Moja
ya udhaifu mkubwa unao kumba mataifa mengi hasa barani Afrika ni kutokua na
mikakati ya uzuizi na endelevu dhidi ya uhalifu mtandao. Imethibitika kua Nchi
nyingi zimekua zikingoja tatizo litokee ndio jitihada zinachukuliwa kutatua
tatizo huku athari ikiwa imeshaonekana.
Mwaka
huu baada ya Nchi ya Ghana kua miongoni mwa waathirika wa uhalifu mtandao ambapo mtandao mkuu wa serikali ya nchi hiyo inao
hudumia tovuti 58 za serikali ulidukuliwa na kusababisha tovuti 11 kuingiliwa
na kuathiriwa na wahalifu mtandao; waziri wa mawasiliano wanchi hiyo Dr. Edward
Omane Boamah ametangaza mapambano dhidi ya uhalifu mtandao ili kulinda usalama
mtandao wanchi hiyo.
Tukio
hilo la udukuzi baadae CERT ya nchi hiyo
yenye dhamana ya kutambua na kuzuia
uhalifu mtandao kabla haujatokea pamoja na na kuhakiki usalama mtandao wan chi hiyo
unaendelea kubeba sura njema ilisema wahalifu mtandao walifanikiwa kudukua tovuti
hizo za serikali na kuziathiri vibaya kutokana na mapungufu ya kutokua na
program zinazoendana na wakati katika tuvuti
hizo.
Katika
hotuba iliyosomwa na Patricia Dovi Sampson kwa niaba ya waziri wa mawasiliano
wa Nchi hiyo katika jukwaa la wadau wa maswala ya usalama mitandao Julai Mosi mwaka huu 2015, iliainisha kua nchi hiyo
tayari imetengeneza sera na mkakati wa taifa wa usalama mtandao (National Cyber
Security Policy and Strategy (NCSPS) document) ili kupambana na uhalifu mtandao
nchini humo.
Ikisisitiza
Hotuba hiyo ilieleza, Nchi hiyo
inatambua kua uhalifu mtandao hauna mipaka kwani wahalifu udukuzi wa tovuti za
serikali ya nchi hiyo ulionekana wametokea
nchini Uturuki. Hivyo ikaelezwa, Nchi hiyo itaimarisha zaidi ufanyaji kazi
dhidi ya uhalifu mtandao kwa ushirikiano na mataifa mengine ili kufikia
malengo.
Hotuba
hiyo pia ilihimiza vyombo vya habari kuongeza jitihada za kukuza uelewa wa
maswala ya usalama mitandao kwa wanachi wa Nchi hiyo kwani uelewa bado umekua
mdogo sana unaosababisha uhalifu mtandao kuzidi kushika kasi nchini humo na
kuathiri uchumi kutokana na makampuni ya Kifedha ya Nchi hiyo kuonekana
kuathiriwa zaidi.
Aidha,
Mshauri mkuu wan chi hiyo katika maswala ya usalama Mtandao Bwana. Albert
Atwi-Boasiako, alieleza mafunzo ya uelewa yanayo paswa kufanywa kwa taasisi za
serikali na zisizo za serikali bado ya kiwango cha chini sana kwa kiasi kikubwa
hali inayo sababisha taasisi hizo kushindwa kuwa na mikakati stahiki na
endelevu ya kutambua na kudhibiti uhalifu mtandao kabla haujatokea.
Hivyo
mshauri huyo alitoa Wito kwa taasisi
hizo kua na mipango madhubuti ya kujipatia elimu za ufahamu dhidi ya uhalifu mtandao
ili kuweza kubaki salama na kupunguza uhalifu mtandao unao kua kwa kasi Duniani
kote.
Katika
kuhitimisha hotuba ya Waziri wa Mawasiliano Wa Nchi ya Ghana, wito ulitolewa wa kua na njia rafiki ya
ukusanyaji wa taarifa na kupata Takwimu sahihi zitakazo onyesha kiwango cha uhalifu mtandao
huku intelijensia ya utokeaji wa uhalifu huo ikifanyiwa kazi ipasavyo ili kuhimili
vishindo vya uhalifu mtandao nchini humo.
Nini Taifa la TANZANIA linajifunza
kutokana na hili?: Ikumbukwe Tanzania pia imekua ni
miongoni mwa nchi zilizo ainishwa kua na tabia ya kukabiliana na uhalifu
mtandao baada ya kutokea imeaminika njia za kutambua na kudhibiti uhalifu kabla
haujatokea bado ni tatizo na jitihada za dhati zina hitajika.
Kwa
upande wa Sera na mikakati wa maswala ya usalama mitandao bado taifa Halina
kabisa hadi sasa kitu ambacho ni changangamoto kubwa katika kupambana na
uhalifu huu mtandao.
Pia
Uelewa na nguvu kazi watu imeendelea kua changamoto huku nguvu kazi chache
zilizoko kutotumiwa vizuri na taifa. Aidha, ushirikiano kuanzia ngazi ya taifa
pamoja na kuvuka mipaka bado umeendelea kua changamoto kubwa inayo paswa
kutafutiwa suluhu.
Upambanaji
na uhalifu mtandao lazima uwe na mikakati na kuhaki njia stahiki zilizopendekezwa na wataalam wa
usalama mtandao duniani kote zinafatwa ipasavyo ili kuhakiki taifa linabaki
salama kimtandao – Bado kumekua na kusua sua kwa kuwekeza katika maswala ya
usalama mitandao Nchini huku Taifa kuonekana kupiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA ambapo Serikali ya
Awamu ya Nne imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwekeza katika Miundo mbinu na
ukuzaji wa matumizi ya TEHAMA Nchini.
Ukuaji
huu wa kasi wa Miundombinu na utumiaji wa TEHAMA ikumbukwe inaambatana kabisa
na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao Nchini. Hivyo jitihada za dhati na haraka
katika kukabilia na Hali tete ya hapo baadae kimttandao zina hitajika hasa
Baada ya TANZANIA kuorodheshwa kua ni Nchi ya 6 Inayotegemewa kuathirika zaidi
na uhalifu mtandaokatika mwaka wa 2015/2016 huku Ransomeware kwa mara ya kwanza
kuonekana kuathiri taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment