KWA UFUPI: Wakuu wa vitengo vya TEHAMA wamekutana kujadili changamoto na namna
nzuri ya kuzitatua changamoto hizo katika vikao vilivyo kamilika Nchini Kenya.
-------------------------------
Watunga sera na sheria mbali mbali wamekua wakifanya maamuzi ya TEHAMA bila kushirikisha wadau wa TEHAMA – Hii imekua moja ya changamoto inayo leta mkinzano wa utendaji wenye manufaa kwa wana TEHAMA maeneo mengi barani Afrika.
Mjadala
ulioangazia umuhimu wa udhibiti na uangalizi wa watendaji katika sekta ya
TEHAMA umeonekana kua mzuri ila umegubikwa na changamoto kadhaa kutokana na
ushirikishwaji mdogo wa wadau ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye sekta husika.
Mjadala
huu umejadiliwa kufuatia kuwepo kwa sera mpya nchini Kenya itakayo rasimisha Wana
TEHAMA na kuwataka watambulike kabla ya kuweza kuhudumu maeneo mbali mbali.
Hili litafanana na tulicho nacho nchini Tanzania kwa wanasheria pamoja na
wataalam wa maeneo mengine kadhaa.