WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday, 5 January 2018

APPLE YAKIRI KUATHIRIWA NA “MELTDOWN" PAMOJA NA "SPECTRE”

Ugunduzi wa mapungufu makubwa mawili yaliyopewa jina la “Meltdown na Spectre” yaliyoathiri Kifaa cha Kopyuta kinachojulikana kwa jina la“Chip”  ambapo athari zake ni kupelekea wizi wa taarifa kwa watumiaji mtandao umeendelea kuchukua sura mpya baada ya kampuni ya Apple kukiri kua bidhaa zake ikiwemo Komputa za Mac, iPhone na iPads kuathiriwa pia.

Hadi wakati huu ma bilioni ya kompyuta, Simu za mkononi “smartphones” na Tabiti “Tablets” zimeathirika na mapungufu haya ambapo kuna hatari ya taarifa za mabilioni ya watu kuweza kuishia mikononi mwa wahalifu mtandao endapo hatua stahiki kutochukuliwa kwa wakati.



Tayari hatua mbali mbali zimeweza kuchukuliwa kuzuia maafa makubwa kujitokeza kutokana na mapungufu yaliyo gunduliwa ikiwa ni pamoja na kusambaza viraka “Patches” ili kuziba mianya ya mapungufu yaliyo gundulika.


Aidha, Elimu ya uelewa imeendelea kutolewa kwa watumiaji wa mwisho (End user) katika mataifa mbali mbali ili kuweza kuchukua hatua za kusahihisha mapungufu hayo katika vifaa vilivyo athiriwa.

Itakumbukwa – Mwaka Jana Kulikua na ugunduzi wa mapungufu yaliyo athiri program za Microsoft na baadae watumiaji wakashindwa kusahihisha mapungufu hayo kama yalivyokua yamesahihishwa na Microsoft, tukio ambalo lilisababisha uhalifu mkubwa wa kimtandao aina ya “WanaCry” ambapo mataifa Zaidi ya miamoja hamsini yaliathiriwa na mabilioni ya fedha kuingia katika mikono ya wahalifu mtandao.

Kwa kuzingatia hilo, wakati huu imeonekana ni muhimu kuziba mianya hii ambayo tayari imegundulika mapema ili kuepusha wizi mkubwa wa taarifa za watu unaoweza kutokea endapo hili halitochukuliwa hatua stahiki.

Makampuni mbali mbali tayari yamechkua hatua za kusambaza viraka matandao “Patches” na kuwataka watumiaji kufanyia kazi hatua hizi zilizo chukuliwa.

Kumekua na malalamishi kwa baadhi ya watumiaji mtandao ambapo wamedai baada ya kutatua mapungufu yaliyogundulika yamepelekea komputa kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi – Kampuni ya Apple imewathibitishia watumiaji wake kua tatizo hili halitojitokeza kwemye bidhaa zake.

Mapungufu yaliyo gundulika bado hayajasababisha madhara kwa tumiaji – Ingawa Hofu kubwa ni kwamba wahalifu mtandao wanaweza kutumia mwanya wa mapungufu haya kusababisha madhara makubwa siku za usoni endapo hayata fanyiwa kazi mapema.


Angalizo kuu lililotolewa kwa wanaokimbilia kuziba mwanya huu kuhakiki wanakua makini kwani pamegundulika uwepo wa wahalifu mtandao wanao sambaza viraka mtandao “Patches” ambazo sio sahihi na zina mlengo wa kudhuru watumiaji.

Katika hatua nyingine kampuni ya Apple imesisitiza kua mapungufu yaliyo gundulika hayadhuru saa zake maarufu kama “Apple watch” na pia kueleza kua Hadi sasa Kiraka mtandao “Patches” kwa ajili ya Meltdown pekee ndio kimetolewa na baadae watakapo kua tayari watatoa nyingine kwa ajili ya Spectre.


Makampuni mengine ikiwemo Microsoft tayari yamesha toa viraka mtandao “Patches” ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto hii ya kimtandao.

No comments:

Post a Comment