Mswada
wa sheria mtandao nchini Thailand uliwekwa mezani kujadiliwa takriban wiki
kadhaa zilizo pita. Muswada huo ambao ulikua ukingoja kupitishwa kua sheria
umepelekea kelele nyingi Nchini humo ambapo wananchi wake walitaka ufanyiwe
marekebisho kabla ya kua sheria huku wengine wakiukataa kabisa.
Wana
usalama mtandao nchini humo walijaribu kutoa ufafanuzi ambao haukuzaa matunda
na hatimae kutaka msaada kutoka kwa wanausalama mtandao wa maeneo mengine.
Wiki
mbili zilizo pita wahalifu mtandao Nchini humo walitangaza kushambulia tovuti
za serikali ili kushinikiza mamlaka
kufanyia kazi marekebisho ya sheria hizo za mtandao ambazo walidai
hawakukubaliana nazo – Baadae walianza kushambulia tovuti mbali mbali na
kusababisha mtafaruku mkubwa.
Tovuti ya polisi ya nchini humo (Royal Thai Police Office) ni miongoni mwa tovuti zilizo shambuliwa kimtandao ambapo ilidukuliwa na baadae kuangushwa kabisa. Kitu ambacho kilipelekea hasira kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.