Awali
ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya
kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu
mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba
itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli
ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za
usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea
kukua na kubadilika.
Nitaanza
na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa
wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao
kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao
aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita
bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.
Aidha,
Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni
kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila
mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio
ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia
ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.
Tanzania
pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa
faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha
kwa kudalilisha mitandaoni.
Hayo
yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki
wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila
kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa
ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao),
Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki
za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na
mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza
kutambua maeneo athirika zaidi.
Kwenye
hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha
mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama
kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja
au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono
miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na
pongezi ni nyingi sana hadi sasa.
Kuondoa
hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na
wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka
mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na
kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu
niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “
Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka
kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
waliona taifa letu
linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe
kulipaswa kua kwa muda mfupi.
Nimepata
kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo
nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -
MOJA,
hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze
kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua
mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu
ya sharia hizi mtandao.
Uchunguzi
wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa
hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu
kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya
sababu ya uhalifu mtandao.
Uchunguzi
wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa
darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki
vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao
unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila
kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki
katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza
kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.
MBILI,
kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata
kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika
kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua
kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya
kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna
kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii
inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao
katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali
za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa
kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.
TATU,
Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao
kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya
uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu
kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si
kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio
wa kwanza.
Mimi
nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo
potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari
za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha
zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu
kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa
zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu
zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa
kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha (
Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.
Ikumbukwe
athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na
kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi
wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea
wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua
mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza
kufikia malengo ya kudhibiti.
Wabunge
walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika
mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka
udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza
kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.
Naomba
tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye
hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu
mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria
nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo
nazo. Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na
kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya
uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani
kama si muhusika.
Kileo umenifurahisha sana na maelezo yako mazuri, Uwezo wako wa kuelezea umedhihirisha kua ni mkubwa sana mtaalam wetu! Your brother Johson Kimeri Nipo Shinyanga.
ReplyDeleteNashkuru kwa Maoni yako Kimeri.
DeleteHellow Kileo, ni dhairi kwamba ungeupitia huu mswada nadhani ungegundua una mapungufu mengi sana. Moja ni mambo mengi hayana tafsiri halisia ya kinachotegemewa kifanyike na mswada huu. Pili kuna vitu vimechukuliwa kwenye sheria za nchi nyingine ambazo hazitaweza kutekelezeka katika mazingira yetu. Tatu huu mswada ulitakiwa utafsiriwe na wataalam wa mambo haya kwa wana sheria ili ukae kwenye lugha ya kisheria na uweze kufanya kile kinachotegemewa au tarajiwa. Na mwisho ningependa kushauri tu kuwa na sheria bila kuwa na uwezo wa watu wenye uwezo wa kitaalamu wa kuyaweka yale yanayosemwa kuwa ni makosa ya kimitandao kuonekana makosa haitatusaidia kufikia malengo tunayoyatarajia huu mswada kuyafanya. Nchi kubwa duniani zilizoendelea wana hizi sharia na mafanikiao yake yamewezeshwa na uwezo wa kitaalamu wa kupembua na kuyabaini makosa hayo na si kwa kuwa na sheria tu.
ReplyDeleteKwanza kabisa nashkuru kwa maoni yako - Labda naomba nikujulishe tu kua mimi binafsi Fani yangu halisi ni usalama mitandao na uchunguzi wa makosa ya kidigitali ambapo nimesomea katika ngazi ya degree na baadae kuongeza ujuzi katika ngazi ya Masters. Nimetangulia kulisema hili kutokana na sababu kwamba sheria mitandao ni moja ya vitu nimevipitia na moja ya mitaala niliyo itumia nimesha ileta nchini ili kuweza kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuwaongezea uwezo wataalam wetu.
DeleteKama umekua ukifatilia kwa karibu nimekua niki himiza sana sheria kuambatana na uelewa kwa wananchi juu ya sheria hizo pamoja na kuwaongezea uwezo watu wetu wanaoshughulikia makosa haya kuweza kwanza kabisa kuzitafsiri sheria hizi na kujua namna ya kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo stahiki wa kuziendea kitaalam maana hii ni fani na ina taratibu zake.
Lakini pia nimeanisha kwa kina sana kuwa - Siku zote Hofu kubwa inatakiwa iondoe Hofu ndogo ( Uhalifu mtandao una athari kubwa sana kwa taifa na dunia kwa ujumla hasa hapo baadae) hivyo kuwepo na sheria hizi zitasaidia kuweza kudhibiti na kutoa fursa ya kuhimili vishindo vya uhalifu huu.
Aidha, Nisistize tu kua Uhalifu mtandao Duniani kote unafanana na ndio maana unaitwa BORDER LESS CRIME - UHALIFU USIO NA MIPAKA. hivyo sheria kufanana na nchi nyingine sioni tatizo.
Mwisho kwa swala la kupitia - Nimepitia na mapungufu ya kibinaadam ya kawaida ya kimaandishi ( Mfano Kutaja Kiwango cha chini bila kutaja kiwango cha juu cha mtu kuwekwa ndani) hayawezi kunifanya nione haufai . . . Na hii ndio maana tunasema Sheria mitandao zinapitiwa mara kwa mara na kuboreshwa kutokana na ukuaji wa teknolojia una ambatana na mabadiliko ya teknolojia inayopelekea mbinu mpya za uhalifu mtandao kufanyika ( Sheria zilizo wasilishwa sasa sio fixed through out life time).
