Baada ya Mwezi Oktoba
kuisha ambapo kubwa lilikua ni kukuza uelewa juu ya matumizi salama ya
mitandao, Taarifa ya kumalizika kwa mwezi huo inaweza kusomeka "HAPA" Mambo
mengi tuliyo yajadili yameonekana kuangaziwa tena kwenye kongamano la maswala
ya TEHAMA Jijini Cairo Nchini Misri. Muundo wa kongamano hili ulihusisha meza
kuu inayo fungua mijadala na wasikilizaji kuchangia na kuuliza mwaswali pamoja
na kupata njia ya kufikia malengo kupitia mada tofauti tofauti.
Naibu Waziri wa
Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, Katika Meza kuu ya
Mjadala alio husisshwa alipata kuzungumzia jinsi teknolojia ya habari na
mawasiliano inavyo patiwa kipaumbele cha mwishoni na idara za fedha katika
mataifa mbali mbali ingawa ni sekta ambayo ina nafasi kubwa sana katika kuleta
mabadiliko na kukuza kwa haraka uchumi wan chi yeyote kama itatumika vizuri.
Aidha, Kwenye Meza kuu
ambayo Nilikua nimehusika tulipata kuangazia maswala mbali mbali na huku
nikizungumzia kwa kina jinsi usalama mitandao utakapo achwa kupewa kipaumbele
unavyo weza kurudisha nyuma jitihada za dhati za kutumika vizuri kwa teknolojia
ya Habari ili kukuza uchumi wan chi mbali mbali.
Pia nilipata
kuzungumzia umuhimu mkubwa wa kuhakikisha mataifa ya Afrika yanaongeza jitihada
ili kuhakiki Mafunzo yahusuyo usalama mitandao yanakuzwa kwa kasi ili kuhakiika
wataalam wa kutosha wanapatikana na kusababisha watumiao vibaya teknolojia ya
habari na mawasiliano wanaweza kuangazwa kiurahisi na kudhibitiwa kwa manufaa
ya kukuza uchumi wan chi yoyote duniani.
Katika Mkutano Huu
ambao Pia ulihudhuriwa na Mkuu wa
Intel bwana John E. Davies, Kama
anavyo onekana kwenye picha akiwa na Mkuu wa Intel katika Nchi ya Misri,
Sikusita kukutana nao na kujadili maswala mbali mbali yahusuyo usalama mitandao
huku nikitaka kujua jinsi gani Intel inajipanga kuhakiki uinzi mtandao unakua
na nafasi nzuri.
Katika Kunipatia
Majiibu, Nilifarijika kujua ya kua Intel imejipanga kuweka ulinzi mtandao
katika vifaa vyake ambavyo kwa kushirikiana na program za Anti-virus kwa pamoja
zitaimarisha ulinzi wa kina katika Komputa. Alinihakikishia hatua yao hiyo
haita punguza soko la matumizi ya Anti-virus bali kwa pamoja patapatiwa namna
ya kuongeza nguvu ili kukabiliana na wimbi la virusi vinavyo tumwa kwenye Komputa
za watumiaji ili kuleta athar.
Aidha, Kwa Upande wa
Waziri mwenye dhamana ya Sayansi na Teknolojia Nchini Misri, Enginia Atef Helmy
mbali na kuonyewha kufurahi sana kuona mimi nilifanikisha kuhudhuria mkutano
huo alinieleza anajitihada za dhati kuhakikisha panapatikana daraja madhubuti
la kuunganisha Afrika kuanzia kusini hadi kazkazini.
Aliifafanua na kusema
kwa kushirikiana Nchi za Afrika katika maswala ya Tehama na pia kuimarisha
nguvu ya pamoja anaimani kabisa teknolojia ya Habari na mawasiliano ina nafasi
kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika dunia ya kesho. Pia alinieleza kwa kina
ya kua vijana ndio hasa nguvu kazi inayo itajika na dunia ya leo ili kuhakiki
mambo yanasogea vizuri.
Mbali na mijadala mbali
mbali, Pia palikua na matukio yakutia saini makubaliano ya kukuza ushirikiano nanchi
za bara Asia pamoja na mataifa mengine. Palipatikana Ziara maalum ya kutembelea
idara maalum inayo husika na maswala ya ulinzi wa mitandao wan hi ya Misri.
Pale tulipata kujionea shughuli mbali mbali zinazocfanyika kuhakiki Nchi ya
Misri inabaki salama mitandaoni.
Huko mbali na kujionea
mengi na matumizi makubwa ya teknolojia yanavyo tumika kuhakiki Nchi inabaki
salama kiimtandao. Tulipata kuonyeshwa changamoto mbali mbali walizo kumbana
nazo kama taifa na ukanda mzima wa Nchi za mashariki ya kati.
Aidha, Ufafanuzi mzuri
wa namna changamoto zimetumika vizuri kuwa Fursa na kuhakiki mambo yanasogea
tulipata kujizwa. Na pia tulipata kuonyeshwa jia mbali mbali zinazo tumika nan
chi hiyo ili kuhakiki wataalam wa maswala ya usalama mtandao wana zalishwa
ipasavyo ili kuweza kukabiliana na changgamoto za uhalifu mtandao zinazo
endelea kukua kwa kasi. Mengi yalikuua yanafanana na nilicho kizungumza na
kituo cha "MLIMANI TV" ili kutolea ufafanuzi baadhi yam ambo.
No comments:
Post a Comment