WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 13 November 2017

UKUAJI WA MATUMIZI YA TEHAMA WAONGEZA UHALIFU MTANDAO

Mataifa mengi yameendelea kuwekeza katika sekta ya TEHAMA ili kurahisisha huduma mbali mbali kwa jamii za mataifa husika – Ikiwa ni pamoja na mawasiliano, huduma za Afya, kifedha na hata usafirishaji ambapo TEHAMA imekua ikitumika kwa kiwango cha juu zaidi tofauti na miaka iliyopita.

---------------------
UPDATE: Apple has addressed a glitch that caused some iPhones to unexpectedly start auto-correcting the letter "i" to a capital "A" and a question mark.
--------------------

Kuwepo na Kinacho tambulika kama “Internet of things (IoT)” ambapo kimsingi ni kila kitu kitakua kimeunganishwa kwenye mtandao kunapelekea kuendelea kukua kwa uhalifu mtandao ambapo madhara yake yanategemewa kua makubwa zaidi ya ilivyo zoeleka.

Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Tumeshuhudia matukio kadhaa ya kihalifu mtandao ambapo mataifa mengi yamejikuta katika hasara kubwa kutokana na mashambulizi mtandao.

--------------------
NEWS UPDATE: A group of researchers and private industry experts, along with DHS officials, remotely hacked a Boeing 757 airplane owned by the DHS that was parked at the airport in Atlantic City, New Jersey.
--------------------


Mategemeo ni kwamba, 2018 – Mashambulizi mtandao yatakua na athari zaidi kutokana na vitu vingi kuunganishwa kwenye mtandao.

Nikizungumza katika vikao vya viongozi wa TEHAMA vilivyo kamilika nilipata kuainisha mashambulizi mbali mbali ya kimtandao kuanzia katika sekta za kifedha, kielimu, Afya, Serikali mbali mbali na hata katika vyombo vya usafiri ambapo magari aina ya “Jeep” pamoja na “Volkswagen” ni miongoni mwa wahanga wakubwa ma uhalifu mtandao.

Aidha, Nili aninisha mambo ya msingi tuliyo kubaliana mapema mwaka huu na kuingiza katika machapisho juu ya namna ya kukabiliana na aina mbali mbali ya matukio ambayo yamejitokeza zaidi kwa kipindi cha mwaka 2016 – 2017.

--------------------
ALERT: Europol boss, Rob Wainright has warned that Ransomware attacks now number as many as 4000 per day, with cybercrime operations large and sophisticated enough to threaten critical infrastructure.
--------------------



Kubwa zaidi nilisisitiza juu ya “Preventing Cyberattacks and Incidence management” – namna bora ya uthibiti wa mashambulizi mtandao na namna sahihi ya kushughulikia matukio ya kihalifu mtandao yanapo jitokeza.



Katika kukabiliana na matukio ya kihalifu mtandao niliainisha hatua saba muhimu zinazotakiwa kufatwa wakati wa kushughulikia mashambulizi mtandao – Huku nikiwahimiza viongozi hao wa juu wa sekta ya TEHAMA kutosahau hatua ya mwisho ambayo ni kufanya mapitio ya kila kipengele pamoja na hatua zilizochukuliwa kwenye kila kipengele.



No comments:

Post a Comment