Bwana
Chris Gibson, Mkurugenzi mkuu wa CERT (Computer Emergence Response Team) ya
Nchini Uingereza yenye dhamana ya kubaini na kudhibiti uhalifu mtandao nchini
humo ametangaza rasmi kuunga mkono kauli ya mwaka huu ya wanausalama mitandao ambayo
Niliizungumzia rasmi na kuitolea ufafanuzi katika mkutano wa wanausalama
mitandao tulipo kutana jijini Johannesburg mwaka huu mwezi wa Tano mwishoni.
Kauli
hii ya ushirikiano nilipo izungumzia, wataalam wote katika mkutano huo
waliiunga mkono na sasa kupitia mkutano wa wanausalama mitandao wanchi ya
uingereza uliokamilika Jijini London Mkuurugenzi mkuu wa CERT ya nchini
Uingereza amesisitizia hili kwa kusema
vita dhidi ya uhalifu mtandao itakua ngumu kama ushirikiano utakua hafifu.
Itakumbukwa
mwaka 2013 CERT ya uingereza ilizindua CISP – Cybersecurity Information Sharing
Partnership, iliyodhamiria kutoa fursa ya kukuza ushirikiano wa kubadilishana
taarifa za uhalifu mtandao nchini humo huku mashirika binafsi na serikali
zikitegemewa kupiga hatua dhidi ya uhalifu mtandao.
Hili
la kushirikiana kwa taarifa za uhalifu mitandao baina ya makampuni pamoja na
serikali nililitolea ufafanuzi katika mkutano wa wanausalama mitandao 2014
Nchini Cyprus na kusema imefika wakati makampuni yakawa na tabia ya kutoa
twakwimu stahiki za uhalifu mtandao sanjari na inteligensia ya uhalifu huu ili
kuhakiki namna ya uhalifu huu unavyo fanyika unabainishwa na kutoa fursa ya
udhibiti kupatikana mapema.
Maelezo
hayo ambayo baadae yaliweza kuingizwa katika moja ya jarida la usalama
mitandao, Nilielezea kwa kina namna hatua ya ushirikiano wa kupeana taarifa za
uhalifu mtandao baina ya Makampuni inavyoweza kusababisha uhalifu ulioathiri
kampuni moja au nchi moja kutojirudia kwa nyingine kwani tayari kutakua na ufahamu
wa uhalifu usika kutokana na kushirikiana katika kubadilishana taarifa za
uhalifu mtandao baina ya makampuni au Nchi.
Aidha,
katika kuongezea juu ya hili bado naona changamoto kubwa kwa mataifa mengi ikiwemo Tanzania ni
kutokuwepo na mikakati madhubuti ya kutambua na kubaini uhalifu mtandao sanjari
na kuchukua hatua za haraka kudhibiti mara unapokua umetokea kituambacho
kimeendelea kusababisha uhalifu huu kuendelea kushika kasi zaidi hivi sasa.
Takwimu
zinaonyesha Asilimia zaidi ya 71 ya uhalifu mtandao umeendelea kutikisa anga ya
usalama mitandao na kubainika kwake kumechukua zaidi ya miezi mitatu kitu ambacho ni hatari
na kinarudisha nyuma ushindi dhidi ya uhalifu mitandao.
Nchini
Marekani Udukuzi uliogundulika wiki mbili zilizo pita uliosababisha taarifa za watu zaidi ya Milioni Arubaini na moja kuibiwa na wahalifu mtandao ambapo kwa sasa taarifa hizo zimeendelea kuzua mijadala mirefu baina ya wanausalama mitandao baada ya kubainika uhalifu huo umechelewa
kugundulika na tayari athari kubwa imeonekana kutokana na tukio hilo, jambo ambalo
limepelekea mkuu wa FBI wa Nchi ya Marekani
kuthibitisha mategemeo yake ya matukio kadhaa mfano wa hilo kutokana na udhaifu
wa ugunduzi wa mapema wa matukio ya uhalifu mtandao.
Hili
bado libaki kua funzo kwetu kwani yote hayo yanayo jiri katika mataifa mengine
yanaweza kujirudia barani Afrika na hasa Nchini Tanzania. Udhaifu wa kuto
shirikiana katika kupeana taarifa za uhalifu mtandao bado ni changamoto kwetu nabado
tumekua tukitegemea mabadiliko katika udhibiti wa uhalifu huu.
Mfano,
uhalifu Mtandao Aina Ya “Spearfishing” bado umeendelea kutoa athari kubwa nchini Tanzania na kumekua na jitihada ndogo
za kukuza uelewa dhidi ya uhalifu huu huku kuubaini na kudhibiti kua bado kuko
chini. CERT ya nchini Tanzania yenye dhamana ya kubaini na kuzuia uhalifu mtandao
kabla ya kuleta athari Nchini inakila sababu ya kujifunza zaidi kutoka kwa
wengine na kuhakiki inaingiza katika vitendo yale ya msingi yanayopatikana ili
kuhakiki Taifa linaendelea kubaki salama.
Aida,
Nitoe wito kua kama ilivyo udhibiti wa uhalifu wa kawaida ambapo unapelekea mtu
momoja kuweka milango, Madirisha na mengineo na baadae kuunda vikundi binafsi
vya sungu sungu kuweza kuimarisha ulinzi na baadae kutegemewa Polisi wenye
dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao kuuendeleleza ulinzi – Dhana hii lazima
ielekezwe katika mitandao ambapo kila mmoja anapaswa kujua anadhamana ya
kujiweka salama binafsi na kuunganisha nguvu baina ya vikundi vidogo huku
vitengo venye dhamana ya kulida mitandao katika ngazi ya taifa kuendelea kutoa
msaada stahiki.
No comments:
Post a Comment