KWA UFUPI: TaskRabbit imekua muhanga wa uhalifu mtandao – IKEA, Imethibitisha.
Hii ni katika muendelezo wa Programu tumishi
(Applications) na huduma zingine za kimtandao kuingiliwa na wahalifu mtandao
ambapo taarifa za watu zimejikuta katika mikono isiyo salama.
---------------------------------
TaskRabbit
iliyo anzishwa mwaka 2008 na Bi. Leah
Busque iliyokua na madhumuni ya kutoa ajira zisizo rasmi kwa watu ambapo ilinunuliwa
na IKEA mwaka 2017. Imekua ikitoa huduma zake kwa kujitegemea ndani ya mjumuiko
wa makampuni ya nayo milikiwa na IKEA.
Program
tumishi hiyo imekua ikitumiwa Zaidi na Raia wa Uingereza na maeneo mengine
kujitafutia ajira zizizo rasmi kama kazi za ndani, kazi za bustani na nyinginezo
ambapo wateja wa program tumishi hiyo na huduma za kimtandao zinazo shabiana na
program tumishi hiyo imekua ikikusanya taarifa za watafuta ajira na wanao
tafuta wakuwafanyia kazi hizo.
Mjadala
wa wanausalama mtandao umeeleza taarifa binafsi nyingi za wateja zimekua zikikusanywa
na sasa zimeingia mikononi mwa wahalifu mtandao. Prorgram tumishi pamoja na
tovuti zimefungwa kwa muda kufuatia tukio hili.
Kamishna
wa mawasiliano wa uingereza aamekiri kua na taarifa juu ya tukio hilo na ameeleza
wanalifatilia kwa karibu. Aidha, TaskRabbit hadi sasa imekaidi kutoa ufafanuzi wa
uhalisia wa tukio husika huku ikikadiriwa udukuzi umeathiri kwa kiasi kikubwa
na huwenda umedumu kwa muda.
Kampuni imeeleza
inafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo huku ikewataka wateja wake
kubadili maneno siri (Nywila) na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya uchunguzi
kukamilika juu ya athari Zaidi sanjari na kuwahakikishia wateja wake
walioshindwa kufanya kazi zao kutokana na hitlafu zilizopelekea kufungwa kwa
muda kwa huduma watapatiwa fidia.
NINI CHA KUJIFUNZA?
WAMILIKI WA PROGRAM TUMISHI: Kumekua
na msisitizo mkubwa kwa wanaotoa huduma za mitandao ikiwa ni pamoja na program
tumishi kutakiwa kuhaki wanajipanga kulinda taarifa za wateja wao kabla ya
kuanza kutoa huduma.
Aidha, Kutokana
na wimbi kubwa la wahalifu mtandao kuingiza tarikishi zisizo salama kwenye
program tumishi bila ya wamiliki kua na ufahamu – Tumetoa muongozo mpya wa
kuhakiki wamiliki wanalinda wateja/ watumiaji na endapo itatokea wahalifu
mtandao wakadhuru wakuwajibishwa awe ni mmiliki.
Itakumbukwa
tukio la Uber ambapo mamilioni ya taarifa za watumiaji wa program tumishi hiyo
maarufu kwa kutafutia watu usafiri ilijikuta matatani baada ya kutoa mwanya wa
wahalifu mtandao kuingiza tarikishi zisizo salama zilizo pelekea mamilioni ya
Taarifa kuingia mikononi mwa wahalifu mtandao.
WATUMIAJI WA PROGRAM TUMISHI: Awali
ya yote kila mtumiaji wa program tumishi yoyote anatakiwa kutambua anajukumu la
kutambua faragha yake inalindwa vipi na program tumishi husika.
Kumekua
na nahatua mbali mbali ambazo tumekua tukizichukua kuhaki taarifa binafsi za
watu zinakua salama lakini pia ni jukumu la mtumiaji kufuata maelekezo tunayo
yatoa.
Mfano:
-
Kabla ya kupakua na kuijumuisha program tumishi
katika simu yako, mahitaji yanakuwepo? Na ulazima wakua nayo unakuwepo?
-
Unaifahamu vizuri progam tumishi uitumiayo?
Hususan inachochukua kutoka kwako kabla ya kukupatia huduma?
-
Unatoa ruhusa wa taarifa chache pekee kuenda
kwenye program tumishi au unaipatia taarifa nyingi zaidi zinazo hatarisha
faragha yako?
-
Unatumia Nyila madhubuti na kibadilisha mara
kwa mara kujilinda binafsi?
Pamoja
na jitihada kubwa ambazo tumeendelea kuzichukua – Changamoto kubwa imekua
watumiaji wamekua na uelewa mdogo wa namna ya kujilinda binafsi inayo pelekea
matukio ya faragha za watu kuingia mashakani kutokana na kuendelea kukua kwa
uhalifu mtandao maeneo mengi duniani.
No comments:
Post a Comment