Kampuni
ya Microsoft imetoa angalizo kwa wateja wake ambao bado wanatumia “Window XP”. Kampuni
hiyo imeeleza kuwa hapatakuwepo na “updates” zaidi kwenye “Window XP Service
Pack 3” baada ya mwezi wanne mwaka 2014.
Akiongea
na wataalam mbali mbali wa maswala ya ulinzi mtandao August 16 Mwaka 2013,
Bwana Tim Rains alisema “Ingawa Window XP wakati imetolewa ilikua ni yenye ubora
na yenye kupendwa zaidi, kwa sasa imekua
ni dhaifu kutokana na ongezeko la uhaifu
mtandao”
Aliongeza
na kusema Mara baada ya kuacha kuendelea kuihudumia Window XP wahalifu mtandao
“Hackers” watatumia mianya hiyo kuweza kuingilia Komputa za wateja wao ambao
watakua wanaendelea na matumizi ya Windo XP huku akiendelea kusisitiza Windows
mpya ambazo zimekua ziki endelea kutolewa na Kampuni hiyo Ya Microsoft
zimeendelea kutafutiwa suluhu pale tu inapo onekana wahalifu mtandao wameweza
kugundua namna ya kupenyeza na kuweza kuingia katika Komputa za watu bila
ridhaa yao bodhaa zao za Microsoft.
“Kwa
sasa Microsoft Security Response Center imekua ikotoa “Updates” kwa wateja wao ili
kuwalinda dhidi ya wahalifu wenye nia ya kupenya kwenye komputa zinazotumia
bidhaa zao. Ifikapo tarehe 8 ya Mwezi wa Nne mwaka Huu wa 2013, Makampuni
ambayo bado yatakua yanatumia Window XP wahalifu mtandao “Attackers” wanaweza
kuwa na namna ya kutafuta mapuungufu katika Window XP ambapo baadae wanaweza
kutumia mapungufu hayo kuleta athari na Kampuni ya Microsoft haitakua na
usaidizi wa bure au wa kulipia ndidi ya hali hiyo kwani tayari itakua imekwisha
acha kutoa msaada dhidi ya Window XP” alisema bwana Tim Rains.
Wachangiaji
wa mada hiyo waliweza kuonyesha Hisia tofauti dhidi ya angalizo hilo, Na tulipo
zungumza na bwana Yusuph Kileo ndidi ya Taarifa hiyo alisema, “Naimani kabisa
Tarehe zitafika nabado baadhi ya Makampuni yataendelea na matumizi Ya Window
hiyo ambapo huwenda ikaongeza urahisi wa wahalifu kupenyeza katika mifumo mbali
mbali inayo tumia window Hiyo ya XP ingawa Microsoft tayari wamesha tangaza ya
kua msaada zaidi katika Window XP hautakuwepo na huwenda ikawa ndio sababu ya
wahalifu kuanza kutumia mwanya huo kuingilia Komputa za watu wenye matumizi ya
Window hiyo ya XP”
Aidha
kwa taarifa nyingine, Tarehe 19 Ya Mwezi wa nane 2013 Jijini California Nchini
Marekani Jaji Charles Breyer wa mahakama ya Wilaya jijini humo ametoa hukumu
kwa watumiaji wa mitandao ambao wamekua na tabia ya kubadilisha IP (internet
protocol) au kuwa na matumizi ya “Proxy server” kwa malengo ya kuzingilia
Tovuti nyingine “Public Websites”.
Katika
kesi hiyo iliyo husisha makampuni mawili ya nchi hiyo yaliyo jilikana kama “Craigslist”
pamoja na “3taps” Jaji huyo Alifafanua
kwa kusema mtumiaji anapokua na tabia hiyo atakua amekiuka kipengele cha katiba
ya nchi hiyo kinachojulikana kama CFAA “Computer Fraud and Abuse Act”.
Alipo
ulizwa bwana Yusuph Kileo kuhusiana na tukio hilo alizungumza na kusema
“Kilichotokea katika kesi hiyo ni kwamba 3taps wali ingia kwenye Kampuni ya
Craigslist kwa kubadilisha IP(Internet Protocol) yake na kutumia “Proxy server”
ili kuficha utambulisho wake “Identity” huku wakichukua taarifa kutoka katika
kampuni ya Craiglist ndipo Graiglist
walipo fungua mashtaka dhidi ya kampuni ya 3taps.