Yapo
maeneo mengine ambayo yanaweza kuathiriwa vibaya na uhalifu mtandao – UCHUMI,
ni moja ya eneo muhimu ambalo wahalifu mtandao wanaweza kuliletea athari.
Aidha, Unapotazama kinacho wapelekea wahalifu mtandao kufanya uhalifu moja wapo
ni kujipatia fedha.
Ni
wazi kua Raisi wa awamu ya Tano ana pambana kwa dhati kuhakiki wa Tanzania
wanaondokana na umasikini ulio kithiri ambapo anaendelea kuchukua jitihada na
hatua mbali mbali hadi sasa.
Mfano:
Kumekua na uhimizaji mkubwa wa ukusanyaji wa kodi ki elektriniki – Kwa njia ya
mtandao ambapo amesisitiza anataka aone TEHAMA inatumiwa vizuri katika eneo
hili ili kuhaliki hakuna upotevu wa pesa katika ukusanyaji wa kodi Nchini.
Aidha,
Mabenki yameendelea kuboresha mifumo ya Kimtandao kuhakiki miamala inafanyika
zaidi kupitia mtandao na nikitolea mfano, mabenki Nchini yamekua yaki hamasisha
huduma mtandao kama vile (Huduma za kifedha kupitia simu, kutumia kadi zetu
kufanya manunuzi pamoja na matumizi ya mashine za kutolea fedha “ATM”)
Makampuni
ya simu nayo hayajakubali kubaki nyuma – Yame hakiki yanaingiza huduma
inayoshika kasi zaidi Nchini ya kuweza kufanikisha miamala ya kifedha kupitia
simu zetu (Mobile money) ambapo wana nchi wengi wameendelea kuona huduma hizi
ni rahisi na wengi wanazitumia.
Maeneo mengine nayo yameona huu ndio muelekeo – Mabasi ya mwendo kasi
yamehamasisha miamala kufanyika kwa kadi, huku ulipaji wa bili mbali mbali nao
kuendelea kufanyika kupitia mitandao.
Hali
hii ni nzuri sana – Kitendo cha mtu kuweza kufanya miamala ya kifedha bila
kuhangaika kutoka shemu moja kwenda nyingine kunapelekea uokoaji wa muda na
kuongeza ufanisi kwa tunayo yafanya. LAKINI – Je, Upande wa pili wa shilingi,
kuna jitihada zozote tumechukua kuangazia? Hapa nazungumzia wahalifu mtandao
ambao pia wana uwezo mkubwa wa kupelekea upotevu mkubwa wa pesa
tunazozizungusha mitandaoni.
Ni
mara ngapi tumekua tukiathirika kimtandao kunapo pelekea kupoteza pesa zetu,
bila kujadiliwa kwa sura ya kipekee? Kuna wanao lalama bila kufata taratibu juu
ya kupotelewa kwa fedha, na kuna wanao potelewa bila kujua na pia kuna wanao
dai wametoa taarifa lakini hakuna matokeo chanya.
Taasisi
za kifedha nazo si kweli kua hazi kubwi na kadhia ya upotelewaji wa fedha
kupitia mitandao, Lakini ni Aghalab kusikia haya yakizungumzwa na kujadiliwa
kwa kina.
COSTECH
iliandaa mkutano uliokutanisha watafiti na wana sayansi katika fani mbali mbali
nchini ambapo ulidumu kwa siku tatu – Kutokana na sababu kadhaa, Nilifanikiwa Kushiriki
vikao hivyo katika masaa ma chache ya mwisho pekee ambapo mjadala wa maswala ya
usalama mtandao ulifanyika na mambo mengi ya msingi kujadiliwa.
Kwa
mujibu wa Tafiti zilizo wasilishwa na AARSC kwenye moja ya mjadala, zime eleza asilimia sita (6%) pekee ya tovuti nchini
ndizo zenye ulinzi mtandao unao ridhisha na Asilimia kumi na tisa (19%) zipo katika hatari zaidi ya kuweza kuvamiwa na
wahalifu mtandao.
Aidha,
Asilimia zilizo bakia, sabini na tano
(75%) zipo katika hali mbaya kwa kiwango cha wastani sanjari na kiwango
kidogo – Ambapo pia zinabaki kua katika hatari ya kuweza kuingiliwa na wahalifu
mtandao. Mjumuiko wa takwimu hizi ni pamoja na tovuti za mabenki yetu Nchini.
