WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Sunday, 14 August 2016

WAHALIFU MTANDAO WAUNGANISHA NGUVU KUDHURU MABENKI

Makundi mawili makubwa ya kihalifu mtandao yanayo andika program hasidi “Malware” zenye mlengo ya kudhuru mabenki yametangaza kuungana ambapo imezungumzwa kuwa huwenda ndio sababu kuu ya kumepelekea takwimu mpya za mashambulizi dhidi ya taasisi za kifedha kwa Mwezi (4, 2016 – 6, 2016) kuongezeka kwa Asilimia 16 (16%)  kulinganisha na takwimu za Mwezi (1, 2016 – 4, 2016) .

Makundi haya mawili ambayo ni waandishi wa “Nymaim Trojan” pamoja na “Gozi Trojan” katika hatua yao ya kuunganisha nguvu yanatabiriwa kuongeza tishio kubwa la matukio ya wizi wa fedha katika taasisi za fedha duniani kote – Na inatabiriwa makundi mengine yakielekea kufata njia hii ya kuunganisha nguvu ili kuongeza kasi ya kudhuru na kuiba fedha katika Taasisi za fedha.

Nikielezea umuhimu wa wanausalama mtandao kuunganisha nguvu [KATIKA ANDIKO LINALOWEZAKUSOMEKA HAPA] nilionyesha namna ushirikiano wa dhati baina ya wanausalama mtandao unavyoweza kupunguza  uhalifu mtandao duniani kote hasa ukizingatia uhalifu huu unafanyika bila kuzingatia mipaka.

-----------------------------
NOTE: Banking Trojans are often propagated through compromised or fraudulent websites and spam emails. After infecting users, they mimic an official online banking page in an attempt to steal users’ personal information, such as bank account details, passwords, or payment card details.
--------------------------------

Awali, “Nymaim Trojan” ilieundwa kama “Ransomware” ambapo kazi kuu ilikua ni kufungia mifumoya watu  na kudai fedha ili kuifungua. Na kwa sasa baada ya mbili hizi kuungana imeongeza sifa nyingine ambapo kwa sasa imekua na uwezo pia wa kusababisha mtu aliyeko mbali kuweza kutumia mfumo wa mtu mwingine bila ridhaa.


Hatua hii ya kuungana kwa makundi haya mawili ime elezwa kua situ katika utengenezaji bali na usambazaji wa program ambazo zitadhuru kwa kiasi kikubwa taasisi za kifedha. Hadi sasa Gozi iko katika nafasi ya pili kuathiri taasis za fedha huku nafasi ya kwanza ikiendelea kushikiliwa na “Zbot”.

Kumeendelea kua na ushawishi mkubwa wa Zbot kuunganisha nguvu na makundi mawili ya awali ambapo wana usalama mtandao katika ngazi ya kidunia wana hofia hali hiyo ikifanikiwa, taasisi za fedha zitakua katika hali mbaya zaidi.

------------------------
NOTE: If cyber criminals do not succeed in stealing users’ personal data, they will encrypt it and demand a ransom. Yet another example is the Neurevt Trojan family. This malware was used not only to steal data in online banking systems, but also to send out spam.
---------------------------

Kwa mujibu ya Ripoti [INAYOWEZA KUSOMEKA HAPA] iliyo wasilishwa kwa wana usalama mtandao, inaeleza, UTURUKI kushika nafasi ya kwanza katika Nchi zinazo shambuliwa zaidi na virusi vinavyo dhuru taasisi za kifedha ikifuatiwa na URUSI huku BRAZILI ikishika nafasi ya tatu.

Kumekua na utengenezaji mkubwa wa Virusi / Programu hasidi zenye mlengo wa kudhuru mifumo ambapo kasi yake imeendelea kua kubwa zaidi kulinganisha na Mwaka jana. Hali hii inachangiwa na  programu hizi kuingia katika mfumo wa kuduma “ Malware as a service” ambapo huduma hii imeendelea kukua kwa kasi ya kipekee hivi sasa.

Kwa mujibu wa Ripoti, Nchi kuu tatu zilizo ongoza kwa utengenezaji wa program hizi hasidi “Malware” ni pamoja na Marekani (35.4%) ikifuatiwa na Urusi (10.3%) pamoa na Ujerumani (8.9%). Huku katika kila komputa tano (5) -  Moja (1) imekua ikishambuliwa ambpo kampuni ya Kaspersky pekee kwa kipindi cha miezi mine imefanikiwa kugundua mashambulizi mtandao 16,119,489.

Bado tunaendelea kutoa wito kwa taasisi za kifedha kujitazama upya na kuhakiki wanaunganisha nguvu kama inavyo onekana katika makundi ya kihalifu mtandao  Hii ikiwa ni pamoja na kuimarisha mashirikiano katika kubadilishana taarifa za mashambulizi na namna mbali mbali zinazoweza kufanikisha kutatua tatizo huku mahirikiano na mamlaka za udhibiti uhalifu mtandao ukiimarishwa zaidi.


Kinyume na kufanya hivi hali ya uhalifu mtandao itaendelea kushika kasi na upoteaji mkubwa wa fedha katika taasisi zetu z kifedha zitapelekea kuyumbisha uchumi wa mataifa yetu.



No comments:

Post a Comment