WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday, 28 December 2016

WATU 9 WAKAMATWA KWA UDUKUZI WA TOVUTI ZA SERIKALI

Mswada wa sheria mtandao nchini Thailand uliwekwa mezani kujadiliwa takriban wiki kadhaa zilizo pita. Muswada huo ambao ulikua ukingoja kupitishwa kua sheria umepelekea kelele nyingi Nchini humo ambapo wananchi wake walitaka ufanyiwe marekebisho kabla ya kua sheria huku wengine wakiukataa kabisa.

Wana usalama mtandao nchini humo walijaribu kutoa ufafanuzi ambao haukuzaa matunda na hatimae kutaka msaada kutoka kwa wanausalama mtandao wa maeneo mengine.

Wiki mbili zilizo pita wahalifu mtandao Nchini humo walitangaza kushambulia tovuti za serikali  ili kushinikiza mamlaka kufanyia kazi marekebisho ya sheria hizo za mtandao ambazo walidai hawakukubaliana nazo – Baadae walianza kushambulia tovuti mbali mbali na kusababisha mtafaruku mkubwa.





Tovuti ya polisi ya nchini humo (Royal Thai Police Office) ni miongoni mwa tovuti zilizo shambuliwa kimtandao ambapo ilidukuliwa na baadae kuangushwa kabisa. Kitu ambacho kilipelekea hasira kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.





Naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi Mh. Prawit Wongsuwon, alitangaza kukamata washukiwa tisa (9) wa uhalifu huo mtandao pamoja  na vifaa vyao huku akiongeza ya kua serikali ya nchi hiyo haita linyamazia tukio hilo na kusema watachukua hatua stahiki kwa kila atakae thibitika na uhalifu huo.


Tayari kati ya tisa (9) walio kamatwa , Kijana mdogo mmoja amepatikana na hatia huku wengine nane (8) bado wanaendelea kufanyiwa uchunguzi. Kijana aliye patikana na hatia ni Natdanai Khongdee (Umri, Miaka 19) ambapo mkuu wa polisi wa Nchi hiyo Chakthip Chaijinda, alimtangaza mbele ya vyombo vya habari vya Nchi hiyo.


Mkuu huyo wa polisi alisema, Mtuhumiwa amekua pia akiuza bunduki mtandaoni na katika upekuzi walimkuta na Bunduki , Risasi pamoja na bangi. Washukiwa wengine nane bado hawajatajwa majina yao kwa sababu za kipelelezi.

Wizara ya utalii ya nchi hiyo nayo tayari imesha peleka mashtaka kufuatia kuangushwa kwa tovuti yake.

Aidha, Matukio ya udukuzi yameendelea maeneo mengi katika siku chache zilizopita ambapo ukurasa wa twitter wa Sony nao uliingia mikononi mwa wahalifu mtandao na hatimae kuchapisha taarifa za uongo kua Britney Spears amefariki – Ukurasa huo ulifanikiwa kurudishwa  kwa mmiliki halali na kufuta ujumbe huo sanjari na kuomba radhi juu ya tukio hilo.


Huu ni mwendelezo wa matukio ya udukuzi yanayo tokea maeneo mengi ambapo si tovuti pekee bali na kurasa za mitandao ya kijamii ya watu maarufu pamoja na watu wengine wameendelea kuwa wahanga wa uhalifu mtandao.

Mwaka 2017, Bado tunategemea matukio kadhaa ya namna hii kuendelea – Msisitizo wa kuhakiki tunafanyia kazi ulinzi mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi ni jambo linalo sisitizwa zaidi.

1 comment:

  1. Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!

    An Thái Sơn chia sẻ trẻ sơ sinh nằm nôi điện có tốt không hay võng điện có tốt không và giải đáp cục điện đưa võng giá bao nhiêu cũng như mua máy đưa võng ở tphcm địa chỉ ở đâu uy tín.

    ReplyDelete