Wadukuzi
wa kichina katika utaftaji wa taarifa zihusianazo na mitambo inayo ongozea
makombora yanayotumiwa na wa Israel nchini palestina wamefanikiwa kuingilia
mifumo ya wakandarasi watatu wa ki Israel. Wadukuzi hao wa kichina
wamefanikiwa pia kupata kujua taarifa za mipango mingine yawa Israel pamoja na
taarifa nyingine muhimu za makombora yawa Israel.
Taarifa
hii imekua ikipokelewa kwa namna tofauti na makundi mbali mbali yaliyo onyesha
hisia zao kupitia mitandao huku baadhi wakihoji kama inaweza kuleta salama
katika hali ya mapigano yanayo endelea hivi sasa huko Gaza.
Kwa
mujibu wa taarifa inayosomeka "HAPA", imeelza wadukuzi hoa wana uhusiano wa
karibu na Jeshi la Uchina. Mwezi wa tano mwaka Huu 2014, Marekani ilitangaza
kuwatafuta wadukuzi wa tano wa kichina wakiwashtumu kuingilia mitandao ya
mifumo ya kimarekani. Taarifa hizo hazikuweka wazi ni taarifa kiasi gani
wadukuzi hao walifanikiwa kuzichukua huku ikisemekana taarifa 700 ndizo
zilizochukuliwa na baadae kuaminika huwenda ikawa ni zaidi ya idadi iliyo
tangazwa awali.
Kwa
mujibu wa mtafiti wa Chuo kikuu cha Kalifonia cha marekani bwana. John Lindsay
alipozungumza na "BUSINESS INSIDER" alielezea huwenda udukuzi huo unaambatana
na jitihada za wachina kujifunza zaidi maswala ya mifumo ya kuongozea mitambo
ya kivita.
Wakati
gumzo la Udikuzi huu ukiendelea kujadiliwa, baadhi wamekuwa wakisema ya kuwa wadukuzi
wakichina huwenda walivutiwa na mifumo hiyo yawa Israel ya kuongozea mitambo ya
kivita baada ya kushinda kwakwe mapigano ya mwaka 2012 dhidi ya wapiganaji wa
kipalestina.