi, Kupoomoka kwa
maadili, kutikisika kwa amani na Kutopatikana kwa huduma muhimu zinapo hitajika
ni miongoni tu kwa uchache kwa kinachoweza kuleta shida ndani ya mataifa yetu
ikiwa ni zao la kukithiri uhalifu mtandao.
Bado
imekua ni aghlab kusikia wakuu wa Nchi za Afrika kuzungumzia maswala ya usalama
mitandao isipokua tu pale wanaposhiriki makongamano ya kiusalama mitandao.
Natoa
wito kwa Nchi zetu za Afrika kuhakiki zinawekeza zaidi kulinda mifumo yetu ya
kitehama ili kuweza kusababisha athari kubwa zinazotokana na uhalifu mtandao
kutoshika kasi kama ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment