Ili
kuwezesha upatikanai rahisi wa huduma za mtandao – Mahoteli, Viwanja vya ndege
na maeneo mengine ya mkusanyiko wa watu kumekua na huduma ya Mitandao inatolewa
kupitia teknolojia ya “Hotspot – Wi-Fi” ambapo imeendelea kua na umaarufu
mkubwa hivi sasa.
Kama
ilivyo katika maeneo mengine ya Hili nalo limekua na upande wa pili ambapo kumeibuka
wimbi la wahalifu mtandao wanaotumia udhaifu uliyoko kwenye huduma hizi za bure
za “Wi-Fi – Hot spot” kudukua na kuleta
madhara kwenye mtandao.
Wahalifu
mtandao wamekua wakiweka “Wi-Fi” za bure ambazo si sahihi “Fake” ambapo
wanategemea watu wengi watazitumia na baadae kukusanya taarifa zao na kufatilia
vinavyosambazwa kwenye mtandao na baadae kupelekea kufanikisha uhalifu mtandao.
Kampuni
ya usalama mtandao ya “Avast” hivi karibuni imefanya jaribio la kuangazia
uelewa wa watu juu ya huduma hizi za bure za kujipatia mtandao “Free Wi-Fi” ambapo
kampuni hiyo iliweka idadi kadhaa ya “Fake Free (Hot spot) Wi-Fi” kwenye
mkutano wa Kisiasa nchini Marekani “Republican National Convention”.
---------------------------------------------------
NOTE: "Travellers should be conscious of
hackers who will attempt to physically steal laptops, tablets and cell phones
from luggage, hotel rooms or coffee shops when they are left unattended"
---------------------------------------------------
Takwimu
zlizo kusanywa na Kampuni hiyo zinasema watu zaidi ya 1200, Walitumia huduma hiyo iliyokua imewekwa kwa mtego na asilimia
68.3 walitoa taarifa zao binafsi. Huku
ikielezwa mashindano ya Olympik hili pia linategemewa kujitokeza.
Aidha,
Takwimu za jaribio hili ziliendelea kueleza – aribio lilifanikiwa kufahamu Asilimia
38.7 walitumia Facebook; asilimia 13.1 walitumia Yahoo Mail, asilimia 17.6
waliperuzi barua pepe zao kupitia Gmail,
na Asilimia 13.8 walitumia programu zyingine za kuwasiliana kama vile WhatsApp, WeChat pamoa na Skype.
Kiuhalisia
kama zoezi hili lingekua limefanywa na wahalifu mtandao, Hakika wangefanikiwa
kudukua kila kinachopatikana kwenye mifumo ya washiriki kaika mkutano huo ambapo
jaribio hili lilifanywa. Na hii ni hatari zaidi hasa pale unapo tumia kifaa cha
ofisi kilichokusanya taarifa muhimu/za siri ambazo hazikutakiwa kuangukia
kwenye mikono ya asiye husika.
-----------------------------------------------
NOTE: “users should never insert CDs, disks or
thumb drives they found into their devices. Hackers drop these items at public
places specifically to get unsuspecting individuals to plug them into their
devices in order to infect them."
-------------------------------------------------
MJADALA WA WANAUSALAMA
MTANDAO KWENYE HILI:
Kumekua
na utupianaji wa lawama kwenye hili mabapo imesemekana kwa sasa ime endelea kua
ngumu kujua huduma hizi za bure zilizo sahihi (genuine) na zisizo sahihi
(fake).
Jerry
Irvine, Mwana usalama mtandao yeye ameeleza kuwepo kwa viwezeshi lukuki na
urahisi unao vizunguka kwa kila mmoja kuweza kutengeneza hili imekua ni
changamoto kubwa hivi sasa.
Huku
bwana Gary Davis, mwana usalama mtandao kutokea kampuni ya Intel akifafanua ya
kua sababu kubwa inayopelekea wahalifu kuendelea kufanikiwa katika zoezi la
kuibia watu pesa zao mitandaoni “Fraud” ni kutokana na upatikanai rahisi na wa
kiholela wa viwezeshi vinavyoweza kusababisha komputa ya mtu kuwa kama “Wi-Fi
hotspot”.
Niki
changia hili, Nilieleza kwenye mikutano na mikusanyiko mingine kumekua na
taratibu ya kupatiwa “Free Wi-Fi” ambapo tumekua tukizitumia bila hata
kujiuliza maswali yoyote kwani tayari imesha kua kawaida hasa pale utakapo kuta
imepewa jina linalo wiana na mkutano husika au tukio linalo endelea na wakati
mwingine eneo ulilopo kitua ambapo kinapelekea urahisi wa wengi kuwa wahanga
pale wahalifu mtandao wanapo kua wamedhamiria kufanya uhalifu mtandao.