Muwasilisha
tafiti aliendelea na kusema, Kilicho ikumba benki ya Bangladeshi – Mapungufu yaliyo
patikana yana wiana pia na mapungufu yaliyo patikana kwenye tovuti za kwetu
nchini. Beki ya Bangladeshi iliweza kuingiliwa na wahalifu mtandao na kupelekea
upoteaji wa kiasi kikubwa sana cha pesa. Unaweza kupitia kwa kirefu kuhusiana
na tukio la Benki ya Bangladesh kwa ku “BOFYA HAPA”
Aidha,
kwenye hitimisho la tafiti iliyo wasilishwa iliainisha – Kwa uumla hali ya tovuti
zetu nchini ni mbaya. Kitu ambacho kilinifanya nijiulize maswali kadhaa. Wachangia
mada walitolea mfano shambulizi mtandao la hivi karibuni katika Chuo cha IFM pamoja
na kampuni ya simu ya TTCL.
MASWALI YA MSINGI
Kuna
maswali mengi mtu anaweza kujiuliza, Mfano: Matukio haya ya kihalifu mtandao wa
Tanzania huwa wanajua kinacho endelea? Tatizo hasa liko wapi? Nini kifanyike? Pamoja
na maswali mengine mengi.
Sitaki
kutupa lawama moja kwa moja kwa walio nyuma ya utengenezwaji wa tovuti pamoja
na wasimamizi wake Nchini – Huwenda swala la usalama mtandao bado ni JIPYA
kiasi kwamba inakua vigumu kuweza kufahamu mapungufu ya kinacho tengenezwa
(Tovuti na mifumo mingine).
Au
Inawezekana ikawa kuna changamoto ya kuzungumzia udhaifu tulio nao katika
mifumo yetu kutokana na sababu mbali mbali. Najiuliza, Kama hili ni kweli –
hatuoni tunachofanya ni sahihi hasa ulizingattia Uchumi wa taifa lolote duniani unaweza kuyumbishwa vibaya na
wahalifu mtandao?
Katika kujibu maswali
tunayoweza kujiuliza – Naweza kusema,
Uelewa bado uko chini sana wa maswala haya ya uhalifu mtandao ( Hapa namaanisha
utambuzi, Kujilinda pamoja na hatua za kuchukua tatizo linapo tokea) Hii ni
kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi ngazi ya Kitaifa.
Ni
wazi kuna tatizo kubwa, na hili si tatizo la taifa moja ni tatizo la kibara na
kidunia. Kubwa kuliko yote ni kua tumekua na wadhibiti dhaifu kuliko wahalifu
mtandao na hatuna miundo mbinu rafiki ya kuhakiki tuna tumia rasili mali watu
vizuri kwa kuzitambua na kuhakiki zinabaki upande salama badala ya kuwa wa
halifu. Hii ni moja kuu lakini bado kuna sababu nyingine 11 mbazo katika
nyakati tofauti nimekua niki zielezea.
Kinachotakiwa
kufanyika, Kikubwa ni kua na UTAMBUZI wa changamoto za uhalifu mtandao pamoa kua
na UTAYARI wa kuzitatua na kuhakiki mapendekezo tuliyo kubaliana (wana usalama mtandao
) na kuyapitisha tulipo kutana ijini Johannesburg Nchini Afrika kusini ambayo mataifa mengine sasa yako katika
kuyafanyia kazi nasisi tuna yafanyia kazi kama taifa.
JITIHADA NYINGINE – TEHAMA
Ni
ukweli ulio wazi kua, TEHAMA ina mchango mkubwa sana wa kuondoa umasikini kwa
watanzania – Na bahati nzuri kitabu kilicho zinduliwa mwisho wa mkutano “ICT pathway
to Poverty reduction” kinaelezea vizuri hili.
Katika
utambuzi wa manufaa makubwa ya matumizi ya TEHAMA, Taifa limewekeza vizuri
kwenye maswala ya TEHAMA – Nikitolea mfano michache, naweza kuzungumzia mkonge wa
taifa, Ghala la taarifa la taifa “National Data Centre”, na mifumo mbali mbali yaki
TEHAMA inayotumika katika miamala ya kifedha Nchini.
Aidha,
bado kuna jitihada pamoja na ahadi kadhaa za kuendelea kuwekeza zaidi katika
TEHAMA nchini ili kurahisisha maisha ya watanzania na kuhakiki kila mmoja wetu
ana nufaika kupitia TEHAMA ikiwa ni miongoni mwa vichocheo vya kutupeleka
katika Uchumi wa Kati sanjari na kua taifa la viwanda.
Sekta ya Afya
imeendelea kujikita katika matumizi ya TEHAMA (Mfano: Telemedicine) – Nimetolea
ufafanuzi wa taarifa ya hivi karibuni tuliyo jadili ya changamoto za TEHAMA
katika sekta ya Afya kupitia andiko linaloweza kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA”
ambapo ninaamini kuna mengi tunaweza kujifunza na kuzingatia.
No comments:
Post a Comment