Kama kuna maeneo unadhani ni ya kuweka sawa ya kimaandishi - Hili litafanyiwa kazi kwenye review.
Ahsante sana.
Binafsi maelezo uliyoyatoa Kileo Ni mazuri na kuwatoa wadau hofu juu ya wataalamu. Naomba kwanza ku-declare interest kuwa Mimi Ni Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dodoma katika College of Informatics and Virtual Education. Baada ya kuona changamoto zinazoikabili nchi juu ya wataalamu WA kulinda mitandao yetu tulianzisha degree ya BSc. In Computer and Information Security toka mwaka 2008/2009 na mpaka sasa tunao vijana WA kitanzania wengi ambao wamemaliza katika fani hiyo na kwa kiasi Fulani wanaendelea kusaidia nchi katika idara mbali mbali ikiwemo usalama WA taifa, jeshi, polisi n.k na kwasasa tupo kwenye mchakato kutoa Masters in Information Security and Assurance ambayo PIA inachukua vijana wengi wengi WA kitanzania na hivyo kusaidia kujenga vijana wetu wenye ujuzi WA kutosha.
DeleteMwisho, sheria hii naona imechelewa Kuja na sisi kama wataalam tunaiona hii Ni hatua kubwa. ILA wazi lililotolewa na mdau juu ya kushirikisha watu WA sheria na nadhani lilikuwa zuri na naamini wameshirikishwa ili kutoa tafasiri za kisheria hasa utekelezaji ukianza.
Mimi nadhani hapa Tanzania ilipofika ndipo hasa pa kuanzia,kama mtaalamu anavyosema ni muhimu kuangalia kuweka sheria lelemama ili watu waogope kutumia teknolojia kwa vile kuna watu wanaotaka kuendelea kuiba na kutukana watu na kuweka picha za ngono?au kuweka sheria ngumu ila kila anayetumia mtandao kuwa na uoga wa kufanya uhalifu kupitia mtandao.
ReplyDeleteLa pili ni serikali iwaambie wananchi kuwa ina wataalamu wangapi na kama wapo vifaa vipo ?au ni ujanja wa kuwapa watu kesi za mtandao na kuchukua muda kufanyiwa uchunguzi?Je majaji nao wanajua kuhusu hizi kesi?je wanasheria wanajua?
Ni nini unachofanya sasa hivi kama mtaalamu kuhakikisha wananchi wanaepuka kufanya makosa kwa kutokussudia?
kwanza nashkuru kwa maoni yako.
DeleteNatambua kuna Uhalifu mtandao unafanyika pasi na kusudia.
Nimesha andikia mara kadhaa kuhusiana na concern yangu ya AWARENESS PROGRAM pamoja na maboresho yake kwani iliyopo sasa inahitaji Improvement kiasi na msisitizo zaidi.
Aidha, mimi Binafsi nilisha endesha mafunzo kwa wachunguzi wetu wa makosa mtandao nchini kuhakiki kunapatikana uwezo mzuri wa kukabiliana na uhalifu huu - Point hapa ya msingi ni kwamba natambua kuna mahitaji ya Capacity building kwenye hili ( Hasa ukizingatia ni Kitu kipya bado kwa wengi)
Nashkuru sana kwa mchango wako.
Brother Kileo,
ReplyDeleteShukran kwa ufafanuzi mzuri na natumai kwa watu watakao pitia jinsi ulivyofanya uchambuzi huu nadhani wataelewa na kuona manufaa ya Sheria hii kwa wakati huu na ujao, kwani kasi na ukuaji wa watumiaji wa mtandao unazidi kukua kwa kasi sana. Hivyo natumaini sheria hii inasaidi kwendana na kasi hiyo ili isilete madhara ambayo tunaweza kuyaepuka.
Nashkuru sana Salum Kwa maoni yako.
DeleteAhsante.
Wewe unaishi Tanzania?Haya yote unayosema ni kwenye vitabu lakini mahakama na vyombo vyote vilivyopaswa kuwa vya haki nchini havifuati hivyo ukiwa na pesa ndio utanunua haki.!
ReplyDeleteMimi Ni Mtanzania na Baada Yakupata Elimu yangu Nje - Nimesha rudi Tanzania Mkuu.
DeleteHili la Kununua haki, Ni mapungufu yapo kila mahali na si tu kwamba litakuwepo kwenye sheria hizi mtandao pekee.
Ahsante sana kwa Mchango wako.
Asante sana Ndg Kileo.
DeleteMimi ningeshauri pamoja na sheria elimu itolewe kuhusu hatari za mitandaoni, kwani mtandao unaunganisha dunia kuwa kama kijiji.Kwa mfano wengine wanatoa program za bure kama 'antvirus' je tutajuaje kama hizo programs ni salama au la. Kwani Watanzania wengi hatuna ufahamu wa kutosha juu ya hizi progams.
nasjkuru kwa maoni yako.
DeleteNachoweza kusema tu ni kua kubwa ambalo limekua tukilipigia kelele sana katika vikao vyote vya kiusalama mitandao maeneo yote hili la Awareness ni namba moja na pia kuna mengine mengi tu ya kufanyiwa kazi ili kufikia malengo.
Ahsante.