DHAMIRA YA WAHALIFU
MTANDAO NININI KWENYE HILI:
Mara
zote wahalifu mtandao wanapo lifanya hili wanadhamiria kufanya kitu ambapo
kitaalam tuna kiita “Man in the Middle (MitM) Attack” inayotoa fursa kwa
mhalifu mtandao kunakili kila kinachosafiri kwenye mtandao kwa yule atakae
tumia huduma yao hiyo (Wi-Fi)
Ikumbukwe
kwa huduma zile ambazo zinatumia teknolojia ya “HTTPS” ambapo inaaminika huwa
ziko salama nazo si salama sana kwani si kila kinacho safari kupitia teknolojia
hiyo hakiwezi kuonekana/kusomeka na wahalifu mtandao pale unapo kua umeingia
kwenye mtego wao kwa kutumia huduma yao (Wi-Fi)
Hivyo
wanapo fanikisha kupata mtu ametumia huduma yao (Wi-Fi) wanatumia njia ya
usafirishaji wa taarifa kuingilia kwenye kifaa unachotumia (Simu au Komputa) ambapo
wataiba taarifa, kuingizia virusi vinavyoweza kuathiri kifaa chako na wakati
mwingine kusababisha uhalifu mwingine wowote.
SULUHISHO
KWENYE HILI
Kubwa zaidi,
kwa wale wanao jijua wanakua na mahitaji makubwa ya mtandao, wawe na vifaa vyao
binafsi vinavyo weza kuwapatia huduma ya mtandao hasa wa wapo safarini. Kwa
kufanya hivyo inakupa fursa ya kujua untumia mtandao kupitia kifaa unacho kijua
(Mfano: Modem)
Njia
nyingine unaweza kutumia sumu yako – Ambapo unafungua “data” na kuiruhusu kua “Hotspot”)
baadae kuitumia kujipatia mtandao. Kwa kufanya hivi pia inakupa fursa ya kujua
mtandao unao utumia.
Aidha,
Pale unapo ona njia mbili za awali huna, nabado una mahitaji ya mtandao unaweza
kutumia “Hotspot” inayopatikana katika eneo husika ila, Hakikisha haikuhitaji
uingize taarifa zako binafsi kabla ya kuanza kupata mtandao na pia ujenge tabia
ya kuhakiki kama ni sahihi ambapo unaweza hata kuuliza tu kwa mhudumu kama
unayopaikana/ iona kweli ni ya kwao.
MUHIMU: Epuka kufanya miamala ya kifedha au
kusafirisha taarifa za siri pale unapokua umetumia njia ya pili ambayo inakuja
tu pale unapokua hauna namna nyingine. Hii ni kutokana na kujitengenezea
mazingira ya kulinda taarifa zako na fedha zako dhidi ya wahalifu mtandao.
Kuna
teknolojia ambayo ipo kwa ajili ya kutatua tatizo la mhalifu kuweza kufatilia
kinacho safari ambapo ina julikana kama “Visual private Network – VPN” ambapo
inalinda mawasiliano yako unapo tumia hizi huduma za mtandao zinazopaikana
maeneo ya Umma pamoja na kulinda kifaa chako unachotumia. Ni vizuri tukajenga
tabia ya kutumia teknolojia hii.
BINAFSI HIVI KARIBUNI
NILIATHIRIKA KWENYE HILI
Hivi
karibuni, nilipokua kikao Pretoria, Nchini Afika kusini – Nilitumia huduma hii
baada ya kuona imepewa jina la mkutano na baada ya muda nilikuta program zangu
kwenye simu zote hazipo na nikaamua kuondoka mtandaoni ili kuweza kufanya
marekebisho ya kilichoni sibu na baadae nilijikuta nime lazimika kufuta kila
kitu kwenye simu yangu na kuanza upya.
Hasara
ambayo ilinikumba ni pamoja na kupoteza baadhi ya taarifa ambazo zilikua kwenye
simu (Mfano: Contact, Message n.k). Bahati nzuri sana kabla ya kufanya
mabadiliko hayo niliondoa kifaa cha kutunzia vitu vyangu (Memory card) ambapo
baadhi ya vitu vyangu nilifanikiwa kuvirejesha.
Kama
hili limeweza kunikumba mimi na nikaelezea wenzangu wengine tulikua nao kwenye
mkutano – Basi pia linaweza kumkuta mwingine.
Nilicho
jifunza ni kua kulikua na “Wi-Fi – Hotspot” Mbili ambapo zilikua na majina
yanayo fanana. Moja ilipo kua chini (Weak) niliona nyingine iko vizuri.
Kutokana na uharaka, na imani niliyokua nayo nilijikuta nimejiunga na iliyokua
si sahihi bila kujua na hatimae ndio nikajikuta nimeingia mtegoni.
Aidha,
Kituo cha mabasi cha mawasiliano – Nimepata kuambiwa mtu unapokua ukitafuta
huduma ya “Wi-Fi” unapata zisizo sahihi ambozo pia zinakutaka uingize taarifa
zako. Jambo ambalo binafsi nategemea kulifatilia na kujua kama hili nalo lipo
maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment