KWA UFUPI: Mifumo ya kimtandao katika baadhi ya wizara za serikali ya Ujerumani ilikumbwa na udukuzi uliopelekea kuibiwa kwa taarifa kadhaa huku baadhi ya vyombo vya habari vimeishutumu Urusi dhidi ya shambulizi hilo la kimtandao. Nae waziri wa Ujerumani wa maswala ya uchumi akieleza hawana uhakika kua Urusi imehusika na shambulizi hilo. Aidha, Urusi imekana kuhusika na shambulizi hilo.
------------------------------------------
Mataifa
makubwa yenye uwezo wa kimtandao yamekua yakishutumiana panapo tokea
mashambulizi mtandao kwenye mataifa hayo. Urusi, Uchina na Korea ya Kaskazini
wamekua wakishtumiwa Zaidi na mataifa ya Ulaya na marekani.
---------------------
TAARIFA: Tume ya TEHAMA ya nchini Tanzania imekaa kikao chake
cha kwanza mahsusi kujadili maswala ya usalama mtandao Nchini ambapo mengi
yalipata kuangaziwa na lengo kuu limekua ni kuhakiki tunapata taifa salama
kimtandao.
---------------------
Ujerumani
Hivi karibuni imekumbwa na shambulizi mtandao katika wizara zake mbili hadi
sasa ambao umepelekea taarifa kadhaa za wizara hizo kupotelea mikononi mwa wahalifu
mtandao.
Wabunge
wa Ujerumani wametupia lawama serikali kwa kutokuwaambia kuhusu mashambulizi hayo
ya mtandaoni huku kamati ya masuala ya dijitali ya bunge la Ujerumani ikiketi
kwa dharura kwa madhumuni ya kuipitia taarifa juu ya udukuzi huo ulio gundulika
Mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2018.
Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya digitali – Anke Domscheit-Berg, kutokea chama cha
mrengo wa kushoto, Die Linke ame eleza ya kua serikali ya ujerumani ilipaswa
kujua mashambulizi hayo ya kimtandao mapema na kuyadhibiti.
@YUSUPHKILEO , Kay Ngalomba @Tigo_TZ and Sheria Maarifa-BoT sharing their views on Legal and enforcement issues....#CybersecurityTanzaniaForum pic.twitter.com/R8GXnuUFn3— ICT COMMISSION (@ict_commission) February 23, 2018
Shirika
la habari la Ujerumani, DPA, lilivinukuu vyanzo vya usalama ambavyo havikutajwa
majina vikisema kwamba kundi la APT28 la Urusi lilidukuwa mifumo ya mawasiliano
ya wizara za mambo ya nje na ndani za Ujerumani na kufanikiwa kuiba taarifa.
Shirika
hilo linasema kuwa mashambulizi hayo yaligunduliwa mwezi Disemba mwaka jana na
inawezekana yalikuwa yakiendelea kwa mwaka mzima.
Thomas de Maiziere. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani |
Kufuatia
ripoti hiyo, wizara ya mambo ya ndani ilithibitisha kudukuliwa kwa kompyuta za
serikali kuu ya shirikisho, ikisema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kwenye
masuala yasiyohusiana na siri za serikali na kwamba yalidhibitiwa.
Hata
hivyo, msemaji wa wizara hiyo hakuweza kutoa undani zaidi wa suala hili,
akisema limo kwenye uchunguzi na kwamba hatua za kiusalama zinaendelea
kuchukuliwa.
Lakini
kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, udukuzi uliachiwa kuendelea hadi
Februari 28 ya mwaka huu wa 2018 ili wachunguzi wakusanye taarifa kuhusiana na
upana, malengo na watendani wenyewe.
"Ikithibitika
kuwa ni kweli, hivi vitakuwa ni aina ya vita dhidi ya Ujerumani," alisema
mkuu wa kamati ya masuala ya dijitali ya bunge la Ujerumani, Dieter Janacek,
kutoka chama cha walinzi wa mazigira, Die GrĂ¼ne, kwa mujibu wa gazeti la
Berliner Zeitung.
Janacek
aliyataja mashambulizi hayo kubwa ni mabaya kabisa, na ametoa wito kwa serikali
kuzifikisha taarifa zote ilizonazo bungeni.
Vikao vya kwanza vya Usalama Mtandao vilivyo andaliwa na Tume ya TEHAMA Nchini Tanzania |
Alipoulizwa
endapo mashambulizi hayo yalifanywa na kundi linaloungwa mkono na Urusi, mbunge
kutokea muungano wa CDU/CSU wa Kansela Angela Merkel, aliutetea mkakati wa
serikali kuzuia taarifa. Stephan Mayer kutoka chama cha CSU alisema
"uchunguzi kamili na wa kina" ulikuwa unahitajika "lakini sio wa
kuwekwa hadharani." Mbunge huyo aliongeza kuwa "kuwadhania vibaya
wengine hakuwezi kuusaidia uchunguzi huo".
Kundi
la APT28 au wakati mwengine huitwa Fancy Bear, ambalo linahusishwa na idara ya
ujasusi kwenye jeshi la Urusi, limewahi kutajwa kuhusika na mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Bunge la Ujerumani
mwaka 2015 na pia ofisi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO na serikali za mashariki
mwa Ulaya.
Brigitte Zypries Waziri wa Nishati na Uchumi Ujerumani. |
Tayari
waziri wa nishati na uchumi wa Ujerumani Mh. Brigitte Zypries amezungumzia shambulizi
hili na kueleza yakua hakuna Ushahidi unaothibitisha ya kua Urusi ndio
imehusika.
Aidha,
Urusi nayo imekana kuhusika na shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment