Taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” ilitolea ufafanuzi wa Nchi ya India inavyo pambana ili
kuweza kufikia malengo katika kuboresha usalama mitandao hasa katika wizi
unaofanywa kupitia ATM. Na baada ya kupata kutolea ufafanuzi muswada
wa sharia mtandao, taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” Ilifafanua yamuhimu kuzingatia
ili sheria hiyo iweze kupelekea kufikiwa kwa malengo kusudiwa ya kupata Tanzania
salama kimtandao na kupunguza wimbi la makosa mtandao nchini.
Baada
ya hayo nilipata kuhudhuria mikutano kadhaa katika nchi mbali mbali ambapo
nilifanikiwa situ kuwasilisha mada kwa wataalam wengine wa maswala ya usalama
mitandao bali pia kujifunza mengi kutoka kwao katika maswala mbali mbali ya
msingi ya kufanyiwa kazi ili kuweza kuboresha usalama mitandao situ katika ngazi
ya kitaifa bali na kibara pamoja na Dunia
kwa ujumla.
Makubwa
matatu ambayo nimeona niyazungumzie leo ni pamoja na kuhakiki kuna njia
madhubuti na zenye mpango stahiki za kukuza ulewa kwa watumiaji mitandao jinsi
ya kujilinda na kulinda wengine watumiapo mitandao, Kuhakikisha Taifa linakua
na mikakati endelevu ya kutengeneza na kuongeza uwezo wataalam wa maswala ya
usalama mitandao pamoja na kupatikana na ufumbuzi wa kudumu wa kukabiliana na
wimbi la wizi wa fedha kupitia mashine za ATM.
Nilipokua
Nchi KENYA nilipata kuwasilisha mada mbali mbali pamoja na kuwa na mazungumzo
na washiriki mbali mbali nchini humo kuhusiana na nini kinacho kwamisha
kufikiwa kwa malengo ya program zinazofanywa zenye malengo ya kukuza uelewa wa
matumizi salama ya kimtandao.
Katika
hili – Nimeona tatizo kubwa ni kuwa na udhaifu mkubwa katika maandalizi na
ufahamu wa namna ya kuwasilisha program zenye malengo ya kukuza uelewa wa matumizi
salama wa mitandao. Ili kujua hili kuna taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” itakayoweza
kutoa yakuzingatia wakati wa kuandaa program za kukuza uelewa wa matumizi
salama ya mitandao “Awareness program”.
Nchini
ZIMBABWE, Kubwa nililoliona nila jitihada za kuhakiki Bara la Africa linakua na
tabia ya kukuza wataalam wake ili kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali
za kiteknolojia huku suluhu ya wizi wa fedha kupitia ATM ni muhimu kuangazikwa
kwani wizi huo umekua ukisababisha kuyumba sana kwa uchumi. Hili lilionekana
pia katika mkutano mwingine wa Kenya kama taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” inavyo
fafanua.
brother nimekuandikia katika page yako ya Facebook
ReplyDeleteNaomba unijibu ni muhimu sana.
Ahsante.