Nchi
ya Tanzania ya bahatika tena kwa mara ya tatu kua mwenyeji wa mkutano wa “Connect
2 Connect” ambapo kauli mbiu ya mwaka huu imekua ni Kuunganisha bara la afrika
mwambao hadi mwambao. Katika hotuba iliyotolewa siku ya kwanza katika ufunguzi
wa mkutano huo ili elezea changamoto kubwa za usalama mitandao na namna
unavyoweza kuleta athiri kwa kiwango kikubwa endapo usalama huu mtandao
hautaangaziwa macho. Hotuba hiyo pamoja na mjadala nilio ongoza kwa siku ya
kwanza unaweza kusomeka na kuonekana kwa “KUBONYEZA HAPA”.
Mkutano
huu wa mara hii uliokusanya washiriki kutoka katika mataifa 30 duniani
kote ulihusisha wafanya maamuzi ya juu,
watengeneza sera na wadau wengine kadhaa ambapo Mawaziri na Manaibuwaziri wa Nchi kadhaa wkiwa ni miongoni mwa waliopata
kuongoza mijadala pamoja na kuunganisha mawazo katika maswala mbali mbali ya
barani Afrika.
Kongamano
hili la mwaka huu lililoandaliwa kwa kushirikiana wizara ya Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia pamoja na kampuni ya simu
ya TTCL limeonyesha mafanikio makubwa sana kwa kuwezesha kauli mbiu ya mwaka
huu kufikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia mijadala mbali mbali iliyo jadiliwa
katia kongamano hili.
Mbali
na mada nyingine mbai mbali – Kwa siku zote mbili za mkutano huu mijaadala mizito
ya usalama mtandao ilipata kujadiliwa kwa kina ambapo nilipata bahati ya
kuongoza mjadala wa siku ya kwanza na kuhutubia kwa siku ya pili juu ya maswala
ya usalama mitandao.
Katika hotuba yangu ya siku ya pili katika mkutano huu
nilipata kuangazia hali ilivyo duniani kote na kueleza kwa kifupi kuhusiana na
Mkutano mkuu wa mwaka ulioangazia maswala ya usalama mitandao jijini Johannesburg
ambapo pia nilihutubia kwa niaba ya Bara la Afrika tulipo kutana wataalam wa
maswala haya katika ngazi ya dunia. Zaidi niliweza kuainisha mapungufu makuu
tuliyo nayo yanayo sababisha vita dhidi ya uhalifu mtandao kuenekana kutushinda
kutokana na uhalifu huu mtandao kuendelea kushamiri.
Msisitizo
mkuu nilio toa mbali na kuhimiza ushirikiano na kutumia vizuri wenye ujuzi na
elimu hii ya usalama mitandao, Nilipata kuainisha makundi ma nne ambayo ni Mtu
binafsi, kundi la Watu ( Wana usalama mitandao), Kampuni , pamoja na serikali
na kueleza kuna dhana potofu inayo dhani makundi matatu kati ya hayo manne ndio
yenye dhamana ya usalama mtandao na kusahau kabisa kua lazima usalama mtandao uanzie
katika ngazi ya MTU BINAFSI.
Nikitolea
hili ufafanuzi – Nilielezea mtu binafsi anakila sababu ya kuhakiki usalama wake
uko vizuri kwa kuhakiki neno la siri “Password” Matumizi ya salama ya mitandao
na kuhakisha kila hatua za kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao kama ilivyo
katika hali ya kawaida ya kulinda makazi yetu zina angaziwa vizuri kwani jukumu la kulinda usalama mtandao si la kundi
flani la watu pekee.
Nikiwa na waziri wa TEHAMA - BURUNDi |
Waziri
wa TEHAMA wa Burundi katika mazungumzo yake mkutanoni na baadae tulipo
kutana kwa mazungumzo baina yetu
alionyesha dhahiri matumizi mabaya ya mitandao hasa hii ya kijamii ilivyo
changia kuyumbia taifa la Burundi huku akiendelea kutoa wito juu ya matumizi
salama ya mitandao ya kijamii ili kuweza kuchochea usalama wa taifa lolote
duniani – Katika kuumunga mkono nilimpatia mifano kadhaa ya Nchi kama Misri,
Libya na nyinginezo ambazo ziliyumba na kuanguka huku sababu kuu ikiwa ni
mitandao ya kijamii kuchochea fujo katika nchini hizo.
Niliwa na Waziri wa TEHAMA - LETHOSO |
Nilifarijika
kuona Nchi ya LETHOSO pamoja na NAMIBIA kuonyesha dhamira yao ya dhati ya
kutaka kujifunza kutoka kwetu kwenye maswala haya ya usalama mitandao na
kupongeza hatua nzuri tuliopiga hadi leo. Katika mazunungumzo yangu na Waziri
wa TEHAMA wa LESOTHO alinieleza wimbi kubwa na matumizi mabaya ya mitandao
nchini mwake ndio limeendelea kua kikwazo na ana mikakati ya kuandaa sera
pamoja na sheria mitandao ili kuhakiki ana himili vishindo vya ukuaji wa
matumizi mabaya ya mitandao.
Aidha,
Kwa upande wa NAMIBIA – Mbali na kunipongeza walionyesha dhamira ya yadhati ya
kufanyia kazi ushauri niliotoa katika mkutano huu, huku wakisisitiza kua
wanaamini kabisa tatizo kubwa ni upungufu wa ukuzaji wa uelewa juu ya mambo ya
usalama mitandao pamoja na serikali nchini afrika kutoona Usalama mitandao ni
kipa umbele na wakisahau Uhalifu mtandao unauwezo mkubwa wa kuangusha taifa
lolote.
Mwisho,
Nitoe wito kwa serikali ya Tanzania na wadau mbali mbali kutambua athari kubwa
katika Nyanja zote kuanzia kiuchumi hadi kisiasa zinazoweza kuonekana kama
usalama mtandao hauta angaziwa macho ipasanyo. Wakati huu tukiwa tunaelekea
uchaguzi mkuu lazima tujue mitandao ya kijamii inaweza kabisa kuyumbisha taifa
letu hivyo hakuna budi kuwa na umakini madhubuti katika hili. Tayari nimesha
lizungumzia hili mara kadhaa na zaidi unaweza kupitia Andiko linalosomeka kwa “KUBOFYAHAPA”
No comments:
Post a Comment