Itakumbukwa
katika mkutano uliofanyika mapema mwezi
huu jijini "CAIRO" hofu ya ukuwaji wa
uhalifu mtandao unaoweza kurudisha nyuma uchumi wa mataifa ya Afrika ulipata kujadiliwa kwa kina huku nchi ya Misri
ikionyesha washiriki wa mkutano huo jitihada inayoendelea nayo katika
kukabiliana na uhalifu mtandao.
Ime
ripotiwa na Mtandao wa "MGAFRICA - IN ENGLISH" kuhusiana na kilichojiri katika mkutano
uliokamilika jijini Johannesburg, Afrika kusini wa maswala ya usalama mitandao
ambapo Bara la Afrika limetabiriwa kuwa na ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana
na mikakati daifu ya kujiweka salama huku ikiwapatia wahalifu mtandao urahisi
mkubwa wa kuleta maafa siku za usoni.
Kumeendelea
kuwa na wimbi kubwa la uhalifu mitandao ingawa jitihada za kukabiliana na
uhalifu huo zimeendelea kugharimu
mataifa mengi hivi sasa. Mataifa yamekua yakiwekeza kwenye maswala ya usalama
mitandao lakini bado wahalifu mtandao wameonekana kuendelea kutamba.
Mkutano
huo wa maswala ya usalama mitandao uliangazia
kwa karibu sababu za ukuaji wa uhalifu
mtandao na nini kifanyike kwa mataifa ili kuweza kupiga hatua ya kubaki salama
kimtandao. Wataalam wa maswala Mtandao kutoka katika mataifa mbali mbali walikutana
kuyajadili mambo hayo kama ifuatavyo:-
Swala
la kukuza uwelewa kwa watumiaji mtandao kuhusu matumizi salama ya mitandao
lilionekana bado ni changmoto katika mataifa mengi. Na njia rafiki za kuhakiki
kampeni hii ya kuamasisha uma juu ya matumizi salama ilipelekea mambo mengi
kuangaziwa macho huku "TOVUTI" maalum
kwa ajili ya uelewa wa matumizi salama mitandao ikipata kuzinduliwa.
Sheria
nazo zilionekana kua changamoto kubwa sana barani Afrika. Kumekua na kusua sua
sana kwa sheria mitandao kuanza kufanyiwa kazi huku Wataalam kutoka katika
vyombo vya sharia (Mahakama) wakionyesha hali wanayokumbana nayo katika kutolea
maamuzi dhidi ya uhalifu mtandao.
Tulipata
kufafanua na kueleza usalama mitandao haunabudi kwenda sambamba na sharia zake
maalum zinazopaswa kupitiwa mara kwa mara na kuborehwa ili kuendana na wakati.
Bila kufanya hivyo hali ya wahalifu mtandao kufanya matukio na kutopatiwa
adhabu stahiki itaendelea kuchangia ukuaji wa uhalifu huu.
Swala
la Uhaba wa wataalam nalo halikubaki nyuma. Mjadala mkubwa uliangazia jitihada
mbali mbali za mataifa zinazofanywa ili kuweza kuwa na wataalam wakutosha wenye
uwezo sahihi wa kujua namna ya kudhibiti, kukabiliana na kuzuia uhalifu
mtandao.
Ushirikiano
katika maswala ya usalama mitandao kuanzia ngazi ya kitaifa kibara na kimataifa
ilionekana bado ni changamoto kubwa sana ambayo bado ku safari ndefu kuhakiki
tunafikia malengo. Njia rafiki ya kuhakiki tunakua na utamaduni wa kushirikiana
kuanzia ngazi ya taifa moja moja kabla ya kuvuka mipaka ilisisitizwa kufanyiwa
kazi ili kurahisisha vita dhidi ya uhalifu mtandao.
Wataalam
mbali mbali walipata fursa ya kuonyesha kwa vitendo gunduzi mpya za kisasa
zenye kurahisisha uwezo wa kubaini, kuzuia na kukabiliiana na uhalifu mtandao
ambapo kila gunduzi ilipata kujadiliwa kwa kina ili kuweza kuleta tija dhidi ya
mapambano na uhalifu mtandao.
Mataifa
na vikundi mbali mbali pia vilipata fursa ya kuonyesha takwimu mbali mbali za
maswala ya uhalifu mtandao na njia mbazo mataifa hayo yameendelea kukabiliana
na wimbi kubwa la wahalifu mtandao. Mjadala mkubwa katika kuzikosoa na
kurekebisha jitihada hizo ulipata kuonekana wenye malengo madhubuti ya kuwa na
bara salama kimtandao.
Pali
angaziwa pia vifaa mbali mbali vya kiusalama mitandao ambapo vimeendelea
kutumika ipasavyo kuhakiki uhalifu mtandao unakabiliwa ipasavyo. Huku
pakitolewa baadhi ya vifaa hivyo kwa washiriki ili kuweza kuongeza tija kwenye
mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika mataifa mbalimbali barani Afrika.
Mzazi unafanya kazi nzuri sana
ReplyDeleteUmekua ukiipeperusha bendera yetu vizuri sana kimataifa hasa katika anga hii ya usalama mitandao
Big Up zidisha juhudi mzazi.
Nashkuru sana Mkuu - Mwisho wa siku Ni jukum kuhakikisha Bara zima linapata watu watakao weza kuweka mambo sawa kiusalama.
DeleteKwa Mara Nyingine nimeshukuru sana na Please endelea kupitia na kushauri inapobidi.