Nikitoa Neno la Shukran Pembeni Ni - Abner Abaga (ICT Director - Wizara ya ICT,Kenya) |
Mwishoni
mwa mwezi wa kumina moja (Novemba) mwaka huu (2016) Jijini Nairobi Nchini
Kenya, Nilibahatika kuibuka mshindi wa tunzo ya mwanausalama mtandao
bora wa mwaka (Cybersecurity Expert of the Year) – Ikiwa ni kutambua mchango wangu
mkubwa katika mataifa mbali mbali barani Afrika kuhusiana na swala zima la
usalama mtandao.
Mchango
wangu haujakomea Barani Afika, Nimekua pia nikitoa Mchango katika mataifa
mengine mengi nje ya Bara la Afrika. Kutokana na Tunzo niliyopokea,
Imeniongezea nguvu na hari mpya ya kutumikia fani yangu vizuri kwa manufaa ili
kuhakiki situ tunapata Bara salama bali dunia salama kimtandao.
Kwa
mujibu wa BBC kama inavyo someka “HAPA” – Imeelezea mchango wangu kua chachu ya
kufanya mataifa mengi barani na nje ya bara kua salama. Aidha, kufuatia
mahojiano yango na BBC nilipo ulizwa juu ya safari yangu Nchi Afrika kusini
kuzungumzia zaidi Uchunguzi wa makosa mtandao mabapo tovuti kadhaa zimekua ziki
ripoti Moja wapo ikiwa ni ya ITWeb kama inavyo someka “HAPA” nilieleza ya kua
ifikemahali kila mmoja ajiulize atadhuriwa kimtandao lini na si kujiuliza kama
anaweza kudhuriwa kimtandao.
Kurudi
na Kikombe cha Tunzo nyumbani na mapokezi yake kwenye vyombo mbali mbali vya
Habari vimeniongezea faraja zaidi – Niliendelea kusisitiza juu ya kuhakiki
swala la usalama mtandao halibaki kua la kundi flani la watu, Pia kila mmoja
ana dhamana ya kuhakiki anajilinda binafi dhidi ya wahalifu mtandao.
Aidha, Makampuni
na Taasisis mbali mbali lazima ziwe na vitengo rasmi vitakavyo shughulikia
maswala ya usalama mtandao pamoja na Taifa kwa ujumla kufunga mikanda zaidi
katika kukabiliana na wimbi kumbwa la uhalifu mtandao unao kua kwa kasi.
Wahalifu
mtandao hawalali, na kila siku wanakuja na mbinu mpya za kufanya uhalifu mtandao
– Itashangaza kama wadhibiti (Wanausalama mtandao) watashindwa kuendana na kasi
ya namna mpya za uhalifu mtandao. Ili kufikia hili lazima kila siku kuwe makini
na maelekezo tunayo yawasilisha kutoka maeneo yote duniani juu ya hali ya usalama
mtandao sanjari na gunduzi mpya za uhalifu mtandao.
Mfano,
Kwa sasa Ma benki na Makampuni ya simu ni moja ya maeneo yanayo windwa sana na
wahalifu mtandao na hadi sasa wamefanikiwa kudhuru mataifa makubwa kama Urusi,
Ujerumani , Uingereza na kadhalika. Hivyo Mataifa mengine lazima yajue
kinachoendelea na kuhakiki wana jipanga kudhibiti athari zozote na kama athari zitazikumba basi kuwe na timu sahihi yenye watu sahihi watakao weza kutatua tatizo mara
moja.
Nilipo
hudhuria uzinduzi wa ripoti ya hali ya usalama mtandao kwa baadhi ya Nchi za
Afrika iliyofanyika Serena jijini Dar-es-salaam Nililiona changa moto kubwa ya
kuto ripotiwa matukio ya kihalifu mtandao imeendelea kusababisha twakwimu
sahihi kutopatikana na kufanya utambuzi wa wapi kwenye tatizo zaidi kuto
gundulika – Kwenye hili lazima tubadilike.
Kwa
mujibu wa Ripoti wasilishwa na wazungumzaji mbali mbali nikiwepo, asilimia 91 (91%) ya matukio ya kihalifu mtandao
hayaripotiwi, Kuna mahitaji ya wana usalama mtandao Elfu thelathini (30,000) zaidi Nchini,
hasara ya zaidi ya dola milioni 85 ($85M) imesababishwa na uhalifu
mtandao kwa mwaka huu pekee, huku Eng. Petter wa UCSAF – akieleza ya kua zaidi
ya matukio elfu
moja mia nane (18000) yalijitokeza mwaka jana pekee ndani ya
Tanzania.
Takwimu
hizi si nzuri sana kwa Taifa – Na tunawajibu wa kufanyia kazi ziweze kupata
suluhu. Hivyo tuanze na utayari wa kutambua uhalifu mtandao ni janga, kisha tupange
timu mpya sahihi ya kukabiliana na janga hili na hakika mambo mengine yote
yatafata kwa urahisi zaidi. Aidha nilitoa wito kwenye mkutano huo juu ya mambo
kadhaa yakiwemo kuhakiki tunakua na familia rasmi ya wana usalama mtandao kama
si ya wana TEHAMA kwa ujumla ili kuweza kurahisisha kubadilishana taarifa na
uzoefu. Pia kutambua michango mizuri ya watu ni jambo muhimu sana.
Kua katika fani ya usalama mtandao na kuhakiki
unatumikia fani hii kwa manufa ili mataifa mbali mbali yabaki salama na sio
kuharibu ni jambo ambalo wengi bado limewawia vigumu. Hii ndio inapelekea kua
na makundi makubwa matatu ya wanaofahamu maswala ya usalama mtandao ambayo ni
wale wanaojua na wakadhuru wangine (Whalifu mtandao) , Wanao jua na wakasaidia
watu (Wanausalama mtandao), Na walio katika kundi la kati (Mchana – Wanausalama
mtandao na usiku – Wahalifu mtandao).
No comments:
Post a Comment